Mmarekani mjanja sana, Iran wamekwama wapi?

Mmarekani mjanja sana, Iran wamekwama wapi?

Kombola halikupindishwa (dislocated) ni kazi ngumu sana kufanya hivyo bali wafyatuaji walikuwa na majasusi wa marekani ambao ni waarabu.. Na ndio hao waliotoa habari za uongo na kombora likkaenda kuangamiza ndege
Hapa ndiyo Waarabu na jamii kama hizo zinapofeli.

Kundi la waandamanaji limetaka Kiongozi wa Juu, Ayatollah Khamenei pamoja na viongozi wengine waandamizi kujiuzulu nyadhifa zao baada ya kukiri kuitungua Ndege ya Boeing 737-800, mali ya Shirika la Ndege la Ukraine (UIA) na kusababisha vifo vya watu 176.

Kwanza, Marekani imeua kiongozi muhimu sana wa Iran. Pili, imepindisha kombora lililokiwa lije kupiga kambi zake likaenda kupiga ndege ya abiria ya Ukraine.

Ukitaka kuamini hili, baada ya ndege tu kupigwa washirika wa USA, yaani Uingereza walitoka na madai kuwa ndege hiyo haikupata tatizo la kiufundi badi ilidunguliwa na Iran.

Mwanzoni Iran walikana, mwishowe wakakubali. Sasa jiulize Uingereza walijuaje kuwa Iran ndiyo walioidungua hiyo ndege; jibu ni kuwa wao na USA ndiyo waliopindisha kombora likaenda kupiga ndege ya Ukraine.

Ikumbukwe kuwa Ukraine ni mshirika wa USA na Iran ni mshirika wa Russia. So hapo Marekani atatengeneza tena ugomvi wa Ukraine na Iran. Ukraine watakuja kudai kuwa ni kwanini Iran apige ndege yao na hapo USA watachochea mgogoro.

Sasa Raia wa Iran wanafanya maandamano kuituhumu serikali yao ni kwanini imedungua hiyo ndege. Kosa kubwa walilofanya serikali ya Iran ni kukubali madai ya Uingereza kuwa wao ndio waliodungua kimakosa.

Ni bora wangenyamaza kimya, wakaendekea kukanusha. Sasa hapo USA atapata mwaya wa kuanzisha vikundi vya waasi kupinga serikali yao na kuanza kudhoofisha serikali ya Iran kama ilivyokuwa Syria.

Katika mgogoro huu, USA atakula tatu mzuka. Ameua jenerali wao muhimu, ameanzisha mgogoro kati ya raia na serikali na pia atachochea uhasama kati ya Iran na Ukraine.

Didas Tumaini

Jr[emoji769]
 
Wewe inaelekea una BIFU na Ben Pol, mademu wote hujawaona umemwona Demu wa Ben Pol tu achukuliwe na Monyweather
Hakuna taifa lenye watu wanaofikiria sana kwa sasa dunia hii kama wamarekani.

Hao waajemi ni kujitutumua tu.

Ni sawa na Mayweather achukue demu wa Ben Pol.

Ben Pol atajitutumua tu kuonesha nae yumo ila siyo kweli kwamba ataweza kumpiga Mayweather

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada atakuwa kaangalia movies sana mpaka analeta fiction za kwenye movies kwenye uhalisia!
Sasa kwanini wasingepindisha mabomu yote badala yake wakapindisha moja?Iran waliitungua ndege hiyo kwa kudhani kuwa ni ndege ya wamarekani katika anga yao!!!Hizo nyingine porojo tu!
 
Watu wanavotuambia kuna nchi hazistahili kua na hayo mabomu ya knulklia tuaze kuwaelewa...Lazima unavomiliki vitu vikubwa uwe mstaarabu.hata utajili ndivo ulivo ,ili uwe tajiri nidhamu yafedha lazima uwenayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Wazungu walishatamka hivi, "Kuruhusu Iran amiliki bomu la nyuklia ni sawa na kumkabidhi kisu chizi"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka hakuna hiyo technology ya kupindisha missile Sana Sana unaweza ku intercept lisifike lilikokusudiwa kwa kutumia anti missile shield.Humu tunadanganyana tu story za kwenye kahawa
Sahihi kabisa ,ila muhimu kuangazia macho sasa ndg zetu America na ulaya wanavosema kunanchi hazistahili kumiliki hizo silaha ni ubabe tu au ni sawasawa,ndege ile ilitunguliwa ili iwaje hasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sahihi kabisa ,ila muhimu kuangazia macho sasa ndg zetu America na ulaya wanavosema kunanchi hazistahili kumiliki hizo silaha ni ubabe tu au ni sawasawa,ndege ile ilitunguliwa ili iwaje hasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ile ndege imetunguliwa ki makosa tu( mistake of fact) Yaani Kama wewe tu uchukue mkuki wako au gobore lako uende shambani Usiku kuwinda ngedere wanaokula mahindi yako,then usikie movement shambani kwako uamue kuvuta trigger na kufyatua risasi bila kuchukua tahadhali mwisho wa siku kuja kuhamaki umeuwa binadamu ambaye alikuwa faragha na mpz wake. Ndicho kilichotokea kwa Iran kuidungua ndege ya abiria ya Ukrain international airline. Wao baada ya kurusha makombola kwenye kambi za Marekani kule Iraq wakawa kwenye EXTREME ALEART wakitegemea immediate response kutoka kwa wamarekani. Hilo kosa walilofanya wa Iran technically tunaweza tukaliita NEGLIGENCE OF THE HIGHEST DEGREE(Uzembe uliopitiliza) umtaani wanasema Uzembe wa kiwango Cha lami. Kwa nchi Kama Iran yenye uhasama na Israel na Saudi Arabia tulitegemea iwe na rada ambazo ni softicated na inter connected nchi nzima walitakiwa ku communicate na mamlaka yao ya civil aviation na kujilizisha before taking such a silly act, japo makosa ya namna hii hutokea lakini angalabu kwenye uwanja wa vita na kitaalamu huitwa friendly firing. Kuhusu Iran kumiliki silaha za nyukilia nchi za Magaribi zinaamini Iran inaweza kuzigawa kwa vikundi vya kigaidi Kama Hezibolaa etc,pia ikumbukwe kwa nyakati tofauti Iran imeshajiapiza kuifuta Israel kwenye uso wa dunia na unapoiongelea Israel unaiongelea Marekani moja kwa moja anae recruit agents wa CIA kwa sehemu kubwa middle East ni Mossad ambao wamefanikiwa kupenya kila Kona ya nchi ya kiarabu , Marekani na Israel zinashea intelligence reports zote kwa upande wa middle East. Over
 
Back
Top Bottom