Keyboard_Warrior
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 6,288
- 10,964
Nimekuwa nikiona kila mahala huko mtandaoni, watu wanauliza kwa kebehi, eti kwanini Iran anashambulia nchi karibia zote hapo Mashariki ya kati, lakini hashambulii Israel!?
Hili ndio swali linalotrend huko mitandaoni kwasasa, lakini wote wanaouliza hili swali ni watu wanaofanana kwenye jambo fulani hivi.
Anyways, tuachane na hii.
Mpaka saa hii nimetoka huko mtandaoni, nimekutana na habari za Iran kushambulia Bahrain na Kuwait na kuua askari kadhaa wa Marekani, hii habari inazunguka sana huko mtandaoni saa hii.
Lakini pia, jana nilisoma mahali nilikutana na habari kuwa Pakistan ametishia kuwa endapo Iran itaishambulia Saudi Arabia, basi itakuwa ni sawa wameishambulia Pakistan.
Ajabu usiku wa kuamkia leo Iran imepiga kituo cha kijeshi cha Marekani kilichopo Saudi Arabia, sijui itakuaje sasa?
Kuwait nao visima vyao vya maji safi vimepigwa na kituo cha kuzalisha umeme kimepigwa pia.
Nakuja kwenye swali langu sasa.
Hawa Iran, wanawezaje kupambana na USA na wakati huo huo kupiga kambi za kijeshi za marekani zilizopo katika nchi za Kiarabu? Hawa jamaa wameishi katika vikwazo kwa takribani miaka zaidi ya 40, wanawezaje kupambana na USA!?
Hapohapo mashabiki wanataka akiwa anapambana na USA aingie ulingoni kupambana na Israel pia, jamani hii Iran mbona kama mnaikuza sana?
Yaani mnaona kupigana na Marekani haitoshi, inatakiwa apigane na Israel kwa wakati huohuo, anawezaje sasa!?
Bila kusahau, Strait of Hormuz haipitiki.
Trump anasema ipo wazi, lakini meli zikikatisha zinapigwa kiberiti na Waajemi.
Trump amepereka meli zake za kijeshi kulinda meli zinazokatisha hapo, lakini bado Iran wanaweza kuzishambulia meli zinazokatisha hapo bila ruhusa ya Jeshi la Iran.
Inashangaza sana.
Hawa Iran wanawezaje kufanya haya yote!?
Mbona kama kuna kiini macho hivi!