Mmepata furaha na amani awamu ya 6

Mmepata furaha na amani awamu ya 6

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2014
Posts
923
Reaction score
1,101
Amini nawaambieni kama awamu ya tano ingeendelea hadi leo hakuna ambaye angepata auheni ya maisha.

Muone Mexence awamu ile alivyopata misukosuko kutwa kucha mahakamani leo sero kesho wapo nyumbani mlangoni wakiwatafuta wahusika wa JF.

Labda siku moja Mello atusimulie jinsi wahusika wa Jamii forums walivyokuwa wanasakwa nyumbani kwake akilazimishwa awataje kwa majina na wapi mnapoishi.

Serikali ilibuni mbinu zote hadi kulazimisha mitandao ya kijamii Kusajiliwa na TCRA hata makali ya JF yalipungua siri nyeti zikawa hazifiki humu kutokana na sheria ya habari na ile ya mawasiliano.

Ukweli ni kwamba hizi kelele kama Rais Samia angekuwa na roho ile hakuna ambacho tungefanya kama alivyofanya Meko.

Meko hakuipenda mitandao ya kijamii hata kidogo, aliichukia JF kuliko umasikini, tumshukuru sana Mello kutokuwa dhaifu kama angekubali kutoa server nusu ya watumiaji humu mngekuwa mapengo kama si vibogoyo.

Ilikubidi Ili uwe whistleblower ilikupasa uwe nje ya nchi ndipo uiseme Serikali vinginevyo Jela na kesi ya uhujumu uchumi ingekuhusu remember Tito Magoti.

Awamu ya sita tunapumua wote tuna midomo mirefu kama chupa kila siku lawama. Samia atapita atakuja mwingine wa kuwabana makende ndiyo mtaanza kumkumbuka. Uzuri wa Samia kama Kikwete matusi ya kila aina akaenda zake kawaachia Meko.

Awamu ya sita tunapumuaaaa, Asante kwa kuheshimu Uhuru wa vyombo vya habari.
 
Meko hakuipenda mitandao ya kijamii hata kidogo, aliichukia JF kuliko umasikini, tumshukuru sana Mello
Sii kweli kuwa aliichukia sana jf, aliipenda sana JF na humu alikuwa anaingia mwenyewe, akitusoma na kutekeleza maoni yetu kimya kimya!. Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic

Mfano mzuri ni hoja ya vikao vya CCM Ikulu tuliibua humu, kwanza akatujibu, na kuwaambia CCM ikulu ni yao, lakini mwishowe akabadilika!. Pongezi Dkt. Magufuli kutenganisha shughuli za Chama na Serikali, Utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!

P
 
*****. akili za kibongo na kindezi hizi.

Nchi iko gizani, hakuna maji ya kunywa, bei juu afu mtu bado anafuraha?

Utakuwa mlamba asali wewe sio bure.
Mkuu kwa nini unakaa gizani?Washa hata mshumaa.Na kama maji ya kunywa ni bei juu,kunywa hata soda.Na hata ukitaka kulamba asali,kwa nini usiagize ile ya Tabora au Itigi?Ni nzuri sana si kwa kulamba tu.Hata ukipaka kwenye kipolo cha ugali kinakuwa kitamu sana.
 
Na wewe utakuwa so called mnyonge, tafuta pesa uache makelele ya maji na umeme
Kwa hii shida unataka unilazimishe kufurahi?

Kwanza mwaka huu umeona Tanzania tunazidiwa na Burudi ? Yaani Burundi wanafuraha kuliko sisi.
 
Bora umeamka salama, ingekuwa awamu ile ungeamkia kuzimu kama siyo jera. Pia tafuta pesa ili bei ya mchele isiwe ishu kwako
Niamkie kuzimu au jela kwani mimi fisadi?
Kwani mimi vyeti feki?
Kwani mimi mpiga madili ya wizi?
Kwani mimi ni mzembe kazini?
Kwani mimi mpenda shortcut?
Mwani mimi muuza unga?
 
Niamkie kuzimu au jela kwani mimi fisadi?
Kwani mimi vyeti feki?
Kwani mimi mpiga madili ya wizi?
Kwani mimi ni mzembe kazini?
Kwani mimi mpenda shortcut?
Mwani mimi muuza unga?

Kambale aliwafunza chuki…. Tito magoti alikuwa na kosa gani.
Lwajabe muhasibu pale Wizara ya fedha alikosa nini…?
Azory mwandishi hoehae alikuwa na tabu gani….?

Mello tukumbushe yaliyokusibu kaka…. Awamu ile.
 
Sasa tuhakikishie Kama wewe sii mmoja wa unaewatafuta wanaJF pengine Hata kung'ata vidole kwa hasira ukiisikia JF na Melo,Kwani bado yapo mengi ya kupazia sauti ikiwa ni pamoja na Sheria za mwendokasi/hati za dharura na kukosekana uzingativu wa Katiba yetu🚶
 
Back
Top Bottom