Mlipuko wa Malaria sugu Dar es salaam!

Mlipuko wa Malaria sugu Dar es salaam!

Jamani naomba mnisaidie ni dawa gani unayoweza kupuliza ndani ikamaliza kabisa mbu manake mbu waliop sasa hivi na wengi na dawa nyingi feki na kibaya zaidi kwa sasa hivi kitu kinachoitwa dripu kwenye maduka yajumla hakuna kabisaa kwa mfani rl, dns ni dhahabu kuzipata sasa kwa wale watu wenye low bp watatumia drip za aina gani .
 
Sio tu Malaria kaka,pia Dengue fever nayo imeibuka Dar, mbaya zaidi ugonjwa huu hauna tiba,Kwani husababishwa na aina flani ya virus wanaoenezwa na Mbu aina ya Ades na dalili zake kuu nyingi zinafanana na magonjwa kama Malaria, Typhoid n.k, mfano ni; kichwa kuuma sana, joto la mwili kuwa kali, maumivu ya misuli hasa miguu,mgongo na mikono,n.k.

Kwa hiyo ukiupata dengue ni kifo tu?
 
Kwa hiyo ukiupata dengue ni kifo tu?

Hapana,kama ikiwahiwa, uwezekano wa kufa ni mdogo. normally treatment is entirely symptomatic and supportive.
Hatari zaidi ni kwa watoto wachanga.
 
Ulishawahi kuchoma vifuu vya nazi ndani? Au nyie ndio mliozaliwa ocean road ha ha ha ha ha.
Jamani naomba mnisaidie ni dawa gani unayoweza kupuliza ndani ikamaliza kabisa mbu manake mbu waliop sasa hivi na wengi na dawa nyingi feki na kibaya zaidi kwa sasa hivi kitu kinachoitwa dripu kwenye maduka yajumla hakuna kabisaa kwa mfani rl, dns ni dhahabu kuzipata sasa kwa wale watu wenye low bp watatumia drip za aina gani .
 
Duh hii kweli hasa Tabata nimeishuhudia aisee...Nyumbani kwangu kuna wagonjwa wawili na wikiendi hii nimeenda kwenye kiota (Kwetu Pazuri) kupiga moja mbili naona jamaa zangu wawili wanakunywa maji kisa Dozi ya Malaria.

Kaka tutafutane basii!Kwetu Pazuri ndo Kiwanja bwana!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Sio tu Malaria kaka,pia Dengue fever nayo imeibuka Dar, mbaya zaidi ugonjwa huu hauna tiba,Kwani husababishwa na aina flani ya virus wanaoenezwa na Mbu aina ya Ades na dalili zake kuu nyingi zinafanana na magonjwa kama Malaria, Typhoid n.k, mfano ni; kichwa kuuma sana, joto la mwili kuwa kali, maumivu ya misuli hasa miguu,mgongo na mikono,n.k.

nahis ninao mwili wangu unachemka sana na pia kichwa kinauma
 
Tatizo wala sio Malaria ya watu,tatizo kubwa ni UKIMWI.Unajua Dar watu wengi wanaumwa ila hawaelewi kwanini Vipimo vya Ukimwi vinasoma Negative wakati wao kwa jinsi wanavyoumwa wanajijua kabisa hawawezi kukosa UKIMWI na wanagongana sana wasife wenyewe,Nadhani Wizara ya Afya iangalie upya Vipimo vya Ukimwi kama viko sawa basi kuna Ugonjwa Mwingine unaofanana na UKIMWI umeingia,wasipokazana hapo wataisingizia sana Malaria ya watu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
huo ni ugonjwa unaitwa DENGE dalili zake na km za malaria na hauna tiba zaidi ya kunywa maji mengi

Mkuu kuna mtu alisema kuna mbu toka India hawa malaria yake ni kali sana na temp huwa juu haipingui 40. Sijui kama serekali wanalijua hili.
 
Siyo Tabata tu, hadi Ubungo kuanzia wiki moja kabla ya pasaka ni majanga tu, mi mwenyewe yamenikuta hayo.
 
Malaria kila nyumba imekua tishio sasa. Na kwa watoto muwe makini maana MRDT haiko sensitive ktk ku detect or diagnose malaria hivyo kwa watoto zingatien BS zaidi. Tofauti na hapa malaria itamzidi mtoto aishie kwenye degedege.
 
Sio tu Malaria kaka,pia Dengue fever nayo imeibuka Dar, mbaya zaidi ugonjwa huu hauna tiba,Kwani husababishwa na aina flani ya virus wanaoenezwa na Mbu aina ya Ades na dalili zake kuu nyingi zinafanana na magonjwa kama Malaria, Typhoid n.k, mfano ni; kichwa kuuma sana, joto la mwili kuwa kali, maumivu ya misuli hasa miguu,mgongo na mikono,n.k.

Thanks mkuu.Nahisi nahitaji kucheck kwa ugonjwa huu.Juzi kati nilikwenda kupima AAR hospital nikaambiwa sina malaria lakini joints zote zinauma pamoja na mgongo!
 
mi sasa hivi nimeacha kutumia dawa za hospital natumia tiba mbadala kwani hizi dawa mbali ya kuwa gharama haziponyeshi malaria sijui kwanini waliondoa dawa za zamani kwani zilikuwa zinatutibu vizuri hizi dawa mpya ni majanga kabisa
 
Ni jambo lililonishtua hasa kwa maeneo ya Tabata.., kila nyumba ninayoingia hukosi mtu anaumwa malaria.., tena utaambiwa kuna wengine wawili watatu nyumba hio hio wamepona juzi juzi tu.., kibaya utaambiwa wameshamaliza dozi ila hawajapona kwa hiyo wanaendelea na sindano.., jamani kwengine vipi huko..?

Sio Dar es alaam tuu .ata Arusha malaria unakunywa dawa malaria hiko pale pale .Dawa ni feki TFDL wameshaingizwa kwenye ufisadi .dawa nyingi sasa hivi ni feki
 
Back
Top Bottom