Mmegombana Akasema anaenda kwao Mpe nauli, na usimfuate wala kumtumia nauli ya kurudia.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Bila shaka mpo kwema!

Vijana, ukiona upo na mpenzi, mchumba au mke ambaye mkigombana kidogo analeta vitisho vya kitoto. Wakati mtu mzima hatishiwi Nyaya.
Mmegombana alafu ati anajikusanyisha mabegi yake na kutaka kuondoka, au anapenda kujisemesha kuwa naondoka! Naondoka! Sijafukuzwa kwetu!
Mpe nauli haraka, ikiwezekana mpe na vipeto cha mchele mwambie akawasalimie huko.

Muda wa kubembeleza mtu mzima kwa mambo ya kipuuzi usiwe nao.

Kijana, ikiwa mkeo au mchumba wako kila mkigombana basi mambo yenu anayatoa kwa Watu iwe kwa wazazi, ndugu, rafiki zake. Fukuza huyo haraka. Hivyo ndivyo Watibeli tunavyofanya.

Kuachana kupo tuu. Tena kuachana na mtu mpuuzi ni upesi zaidi na wala usifikirie mara mbilimbili.

Unaweza kukosea kuchagua mke lakini kamwe usikosee kushindwa kufukuza mke asiye sahihi kwako.
Ni kweli ulikosea lakini hiyo haimaanishi ulinde makosa yako kama mjinga.

Mwanamke akiwa mjuaji, fukuza.
Mwanamke akiwa hana adabu, fukuza
Mwanamke akiwa anajifanya ati yeye yupo na wewe kimakosa yaani umembahatisha, Fukuza.
Mwanamke anayejifanya anasikiliza kwao kuliko kukusikiliza wewe, Fukuza.
Mwanamke anayependa Dini kuliko wewe, Fukuza.
Mwanamke ambaye yupo tayari kugombana na wewe kisa familia yake(kwao), Fukuza.

Mwanamke anayejifanya anataka kuwa mbele yako kwa kujfanya anajua sana, Fukuza.
Mwanamke anayetaka ujali watoto au anayewatumia watoto kama kinga pale anapofanya makosa yake, Fukuza.

Mwanamke ambaye anataka umjali sijui mtoto wake aliyempata kwa mwanaume mwingine kama ndio kigezo cha wewe kuishi naye, Fukuza.

Mwanamke anayetaka kukupimia michezo ya ndani na kukuletea visheria mshenzi visivyo na kichwa wala miguu. Fukuza.

Mwanamke hatakiwa kukupa sheria hata moja. Nasema, hata moja. Narudia, hata moja.

Kuna vile visichana ambavyo ati vinakupa sharti fulani ati ukilifanya ndipo anakupa kitu fulani. Watibeli hatupewi masharti ya kijinga.

Kama demu hataki, aseme sitaki. Full stop.

Mwanamke hatakiwa kukusubirisha. Ati akuweke hapo kama jinga fulani lisilo na kazi za kufanya.. Fukuza au piga Chini.

Mwanamke akikuambia yeye sijui ni wagharama, hivyo unatakiwa ugharimike. Piga chini. Hakuna mwanamke wa gharama. Hizo kauli wanaambiwa wanaume waliodharaulika. Na ukiona Mwanamke anakuambia hivyo jua hajakukubali au wewe sio type yake. Jiongeze!
Hao wanaojiita wagharama na ghali Watibeli tunapiga bure kabisa na hawakohoi. Na wakizingua wanajua nini tunawafanya..

Mwanaume wewe ni mtawala. Mwanamke ndiye anatakiwa akutumikie na wewe sio ujitese kwaajili yake.
Mwanamke aliumbwa na yupo kwaajili yako na sio wewe kwaajili yake. Usiwe Mpumbavu.

Akitishia kuondoka, nenda kwa rafiki yako, mkope kama huna pesa, kisha mpe nauli huyo Mwanamke mwambie aende salama.

Alafu uone kama kuna panya yeyote atakuchezea.
Mwanaume usiuendekeze moyo na kulialia kijinga kisa vitu vya kipuuzi.

Mwanaume unatakiwa ugombaniwe na wanawake na sio ugombee Mwanamke kama jinga au mwanaume mkiwa usiye na sifa.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ilinitokea enzi za ujana bi dada mmoja ilikuwa kila tukikwazana anakimbilia aidha kwenda kwao ama kutishia kwenda kwao.

Ilitokea siku moja tukazinguana akasepa. Kawaida ilikuwa namfuata kumbembeleza. Safari hiyo sikumfuata nikaa kimya.

Baada ya muda akawa anatuma rafiki yake aje kuangalia kama nina mtu.
Kilichotokea yule rafiki yake ndio akawa mtu mwenyewe.

Alipokuja kuamua kurudi alikuta rafiki yake ndio mwenye nyumba.
Akatoka kuwa main chic mpaka side chic kwa upumbavu wake.
 
Hii ilikuwa safi sana
 
impressive comeback 😁
 
Leo naona umeanza kurudi kwenye nondo zako sio ule upupu uliokuwa umeanza, kile sio kitengo chako mkuu
 
Ilinitokea enzi za ujana bi dada mmoja ilikuwa kila tukikwazana anakimbilia aidha kwenda kwao ama kutishia kwenda kwao.

Ilitokea siku moja tukazinguana akasepa. Kawaida ilikuwa namfuata kumbembeleza. Safari hiyo sikumfuata nikaa kimya.

Baada ya muda akawa anatuma rafiki yake aje kuangalia kama nina mtu.
Kilichotokea yule rafiki yake ndio akawa mtu mwenyewe.

Alipokuja kuamua kurudi alikuta rafiki yake ndio mwenye nyumba.
Akatoka kuwa main chic mpaka side chic kwa upumbavu wake.
Wewe ni malaya,Watibeli hawageuzi main chick to side chick.Ukipiga chini piga mazima acha umalaya
 
Back
Top Bottom