Mmarekani mjanja sana, Iran wamekwama wapi?

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
230
583
Hapa ndiyo Waarabu na jamii kama hizo zinapofeli.

Kundi la waandamanaji limetaka Kiongozi wa Juu, Ayatollah Khamenei pamoja na viongozi wengine waandamizi kujiuzulu nyadhifa zao baada ya kukiri kuitungua Ndege ya Boeing 737-800, mali ya Shirika la Ndege la Ukraine (UIA) na kusababisha vifo vya watu 176.

Kwanza, Marekani imeua kiongozi muhimu sana wa Iran. Pili, imepindisha kombora lililokiwa lije kupiga kambi zake likaenda kupiga ndege ya abiria ya Ukraine.

Ukitaka kuamini hili, baada ya ndege tu kupigwa washirika wa USA, yaani Uingereza walitoka na madai kuwa ndege hiyo haikupata tatizo la kiufundi badi ilidunguliwa na Iran.

Mwanzoni Iran walikana, mwishowe wakakubali. Sasa jiulize Uingereza walijuaje kuwa Iran ndiyo walioidungua hiyo ndege; jibu ni kuwa wao na USA ndiyo waliopindisha kombora likaenda kupiga ndege ya Ukraine.

Ikumbukwe kuwa Ukraine ni mshirika wa USA na Iran ni mshirika wa Russia. So hapo Marekani atatengeneza tena ugomvi wa Ukraine na Iran. Ukraine watakuja kudai kuwa ni kwanini Iran apige ndege yao na hapo USA watachochea mgogoro.

Sasa Raia wa Iran wanafanya maandamano kuituhumu serikali yao ni kwanini imedungua hiyo ndege. Kosa kubwa walilofanya serikali ya Iran ni kukubali madai ya Uingereza kuwa wao ndio waliodungua kimakosa.

Ni bora wangenyamaza kimya, wakaendekea kukanusha. Sasa hapo USA atapata mwaya wa kuanzisha vikundi vya waasi kupinga serikali yao na kuanza kudhoofisha serikali ya Iran kama ilivyokuwa Syria.

Katika mgogoro huu, USA atakula tatu mzuka. Ameua jenerali wao muhimu, ameanzisha mgogoro kati ya raia na serikali na pia atachochea uhasama kati ya Iran na Ukraine.

Didas Tumaini
 
Hakuna namna inabidi masaubwire ajiuzulu tu, atakumbukwa kwa off target zake tu

It's Scars
 
Watu wanavotuambia kuna nchi hazistahili kua na hayo mabomu ya knulklia tuaze kuwaelewa...Lazima unavomiliki vitu vikubwa uwe mstaarabu.hata utajili ndivo ulivo ,ili uwe tajiri nidhamu yafedha lazima uwenayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndio waarabu na jamaii kama hizo zinapofeli
..........



Kundi la waandamanaji limetaka Kiongozi wa Juu, Ayatollah Khamenei pamoja na viongozi wengine waandamizi kujiuzulu nyadhifa zao baada ya kukiri kuitungua Ndege ya Boeing 737-800, mali ya Shirika la Ndege la Ukraine (UIA) na kusababisha vifo vya watu 176
........................
Kwanza Marekani imeua kiongozi muhimu sana wa iran.
Pili imepindisha kombora lililokiwa lije kupiga kambi zake likaenda kupiga ndege ya abiria ya Ukraine.

Ukitaka kuamini hili,baada ya ndege tu kupigwa washirika wa USA,yaani Uingereza walitoka na madai kuwa ndege hiyo haikupata tatizo la kiufundi badi ilidunguliwa na Iran.

Mwanzoni Iran walikana,mwishowe wakakubali,sasa jiulize Uingereza walijuaje kuwa Iran ndio walioidungua hiyo ndege,jibu ni kuwa wao na USA ndio waliopindisha kombora likaenda kupiga ndege ya Ukraine.

Ikumbukwe kuwa Ukraine ni mshirika wa Russia na Iran pia ni mshirika wa Russia,so hapo Marekani atatengeneza tena ugomvi wa Ukraine na Iran, Ukraine watakuja kudai kuwa ni kwanini Iran apige ndege yao na hapo USA watachochea mgogoro.

Sasa Raia wa Iran wanafanya maandamano kuituhumu serikali yao ni kwanini imedungua hiyo ndege.Kosa kubwa walilofanya serikali ya Iran ni kukubali madai ya Uingereza kuwa wao ndio waliodungua kimakosa.

Ni Bora wangenyamaza kimya,wakaendekea kukanusha.Sasa hapo USA atapata mwaya wa kuanzisha vikundi vya waasi kupinga serikali yao na kuanza kudhoofisha serikali ya Iran kama ilivyokuwa siria.

Katika mgogoro huu,USA atakula Tatu mzuka.Ameua jeneral wao muhimu,ameanzisha mgogoro kati ya raia na serikali na pia atachochoa uhasama kati ya iran na Ukraine washirika wa hasimu wak mkubwa Russia.

Didas Tumaini
Una ushahidi wa haya uliyoandika?
Au ni story za vijiweni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushabiki maandazi noma sana. Iran imekiri kuwa iliidungua ndege bila kukusudia wewe umekaa hapo Nanjilinji unakuja na yako eti US 'walipindisha' kombora likaenda kudungua ndege.

Usichokijua ni kuwa kuna tofauti kati ya Missile Defense System na Missile Guidance System.

Missile Defense System kazi yake ni ku detect, ku track, ku intercept na ku destroy missiles za adui. Haina uwezo wa ku guide missile ya adui kwenda kwenye target tofauti.

Missile Guidance System kazi yake ni ku guide missiles kwenda kwenye intended target.

Hivyo basi kama US wange intercept hilo kombora hawana uwezo wa kuli guide kwenda kwenye target tofauti. Zaidi wangeliharibu tu lisifikie target lengwa.

Cc: Paula Paul
 
Ukraine watakuja kudai kuwa ni kwanini Iran apige ndege yao

kwanini isiwe Canada ? maana wao ndio wamekufa wengi mle, ndege ilitunguliwa kuua spies , wa kimarekani wenye tiketi na passport za kikanada

spies wamevuna walichokipanda

hukmu ya spies Iran ni kifo, haijalishi kifo cha namna gani

protest kwenye nchi ni kawaida, HongKong na protest yao inakata mwaka sasa ivi, not to mention ya Ufaransa, yellow vest ilidumu kwa takribani miezi 5
 
Kwa hiyo Ukraine ni mshirika wa Russia?
Russia ina mgogoro wa mda mrefu na jirani yake Ukraine, in fact Ukraine ni rafiki wa kudumu wa nchi za magharibi.

Kitendo cha Iran kuitungua ndege ya Ukraine (unintentionally) huku Iran na Russia zikiwa na strong ties, kutaendeleza wimbi la Russia na Ukraine kuendeleza uhasimu wao mkubwa.
 
Back
Top Bottom