Mlokole amnywesha damu ya hedhi mwanaye

Mlokole amnywesha damu ya hedhi mwanaye

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,849
​
attachment.php

‘ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni'. Usemi huu umethibitika hivi karibuni baada ya mlokole mmoja, Ruth Mwakalinga, mkazi wa Matejo, Arusha kumnywesha damu ya hedhi mwanaye, Easter Deodat.

Akizungumza na Risasi Jumamosi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Easter alisema kuwa, wazazi wake walimfanyia kitendo hicho kwa tamaa ya kumiliki mali.
"Baba na mama waliamua kunifanyia hivyo kwa lengo la kunipumbaza akili ili niwe ndondocha na wao wawe matajiri," alisema.

Easter alisema kuwa, siku ya tukio alitoka ndani kwa lengo la kutupa uchafu baada ya kupata siku zake (hedhi) lakini alistaajabu mama yake huyo wa kambo alipomfuata na kumzuia ili arudi ndani.

"Nilipoingia ndani aliniuliza nimebeba nini mkononi, nikamwambia sina kitu, cha kushangaza aliniambia niuchukue uchafu huo kisha niikamulie damu hiyo kwenye kikombe alichonipa," alisema Easter huku machozi yakimtoka.

Msichana huyo aliendelea kueleza kuwa, baada ya kuikamulia damu kwenye kikombe, aliambiwa aendelee na kazi zake. Kesho yake asubuhi aliitwa chumbani kwa mama yake na kulazimishwa kuinywa damu hiyo.

Baada ya kuinywa alipoteza fahamu na alipozinduka alijiona akiwa tofauti na siku nyingine. Tangu siku hiyo alikuwa anatokwa na damu kila sehemu yenye uwazi.

Mkasa kamili wa kisa hicho utausoma ambapo utaona jinsi Easter alivyonusurika kupelekwa mochwari baada ya kupoteza fahamu kwa siku nne mfululizo.

Pia utaona ulokole wa mama yake aliyempaka mafuta sehemu za siri akidai ni ya upako baada ya kupewa maagizo na mchunguji wake wa kanisa moja huko Arusha.

MLOKOLE AMNYWESHA DAMU YA HEDHI MWANAYE-2

attachment.php

Katika Gazeti la Risasi Jumamosi toleo namba 795 la Aprili 30, 2011 kiliandikwa kisa cha msichana Ester Deodat (pichani) kunyweshwa damu yake ya hedhi na mama yake wa kambo. Tuliahidi kuendelea na mkasa huo kwenye gazeti hili.

Awali ya yote tunaomba kufanya masahihisho ya jina la Ruth Mwakalinga ambaye katika habari ile ilisemwa ndiye aliyefanya unyama huo.

Usahihi ni kwamba, Ruth ni mama mzazi wa Ester na si mama wa kambo. Hata hivyo, tunaomba kulihifadhi jina la mama wa kambo aliyefanya mkasa huo.
Baada ya kutoa marekebisho hayo tuendelee na mkasa wa binti huyu kunyweshwa damu ya hedhi na mama yake wa kambo.

“Baada ya kuninywesha zile damu zangu mwenyewe nilipoteza fahamu. Naamini ilitokana na ukweli kwamba, sikutarajia hata siku moja kama naweza kunywa damu yangu tena ya hedhi, hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya mimi kupoteza fahamu. Lakini Mungu ni mkubwa sana jamani.

“Sikumbuki ilipita muda gani, lakini nilipokuja kuzinduka, nilijikuta nipo tofauti na siku nyingine. Hata nilipoangalia mazingira nilijigundua mimi Ester sikuwa wa kawaida, kuna kitu. Lakini akili haikuwa ikiniambia ni kitu gani.

Cha kushangaza ambacho pia kilinishtua, kila nilipokasirika nilikuwa natokwa na damu katika kila sehemu yenye uwazi mwilini mwangu.
Sehemu hizo ni kama matundu ya sikio, puani, sehemu ya haja kubwa, haja ndogo na kinywani. (Ester alianza kulia). Akaendelea:

“Damu yenyewe iliyokuwa inanitoka ilikuwa nzito kama matope hali iliyonifanya niamini kwamba, kwa vyovyote vile kifo changu hakikuwa mbali na siku ile.
Niliendelea kuteswa na hali hii kiasi kwamba, nikawa mtu wa kukaa ndani tu ili majirani au watu wengine wasinione nilivyoteseka.

Baada ya mateso ya muda mrefu, ndipo siku moja baba alilazimika kunipeleka hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru kwa ajili ya vipimo mbalimbali ili kubaini kisa cha kutokwa na damu sehemu zenye uwazi katika mwili wangu baada ya kukasirika.

Pale hospitali, baada ya kusimuliwa maradhi yangu, madaktari walichukua damu yangu kwa ajili ya kuipima,” alisema Ester huku akifuta machozi.

Akaendelea; Lakini sasa na wao wakachanganyikiwa zaidi, kwani walipokwenda kuipima ile damu iliganda na kuwa nyama, hivyo wakashindwa kubaini kinachonitesa.
Kuganda kwa damu hiyo na madaktari kushindwa kubaini ugonjwa, kuliwafanya wanipeleke Nairobi kwa ajili ya msaada zaidi.

Niliamini kama wao wameamua kunipeleka kwa wenzao nje ya nchi, lazima tatizo lingebainika kwani niliamini nje kuna madaktari wazuri kuliko nyumbani Tanzania.
Nilifikishwa kwenye hospitali moja ambayo nimeisahau jina, lakini ipo kwenye Jiji la Nairobi.

Pale, madaktari walifanya kama wenzao wa Mount Meru, walichukua vipimo mbalimbali pamoja na damu, wakaenda kuipima.

Nilikuwa katika wakati mgumu sana moyoni, kwani nikiwa nasubiri majibu, nilihisi kuchanganyikiwa akili. Mawazo yangu yote yalikuwa ni juu ya itakuwaje kama damu itaganda na kuwa nyama kama ilivyotokea awali.

Itaendelea baadae.................

Attachments

  • Emelda.jpg
    Emelda.jpg
    40.8 KB · Views: 2,116
[h=1]MLOKOLE AMNYWESHA DAMU YA HEDHI MWANAYE-3..[/h]ILIPOISHIA :
Nilikuwa katika wakati mgumu sana moyoni, kwani nikiwa nasubiri majibu, nilihisi kuchanganyikiwa akili. Mawazo yangu yote yalikuwa yakiwaza itakuwaje kama damu itaganda na kuwa nyama kama ilivyotokea awali.
SASA ENDELEA....

Waswahili husema ‘Sikio la Kufa Halisikii Dawa', hata mimi nilifikia hatu ya kuwaza hivyo kwani majibu yakawa kama ya nyumbani. Damu iliganda.
Nililia sana, nikatamani kufa au hata kujinyonga ili niachane na dunia hii nzuri ya Mungu, lakini iliyojaa visa, visasi na mateso.

Hakukuwa na jinsi tena, kilichotamkwa pale na madaktari ni mimi kurudishwa nyumbani Tanzania. Moyoni nilisema narudishwa nyumbani ili nikafe, nikasema sawa bwana, aliyewaumba wao ndiye aliyeniumba mimi ambaye sasa nimekuwa si binadamu tena.

Safari ya kurudi Tanzania ilianza, nikafikia Hospitali ya Mount Meru. Lakini hali ya mara hii ikawa mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza kwani damu ilikuwa ikitoka mwilini kama nimepata ajali mbaya ya gari."
Ester ambaye alionesha kukerwa sana na ugonjwa huo, alisema kuwa, alilazimika kulazwa.

Anasema:
"Nikiwa kitandani, nilizungushiwa pamba mwili mzima ili zifyonze damu iliyokuwa inatoka.
Siku ya pili iliingia hakukuwa na dalili yoyote ya unafuu. Daktari mmoja akaniambia nitalazimika kulala katika hali ile kwa muda wa mwezi mmoja huku nikiwa nimewekewa mirija ya kunisaidia kupumua.

Hakika ni Mungu tu alikuwa upande wangu. Niliwekewa pamba mwili mzima ili kufyoza damu na nikawekewa mirija ya kunisaidia kupumua kwani hali ilikuwa mbaya kupita maelezo.

Naambiwa kuwa, baada ya mwezi mmoja nikiwa kitandani, nilipoteza fahamu na manesi wakalazimika kunizungushia shuka za kuashiria kuwa nimefariki.
Mama yangu mzazi, alipopata habari alifika hospitalini, akakataa nisipelekwe mochwari akiamini sijafa.

Pia alikwenda kuripoti kituo cha polisi kuhusu chanzo cha mkasa wangu, hivyo baba na mama yangu wa kambo walikamatwa na kuwekwa mahabusu.

Alisema mama yake wa kambo aliachiwa huru baada ya muda, lakini baba yake aliendelea kushikiliwa na kuhojiwa kwa mapana ambapo baadaye alikiri kuwa yeye na mkewe walitaka kunifanya dondocha ili wawe matajiri.

Kitendo cha kukiri huko kukawa salama kwake na mara alizinduka baada ya siku 4 na kila aliyekuwa kwenye wadi hiyo walikimbia wakidhani ni mzimu.
Easter alisema mama yake alimchukua na kumrejesha nyumbani akiwa katika hali nzuri kidogo lakini kila alipopata hasira, damu ilikuwa ikimtoka.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Easter aliamua kwenda kwa Mchungaji Mstaafu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambikile Masapile ‘Babu' kwa ajili ya kupata kikombe.

Alisema, alifanikiwa kupata kikombe hicho na kujiona ana hali nzuri. Akiwa njiani kurejea Dar, alianza kujisikia kichefuchefu na kisha kutapika damu.

Easter alisema baada ya kufika nyumbani kwao, alikaa kama wiki moja hali ikawa mbaya na alianza tena kutokwa damu mwili mzima kisha akapoteza fahamu.

Itaendelea baadae.....
 
MLOKOLE AMNYWESHA DAMU YA HEDHI MWANAYE-4...

ILIPOISHIA

SASA ENDELEA...

Baada ya kupoteza fahamu, mume wangu aliomba msaada kwa majirani na ndipo walipoamua kupiga simu kwa Askofu na Nabii, Nicolaus Sugeye wa Huduma ya Neno la Upatanisho iliyopo Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maombi.

Nikiwa katika hali ya kupoteza fahamu , jirani yangu mmoja alichukua simu yake na kuiweka sikuoni mwangu. Kwa mbali nilisikia sauti ya maombi sikujua ni yanani, kumbi wakati huyo mtumishi wa Mungu Suguye alikuwa anaomba kwa njia ya simu hiyo. Ghafla nilizinduka na damu iliyokuwa inatoka mwilini iliacha.

Baada ya kunyanyuka mume wangu na rafiki yake walinichukua na kunipeleka kwa Askofu na Nabii Suguye kwa ajili ya kuombewa na katika hali ambayo siwezi kuielezea mpaka sasa, baada ya kukutana na mtumishi huyo wa Mungu na kuombewa hakika nilipona kabisa.

Tatizo hilo lililokuwa linanisumbua kwa muda mrefu nashangaa lilipona siku moja mpaka nataoa ushuhuda huu mimi ni mzima wa afya.

Lakini kabla ya kupata uponyaji huu, nilipelekwa Loliondo kwa Babu kwa ajili ya kunywa dawa inayosadikika inaponya magonjwa sugu.

Nilifanikiwa kunywa dawa hiyo nikiwa na hali mbaya huku mume wangu akifikiri kwamba sitarudi salama nyumbani.Daada ya kupata kikombe hicho, hali yangu ilionekana kuimarika nikawa natembea kama kawaida huku mume wangu akionekana mwenye furaha kubwa.

Safari ya kurudi Dar es Salaam ilianza, lakini nikiwa njiani ghafla nilianza kusikia kichefu chefu kisha nikaanza kutapika damu. Kila aliyekuwa akiniangalia alitokwa machozi kutokana na hali yangu kuwa mbaya.

Kila mmoja alisema lake huku mume wangu akionekana kukata tamaa na hali hiyo kwani ilikuwa haipiti wiki moja lazima hali hiyo initokee.

Namshukuru Mungu mume wangu alionesha upendo wa dhati kwani alikuwa nami bega kwa bega. Kwa kifupi nasema kwamba uponyaji wangu ulipatikana mara baada ya kupata maombi kutoka kwa mtumishi wa Mungu Askofu na Nabii Nicolaus Suguye.

Kikombe cha Babu wa Loliondo hakikunisaidia kwani nilikuwa nimefungwa na nguvu za giza kutoka kwa wazazi wangu. Msomaji huu ni mkasa wa kweli.Ester aliomba nitoe namba yake ili mwenye mashaka azungumuze naye. Namba yake ni 0713618820. ''MWISHO''
 
Hizi story huwa ni za kutunga ajili ya kutumika katika ushuhuda.ni marketing strategy ya wachungaji kuvuta wateja.
Kama alinyweshwa damu ya hedhi akiwa mbinti mwishoni anataja mmewe.lini kaolewa hapo?
 
Sitaki kuamini sababu damu ya hedhi ni sumu mbya mno,tone moja tu linaondoa uhai wa mtu
 
just edit the original post to add more information badala ya kurudia upya in 3 or more posts -.-

on topic:
  1. huyu ni mlokole jina au wa kweli, mbona sijaona aliposema yeye kaokoka?
  2. aside form the gross factor ewww, kunywa damu ya hedhi kuna madhara?
  3. nasikitika ninavyosoma watu walivyo tayari kupata mali kwa njia zozote kasoro hard work
 
Machoni kama watu
Mioyoni hawana utu
Imani imetoweka
Mabaya yanaongezeka
 
Duh...... Hawa bila shaka ni walokole wa dini ya SHETANI
​
attachment.php

‘ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni'. Usemi huu umethibitika hivi karibuni baada ya mlokole mmoja, Ruth Mwakalinga, mkazi wa Matejo, Arusha kumnywesha damu ya hedhi mwanaye, Easter Deodat.

Akizungumza na Risasi Jumamosi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Easter alisema kuwa, wazazi wake walimfanyia kitendo hicho kwa tamaa ya kumiliki mali.
"Baba na mama waliamua kunifanyia hivyo kwa lengo la kunipumbaza akili ili niwe ndondocha na wao wawe matajiri," alisema.

Easter alisema kuwa, siku ya tukio alitoka ndani kwa lengo la kutupa uchafu baada ya kupata siku zake (hedhi) lakini alistaajabu mama yake huyo wa kambo alipomfuata na kumzuia ili arudi ndani.

"Nilipoingia ndani aliniuliza nimebeba nini mkononi, nikamwambia sina kitu, cha kushangaza aliniambia niuchukue uchafu huo kisha niikamulie damu hiyo kwenye kikombe alichonipa," alisema Easter huku machozi yakimtoka.

Msichana huyo aliendelea kueleza kuwa, baada ya kuikamulia damu kwenye kikombe, aliambiwa aendelee na kazi zake. Kesho yake asubuhi aliitwa chumbani kwa mama yake na kulazimishwa kuinywa damu hiyo.

Baada ya kuinywa alipoteza fahamu na alipozinduka alijiona akiwa tofauti na siku nyingine. Tangu siku hiyo alikuwa anatokwa na damu kila sehemu yenye uwazi.

Mkasa kamili wa kisa hicho utausoma ambapo utaona jinsi Easter alivyonusurika kupelekwa mochwari baada ya kupoteza fahamu kwa siku nne mfululizo.

Pia utaona ulokole wa mama yake aliyempaka mafuta sehemu za siri akidai ni ya upako baada ya kupewa maagizo na mchunguji wake wa kanisa moja huko Arusha.

Uwe tajiri kwa kuwafanya wanao mataahira au marehemu inakupa raha gani?? Je, utafurahia maisha na kuishi milele? Kwa nini hao wanaotaka kuwa matajiri kwa njia hizi huwa hawafikirii faida na hasara zake?

Kwa tabia hizi, nawashangaa sana binadamu. Binadamu ambao maisha yao ni kama maua! Binadamu ambao uhai wao hauko mikononi mwao unaweza kutoweka muda wowote!

Fanya kazi kwa bidii, jitume na utajirike kihalali. USITOE/USICHEZEE uhai wa binadamu mwenzako maana wewe ni mavumbi tu.
 
Hizi story huwa ni za kutunga ajili ya kutumika katika ushuhuda.ni marketing strategy ya wachungaji kuvuta wateja.
Kama alinyweshwa damu ya hedhi akiwa mbinti mwishoni anataja mmewe.lini kaolewa hapo?

Pana disconection ya story hapa kama unavyosema Elungata! Eti alikuwa binti anaishi na wazazi tena Arusha, akanyweshwa damu ya hedhi na wazazi, hailezewi alikuwa na umri gani, na alipata nafuu kwa kipindi gani hadi kukutana na mchumba aliyekuja kuwa mume na kuhamia Dar... Na je, mama mzazi alikuwa naishi wapi hata akaja wakati tayari "amekufa" na mama alikuwana uwezo gani wa kuwazuwia madaktari walisema mgonjwa amekufa hasipelekwe mochwari tena kwa siku nne..

Yaani madaktari, na manesi walikubali mtu waliyeamini amekufa akae wodini kwa siku nne tena kukiwa na wagonjwa wengine ambao walianza kukimbia baada ya kuzinduka siku ya nne??

Mbona anatajwa mtumishi wa Mungu aliyemuombea Ester lakini kanisa na mtumishi walikokuwa wanaabudu wazazi wake waliomnywesha damu ya hedhi hatajwi, okey ilikuwa ni lini na kituo gani cha polisi kinachosemekana alipelekwa baba mzazi na mama wa kambo wa Ester?

Baba alishiriki kumnywesha damu ya hedhi ili awe ndodocha na yeye kupata utajiri aliwezaje tena yeye kumpeleka hospitali ili kujua kinachomsumbua?

Haya tunaweza kujua tarehe alizofikishwa hospitali hiyo ya Mount Meru na kama inawezekana alikuwa wodi gani na alihudumiwa na daktari gani (Jina) na gharama za kumepeleka hospitali ya Nairobi ambayo haikumbuki jina alizitoa nani?

Aidha hadithi hii ni ya kutunga, au mletaji amechakachua.........
 
Last edited by a moderator:
mwee kabinti kenyewe kanaonekana bombaa, labda saloon kidogo kwa ajili ya mambo machache tu. Lakini ndiye kafanya hivyo kweli? Bora mimi niendelee kuwa mtaifa!
 
askofu na nabii - WEWE MTU HUYOHUYO MMOJA ......? UMESHINDWA KUWAPATA HUKO MABARABARANI SASA UNATULETEA UTAPELI WAKO HUMU.
MLOKOLE AMNYWESHA DAMU YA HEDHI MWANAYE-4...

ILIPOISHIA
Kitendo cha kukiri huko kukawa salama kwake na mara alizinduka baada ya siku 4 na kila aliyekuwa kwenye wadi hiyo walikimbia wakidhani ni mzimu.

Easter alisema mama yake alimchukua na kumrejesha nyumbani akiwa katika hali nzuri kidogo lakini kila alipopata hasira, damu ilikuwa ikimtoka.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Easter aliamua kwenda kwa Mchungaji Mstaafu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambikile Masapile ‘Babu' kwa ajili ya kupata kikombe.

Alisema, alifanikiwa kupata kikombe hicho na kujiona ana hali nzuri. Akiwa njiani kurejea Dar, alianza kujisikia kichefuchefu na kisha kutapika damu.

Easter alisema baada ya kufika nyumbani kwao, alikaa kama wiki moja hali ikawa mbaya na alianza tena kutokwa damu mwili mzima kisha akapoteza fahamu.
SASA ENDELEA...

Baada ya kupoteza fahamu, mume wangu aliomba msaada kwa majirani na ndipo walipoamua kupiga simu kwa Askofu na Nabii, Nicolaus Sugeye wa Huduma ya Neno la Upatanisho iliyopo Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maombi.

Nikiwa katika hali ya kupoteza fahamu , jirani yangu mmoja alichukua simu yake na kuiweka sikuoni mwangu. Kwa mbali nilisikia sauti ya maombi sikujua ni yanani, kumbi wakati huyo mtumishi wa Mungu Suguye alikuwa anaomba kwa njia ya simu hiyo. Ghafla nilizinduka na damu iliyokuwa inatoka mwilini iliacha.

Baada ya kunyanyuka mume wangu na rafiki yake walinichukua na kunipeleka kwa Askofu na Nabii Suguye kwa ajili ya kuombewa na katika hali ambayo siwezi kuielezea mpaka sasa, baada ya kukutana na mtumishi huyo wa Mungu na kuombewa hakika nilipona kabisa.

Tatizo hilo lililokuwa linanisumbua kwa muda mrefu nashangaa lilipona siku moja mpaka nataoa ushuhuda huu mimi ni mzima wa afya.

Lakini kabla ya kupata uponyaji huu, nilipelekwa Loliondo kwa Babu kwa ajili ya kunywa dawa inayosadikika inaponya magonjwa sugu.

Nilifanikiwa kunywa dawa hiyo nikiwa na hali mbaya huku mume wangu akifikiri kwamba sitarudi salama nyumbani.Daada ya kupata kikombe hicho, hali yangu ilionekana kuimarika nikawa natembea kama kawaida huku mume wangu akionekana mwenye furaha kubwa.

Safari ya kurudi Dar es Salaam ilianza, lakini nikiwa njiani ghafla nilianza kusikia kichefu chefu kisha nikaanza kutapika damu. Kila aliyekuwa akiniangalia alitokwa machozi kutokana na hali yangu kuwa mbaya.

Kila mmoja alisema lake huku mume wangu akionekana kukata tamaa na hali hiyo kwani ilikuwa haipiti wiki moja lazima hali hiyo initokee.

Namshukuru Mungu mume wangu alionesha upendo wa dhati kwani alikuwa nami bega kwa bega. Kwa kifupi nasema kwamba uponyaji wangu ulipatikana mara baada ya kupata maombi kutoka kwa mtumishi wa Mungu Askofu na Nabii Nicolaus Suguye.

Kikombe cha Babu wa Loliondo hakikunisaidia kwani nilikuwa nimefungwa na nguvu za giza kutoka kwa wazazi wangu. Msomaji huu ni mkasa wa kweli.Ester aliomba nitoe namba yake ili mwenye mashaka azungumuze naye. Namba yake ni 0713618820. ''MWISHO''
 
Hizi story huwa ni za kutunga ajili ya kutumika katika ushuhuda.ni marketing strategy ya wachungaji kuvuta wateja. Kama alinyweshwa damu ya hedhi akiwa mbinti mwishoni anataja mmewe.lini kaolewa hapo?
Unahitaji kuwa mjinga hasa kuamini story za namna hii. Kuna sehemu hapo inasem 'dakatri akaniambia utakaa katika hali hii kwa mwezi mzima' hivi dakatari anawezaje kujua damu itaacha kutoka kwa mwezi mzima? Kwanza na wewe MziziMkavu, ilikuwaje mpaka mwanaume ukaanza kusoma Risasi? Habari kama hizi huwezi kuzikuta kwenye magazeti yenye akili zake.
 
Last edited by a moderator:
Kama hi stori ni ya ukweli,basi huyu mama hakua mlokole sema alitumia ulokuole kuficha makucha yake na mambo aliyokua anayafanya
 
Kama hi stori ni ya ukweli,basi huyu mama hakua mlokole sema alitumia ulokuole kuficha makucha yake na mambo aliyokua anayafanya
Bibie Penelope History ya ukweli kama unataka kuamini jaribu kupiga simu hii namba muulize huyo bibie (Ester aliomba nitoe namba yake ili mwenye mashaka azungumuze naye. Namba yake ni 0713618820)
 
Last edited by a moderator:
Hizi story huwa ni za
kutunga ajili ya kutumika katika ushuhuda.ni marketing strategy ya
wachungaji kuvuta wateja.
Kama alinyweshwa damu ya hedhi akiwa mbinti mwishoni anataja mmewe.lini
kaolewa hapo?

Elungata, Bora umeuliza wewe sie wengine tukiuliza ni balaa! ila KAOLEWAJE NA LINI?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom