Amini nawaambieni kama awamu ya tano ingeendelea hadi leo hakuna ambaye angepata auheni ya maisha.
Muone Mexence awamu ile alivyopata misukosuko kutwa kucha mahakamani leo sero kesho wapo nyumbani mlangoni wakiwatafuta wahusika wa JF…
Labda siku moja Mello atusimulie jinsi wahusika wa Jamii forums walivyokuwa wanasakwa nyumbani kwake akilazimishwa awataje kwa majina na wapi mnapoishi.
Serikali ilibuni mbinu zote hadi kulazimisha mitandao ya kijamii Kusajiliwa na TCRA hata makali ya JF yalipungua siri nyeti zikawa hazifiki humu kutokana na sheria ya habari na ile ya mawasiliano.
Ukweli ni kwamba hizi kelele kama Rais Samia angekuwa na roho ile hakuna ambacho tungefanya kama alivyofanya Meko.
Meko hakuipenda mitandao ya kijamii hata kidogo, aliichukia JF kuliko umasikini, tumshukuru sana Mello kutokuwa dhaifu kama angekubali kutoa server nusu ya watumiaji humu mngekuwa mapengo kama si vibogoyo.
Ilikubidi Ili uwe whistleblower ilikupasa uwe nje ya nchi ndipo uiseme Serikali vinginevyo Jela na kesi ya uhujumu uchumi ingekuhusu remember Tito Magoti.
Awamu ya sita tunapumua wote tuna midomo mirefu kama chupa kila siku lawama. Samia atapita atakuja mwingine wa kuwabana makende ndiyo mtaanza kumkumbuka. Uzuri wa Samia kama Kikwete matusi ya kila aina akaenda zake kawaachia Meko.
Awamu ya sita tunapumuaaaa, Asante kwa kuheshimu Uhuru wa vyombo vya habari.