Wana MMU habarini za leo,
Kuna jambo linanitatiza na kuniumi za nataka kusema lakinia naogopa mlengwa atalipokeaje jambo hilo mmh naogopa kuitwa mbeya mie maana wanawake hatunaga vifua vya kuvumilia maumivu.Nina rafiki yangu ambaye ana date na kaka flani hivi for more than a year now mkaka anaonyesha ana mcare na kujifanya yuko muwazi kwake kwa kila kitu.
Wakati wanaanza mahusiano mkaka alimwambia ukweli kuwa alikuwa anaishi na mwanamke na wamezaa ila hawakuoana na wametengana kwa muda huo kila mtu anaangalia maisha yake so my friend akaona sio mbaya coz hata yeye alikuwa single na mkaka ni kweli alimvutia wakaamua kuanza mahusiano.Shida imekuja juzi katika pekuapekua yangu ya kimitandao nimegundua yule kaka ameoa ndoa ya kanisani na still wanaishi na mkewe though mke yuko mkoa mwingine kikazi.
Evidence ninazo kuanzia picha za ndoa mpaka picha ambazo alikuwa anapiga na mkewe kipindi hiki ambacho alikuwa anaenda kumtembelea na kumuongopea shosty yuko safarini wana MMU hebu nisaidieni nifanyeje roho inaniuma coz naona kabisa shoga angu anapoteza muda ila je nikimwambia atalipokeajee? Hatoniona mimi mnafiki nataka kuwagombanisha na kuharibu furaha yao?
Maana shosti anamwamini vibaya sana huyu mkaka and kila mara anamsifia a guy is so muwazi and mkweli.