Mlipuko wa Malaria sugu Dar es salaam!

Mlipuko wa Malaria sugu Dar es salaam!

Tatizo wala sio Malaria ya watu,tatizo kubwa ni UKIMWI.Unajua Dar watu wengi wanaumwa ila hawaelewi kwanini Vipimo vya Ukimwi vinasoma Negative wakati wao kwa jinsi wanavyoumwa wanajijua kabisa hawawezi kukosa UKIMWI na wanagongana sana wasife wenyewe,Nadhani Wizara ya Afya iangalie upya Vipimo vya Ukimwi kama viko sawa basi kuna Ugonjwa Mwingine unaofanana na UKIMWI umeingia,wasipokazana hapo wataisingizia sana Malaria ya watu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Dawa za malaria feki .
TFDL linawahusu ,hivi sasa wanakula rushwa kwa sana .
 
sasa hivi dar kuna mlipoko wa DENGUE FEVER.dalili zake zinafanana sana na maralia.ushauri wangu.ukipata homa kali(namaanisha mwili kupanda kwa joto lake)nenda mwananyamala hosp.pale kuna kituo kinaitwa FEVER STUDY wanapita vipimo vingi kikiwemo na hicho cha DENGUE FEVER.pale itajulikana kama ni malaria au dengue.mshauri hili na mwezio.
 
Kwa hiyo ukiupata dengue ni kifo tu?

hapana.sio ndo kifo.ni selflimiting.inaisha yenyewe ndani ya siku kumi au zaidi.kinachotakiwa ni kushusha homa n.ingawa mara nyingine yaweza kusababisha kutokwa na damu puani na maeneo mengine mwilini.
 
Alla..! kumbe ni denge hili.., wengi wao walikuwa wanasema malaria hawana ila wanasikia kila dalili za malaria.., aisee..!
 
Very well said. Halafu sijajua kama kama wanatumia recommended dose au bado wanatumia SP?

Mzee wa fursa Kaizer, hivi mbu wanauma kuanzia saa ngapi, nimekuja Tabata kusalamia tu ndugu jamani. Hivi wanapenya kwenye Tusker bariidi? Niarifu haraka nifunge virago!
 
Last edited by a moderator:
ni kweli tatizo la malaria ni dar nzima...mabadiliko ya halu ya hewa na sijui labda ni wale mbuu waliyokuwa kwenye madimbwi kule muhimbili...ila malaria imewapata asilimiaa kubwaaa na hadi kuua imeua..naona serikali kupitia wizara ya afya wako kimyaa...hawaja chukua hatua yoyote mpaka sasa

Meya wa Ilala anakwambia hawezi kuzuia mvua, hata planning ya kukabukiana na Malaria nayo hana?
 
Halafu hawa mbu mbona wakali sana? Yani usiku usivae penzi halafu ukakae nje, wakikung'ata utafikiri mtu amekuchoma na msumari. Pia kuna mbu weusi wakubwa hivi ukikaa hata mchana kama sehemu ina kigiza wanakutokea, sijui ndo mbu gani hawa?
 
dengue ishaingia mjini...drink lots of fluids and fruits people..kitu hakina cure kwa ninavyosikia, kule India inawamalizaga wengi tu
 
Tatizo la watu wengi wanachukulia kila homa ni malaria, hata mafua yanaleta dalili kama za malaria. Kila mtu ukimuliza waumwa nini anasema malaria, this isnt the matter. Kwanza hizo maabara tunazoenda pima zimekaa kibiashara ni vigum kuambiwa huna malaria, na mbaya zaidi unapewa dawa ambazo kimsingi cure rate ni ndogo sana kama sp. Hapo unauchezea mwili wako mwenyewe. Yakupasa kufahamu kuna magonjwa mengi zaidi ya malaria, na c kila unakopima wanakupa majibu sahihi, na si kila daktari anaweza kubadili fikra zako na kukusaidia kuwaza zaidi ya malaria, si kila dawa ya malaria inamaliza malaria.
 
Niugua from tar 23 march nilikutwa na Malaria 3 nikatumia mseto hakuna nafuu, nikaenda kwa Dr. Mvungi ikakutwa imeongezeka hadi imekuwa malaria 6 nikalazwa 3 days nimetundikiwa Quinine nilivyoruhusiwa nikapewa duo-cotexin nikazimaliza! Ikapungua ila haikwisha nikarudi tena hapo kwa Dr. Mvungi nikaambiwa bado ipo Malaria 2 nikapewa Quinine ya vidonge nikameza siku ya kwanza ya pili nikaenda kumsalimia mtu msasani nikajisikia kukaukiwa sana yaani mate yanakauka kabisa mdomoni nikawahi TMJ nikatundikiwa Drip mbili za maji nikachukuliwa damu kwa further checkup Nikaambiwa nistop zile dawa za QUININE from that Moment!
Baadae majibu yakaja nikakutwa kwingine(liver function, kidney function e.t.c) kupo Ok ila nikaambiwa inaonyesha kwenye blood kuna infection(Maybe ndo hiyo Malaria) nikapewa dawa fulani hivi kwa siku 5 nilivyorudi nikapimwa nikaambiwa Malaria hakuna tena! Nikaenda sehemu nyingine wakaniambia tena hakuna Malaria!
Nimeumwa almost 3 weeks!
Ila namshukuru Mungu sasa hivi niko very ok!

ki ukweli malaria ni noma sana.. Kuna mahali nina wasiwasi niliipata ile malaria yenyewe.. Tena nje ya Dar.. Ilinicost zaidi ya mwaka.. Nikijitahidi sana basi nitakaa mwezi mmoja tuu unaofuatia malaria... Kuna wakati nikiwa dar ndio haitoki kabisaaaaa...nilienda hospital moja yule daktari aliekuwa ananipa majibu akaniambia hata yeye ana malaria ila ameamua asinywe dawa maana haitoki.. Duh.. Nikawa mpole.. Nilichokuja kuamini ni kwamba.. Kama huna elimu nzuri ya malaria na kutafuta dawa mbadala na kama buna pesa ya kununua dawa za maana malaria inaweza kukuua kabisa. Nimepambana na malaria kwa nguvu kubwa am glad sasa nina MIEZI 7 sijaisikia kabisa..
 
Nimemaliza metakeflin ,nimepima leo wamesema wapo waili.

Nimegonga mwarobaini jioni nasikilizia,asubuh nishtue tena.
 
sasa hivi dar kuna mlipoko wa DENGUE FEVER.dalili zake zinafanana sana na maralia.ushauri wangu.ukipata homa kali(namaanisha mwili kupanda kwa joto lake)nenda mwananyamala hosp.pale kuna kituo kinaitwa FEVER STUDY wanapita vipimo vingi kikiwemo na hicho cha DENGUE FEVER.pale itajulikana kama ni malaria au dengue.mshauri hili na mwezio.
RockSpider tupia jicho uzi huu.
 
Last edited by a moderator:
hapana.sio ndo kifo.ni selflimiting.inaisha yenyewe ndani ya siku kumi au zaidi.kinachotakiwa ni kushusha homa n.ingawa mara nyingine yaweza kusababisha kutokwa na damu puani na maeneo mengine mwilini.

Hatari yake ni kushusha blood pressure.
 
Back
Top Bottom