Mmiliki kiwanda cha tomato ‘feki’ mbaroni

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mmiliki kiwanda cha tomato ‘feki’ mbaroni


na Dina Ismail


amka2.gif
HATIMAYE Jeshi la Polisi mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, limefanikisha kumtia mbaroni mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha tomato zinazodaiwa kuwa ni ‘feki’ kijulikanacho kama Rozana kilichoko Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Habari ambazo zilizopatikana jana kutoka katika vyanzo vyetu vya habari zimeeleza kuwa mmiliki wa kiwanda hicho anatambulika kwa jina Swalaa Ahmed, mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam, na alikamatwa Jumapili maeneo ya Feri Kigamboni akiwa na lita 150 za tomato hizo.
Imeelezwa kuwa Swalaa ambaye kiwanda chake huzalisha tomato hizo amekuwa akifanya biashara ya uzalishaji wa tomato hizo kupitia kampuni ya Rozana ambayo haina kibali cha kuzalisha wala kuuza bidhaa hiyo.
Habari zinaeleza kuwa mara baada ya kukamatwa kwake alipelekwa katika kituo cha Polisi Kati ambako aliswekwa ndani kwa saa kadhaa kabla ya kuwekewa dhamana na ndugu zake.
Tanzania Daima ilipowasiliana na Meneja Kanda ya Mashariki wa TFDA, Agnes Kijo, kupata uthibitisho kuhusu habari hizo ambapo alikiri kukamatwa kwa Swalaa na kusema kwamba uchunguzi dhidi ya tukio hilo bado haujakamilika.
“Kweli tumepokea taarifa juu ya kukamatwa kwa mtu huyo lakini kwa sasa naomba nisiongelee sana suala hilo kwa sababu bado lipo mikononi mwa jeshi la polisi, lakini mbali na hilo uchunguzi wake bado haujakamilika,” alisema Kijo.
Akithitibisha madai ya kukamatwa kwa mtu huyo, kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Ilala, Faustine Shilogile, alisema ni kweli jeshi lake kwa kushirikiana na wananchi wameweza kumtia mbaroni Swalaa akiwa katika harakati za kuusafirisha mzigo huo (tomato) kwenda kwa wanunuzi wake.
“Kwa sasa siwezi kuthibitisha kama ni kweli anazalisha tomato feki au la kwa sababu bado tuko kwenye uchunguzi kwa kushirikiana na mamlaka husika yaani Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Bora Nchini (TBS). Sasa baada ya hapo nitakuwa na kauli ya kwamba tulichokikamata ni feki ama si feki,” alisema.
Alisema endapo itafahamika kama Swalaa alikuwa akizalisha tomato feki atachukuliwa hatua kali ya kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
Yaani baadhi ya vitu tunavyolishwa na hawa wamiliki wa viwanda feki ni Mola tu ndiye anayetulinda kutoka kuugua magonjwa ambayo hata majina yake hayafahamiki...............................
 
Back
Top Bottom