Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,103
- 3,023
Takriban watu 32 wameuawa katika mlipuko uliotokea kwenye msikiti mmoja katika mji wa Peshawar nchini Pakistan.
Mlipuko huo ulitokea wakati msikiti huo ukiwa umejaa waumini na zaidi ya watu 150 kujeruhiwa.
Sehemu ya jengo iliharibiwa, na maafisa wanasema watu wamezikwa chini ya vifusi.Wengine kadhaa wanapelekwa katika hospitali za mji huo.
Chanzo cha mlipuko huo hakijajulikana.Waziri Mkuu Shebaz Sharif amelaani vikali shambulio hilo.
Katika taarifa, Bw Sharif alisema waliohusika na tukio hilo "hawana uhusiano wowote na Uislamu".
Aliongeza: "Taifa zima limesimama kwa umoja dhidi ya tishio la ugaidi".
Mlipuko huo ulitokea wakati wa sala ya alasiri katika mji wa kaskazini-magharibi, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan.
Mohammad Asim, msemaji wa Hospitali ya Lady Reading, alisema kuwa baadhi ya waliojeruhiwa walikuwa katika hali mbaya.
"Ni hali ya dharura," Bw Asim aliongeza.
Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa polisi, jeshi na vikosi vya kutegua mabomu viko kwenye eneo la tukio.
Katika mji mkuu, Islamabad Polisi ilitoa tahadhari ya juu ya usalama na kusema usalama katika maeneo yote ya kuingia na kutoka katika mji huo umeongezeka.
BBC Swahili