mme wa kwanza akishajitambulisha basi.

mme wa kwanza akishajitambulisha basi.

No matter

Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
60
Reaction score
10
hi jf, rafki yangu ana msichana wake(mpenzi wake) mchaga wa rombo, takribani ni mwaka mmoja sasa, juzi huyo msichana akamwambia mshikaji eti kuna jamaa mmoja aliekua anamtaka zamani kaenda kujitambulisha kwa na msichana bila taarifa yeyote kutoka kwa huyo msichana.

huyo msichana hampendi jamaa alienda kujitambulisha bt anampenda sana mshikaji wangu hadi pesa za chuo anamlipia, tatizo tamaduni za kwao msichana ni kwamba mwanamme wa kwanza akishajitambulisha mme mwingine harusiwi na wazee wanamlazimisha aolewe na huyo jamaa.

msichana anataka akimbie kutoka nyumbani, hii ni alternative ya kwanza, pili; akilazimishwa sana anataka akamfilisi jamaa ili amtumie mshikaji pesa afanye maendeleo then amfanyie huyo jamaa vitimbwi hadi waachane within some months ili arudi kwa mshikaji coz huyo jamaa alienda kujitambulisha ana pesa kweli pia wanafahamiana na wazazi wa msichana

plz ushauri wako utawasaidia; wako dilema.
 
Hapo hamna DILEMA kwa binti,.Alichokifanya huyo mwanaume ni utovu wa nidhamu na sio utaratibu wa kutambulishana ktk shughuli ya kuoa.Huyo mwanaume kajipeleka na kujitambulisha kwa wazazi wa Binti kwa taratibu zipi na ruhusa ya kutoka kwa nani? Mimi ninavyojua Binti huwa anatoa taarifa kwa wazazi wake in Advance,wazazi wote au mmojawao lazima awe na taarifa ya Ugeni kama huo kupitia taarifa za ukweli kutoka kwa binti yao.

(KAMA UCHAGANI HAKUNA MFUMO WA KUTONGOZANA NA KUKUBALIANA NA KWENDA KUJITAMBULISHA,ILI MAHARI ITOLEWE BASI JAMAA HANA KOSA,HUYO RAFIKI YAKO AJITOE TU)

Kama wazazi hawakupewa taarifa kutoka kwa binti yao kuhusu huo ugeni na wakampokea,kumsikilia,na kumwamini huyo jamaa,basi hao wazazi ni Mashetani wakubwa,hawamtendei haki Binti yao.(Kama hizo taratibu zitaendelea bila mushkeli basi binti alikubaliana na huyo aliyejitambulisha na kwa huyo RAFIKI YAKO anazugwa tu hapo) Inakera!!!!
 
Mh! Hainingii akilini mwanaume kujipeleka mwenyewe kujitambulisha! Huyo mshkaji wako hana chake hapo huyo msichana anasiri zake moyoni! Mwambie awatch out!
 
Kiongozi mimi kama mimi ninachokiona hapo ni usanii wa Binti. Si kweli kuwa jamaa wa kwanza alienda kujitambulisha au alienda kujitambulisha bila ridhaa ya binti, ni kuwa bidada anataka 'ruhusa' ya kuolewa na jamaa wa kwanza wakati bado anaendelea na jamaa yako. Bidada anacheza na akili ya huyo jamaa yako. Ni kuwa anawataka wote na nafasi ya kwanza kufunga ndoa kapewa jamaa anaeitwa ana pesa. Hakuna kitu kama eti akaolewe na jamaa kisha amfilisi amnufaishe huyo jamaa yako!
 
. Kama ni kweli wazazi wameridhia watakua na matatizo utakubalije utambilusho bila kucomfirm kwa binti au wameona mpunga???

La binti msanii
 
binti mjanja anawataka wote wawili...vinginivyo wazazi wanataka binti yao aolewe na mwenye fweza
 
upuuuuuuuzi mtupu...... ebu jaribuni kua na akili basi hata kidogo..Mungu hakutuumba wajinga hivyo!!!?
 
Watu siku hizi sio lazima wapande stejini au uwaone kwenye bongo movie ndio ujue ni wasanii.. hapo mwambie rafiki yako hana chake!
 
hi jf, rafki yangu ana msichana wake(mpenzi wake) mchaga wa rombo, takribani ni mwaka mmoja sasa, juzi huyo msichana akamwambia mshikaji eti kuna jamaa mmoja aliekua anamtaka zamani kaenda kujitambulisha kwa na msichana bila taarifa yeyote kutoka kwa huyo msichana.

huyo msichana hampendi jamaa alienda kujitambulisha bt anampenda sana mshikaji wangu hadi pesa za chuo anamlipia, tatizo tamaduni za kwao msichana ni kwamba mwanamme wa kwanza akishajitambulisha mme mwingine harusiwi na wazee wanamlazimisha aolewe na huyo jamaa.

msichana anataka akimbie kutoka nyumbani, hii ni alternative ya kwanza, pili; akilazimishwa sana anataka akamfilisi jamaa ili amtumie mshikaji pesa afanye maendeleo then amfanyie huyo jamaa vitimbwi hadi waachane within some months ili arudi kwa mshikaji coz huyo jamaa alienda kujitambulisha ana pesa kweli pia wanafahamiana na wazazi wa msichana

plz ushauri wako utawasaidia; wako dilema.

Hakuna kitu kama kuolewa na mtu alafu umfilisi! Hakuna kitu kama kujitambulisha bila taarifa binti lazima aridhie!! Huyo dada akishaenda kuolewa na huyo mwenye pesa, muelekeze huyo mshkaji wako kwangu *wink*

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom