Mlipuko wa CHADEMA watokea Mtaa wa Mavurunza, Kimara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlipuko wa CHADEMA watokea Mtaa wa Mavurunza, Kimara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by amba.nkya, Feb 22, 2012.

 1. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  WanaJF

  Jumamosi iliyopita kulitokea Mlipuko wa CHADEMA kwenye Mtaa wa Mavurunza, Kata ya Kimara ikiwa ni muendelezo wa kuimarisha, kuendeleza na kudumisha CHADEMAambako kulifanyika Mkutano wa hadhara wa CHADEMA Tawi jipya la Mavurunza kama ni Maandalizi ya uzinduzi rasmi na harambee kwa ajili ya ofisi ya Tawi hilo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi ya wiki hii kwenye Mkutano mwingine wa Kata ya Kimara. Awali, Mh. Dr. Wilibroad Slaaa alitarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye Mkutano huo wa Kata Jumamosi ya wiki hii ingawa bado haijathibitika kama atahudhuria au atateuwa mwakilishi wake.

  Akisoma Risala Mwenyekiti wa Tawi hilo ambaye pia ni muasisi wa Tawi hilo na mwanaharakati wa Maendeleo, kwenye Mkutano huo wa hadhara mbele ya Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kimara Mh. P. Manota; Mwenyekiti huyo alisema katika jitihada za kuhamasisha wananchi kujiunga na CHADEMA, tayari walipatikana wanachama zaidi ya 150 na bado kuna wananchi wengi wameshawishika kujiunga na chama hicho. Aidha, kwenye mkutano huo kulikuwa na wanachama wapya wengi sana walijitokeza kujiunga na CHADEMA ikiwa ni pamoja na wajumbe wa mashina kutoka CCM. Hadi kufikia usiku bado wananchi waliendelea kuorodhesha majina yao na kuchukua kadi za CHADEMA kutoka kwa Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA mkoa wa DSM.

  Mkutano huo wa Jumamosi iliyopita ulihudhuriwa pia na makamanda wengine ambao ni Madiwani (CHADEMA) kutoka kata za Saranga, Makuburi, Ubungo, Sinza, Viti maalum na Mwenyekiti wa Wilaya Kinondoni. Makamanda hao ndio waliokuwa walipuaji wakuu wa masuala yanayohusu hali mbaya ya uchumi wanchi hii kutokana na Utawala wa Chama tawala (CCM) ikiwa ni pamoja na kuanika hadharani tuhuma za kifisadi dhidi ya Diwani wa zamani wa Kata ya Kimara (CCM) na Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Mavurunza (CCM). Mikutano hii ni sehemu ya Operation Ondoa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.


  WITO: Ukiwa kama Mwanachama, Mdau na Mwanaharakati wa Maendeleo unaombwa kuhudhuria Mkutano wa Kata ya Kimara Jumamosi ya wiki hii tarehe 25 Februari 2012 kwaajili ya uzinduzi wa matawi kadhaa ndani ya Kata hiyo.
  Taarifa kamili kuhusu mkutano huu ikiwa ni pamoja na Mgeni rasmi, Ratiba na namna ya kufika kwenye eneo la tukio nitawasilisha mapema kesho. KARIBUNI SANA…!  Nawasilisha….!
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Rekebisha kichwa cha habari hapo! Mlipuko wengine hatujasahau Gongo la Mboto na Mbagala
   
 3. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Tuko pamoja kamanda, tutatia timu na nitaamashisha makamanda wengine wanaoishi kata za jirani (Makuburi/Segerea) kuhudhulia

  CHADEMA mwanzo mwisho
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mripuko wanini? kanjanjanja ni kanjanjanja tu.

  mlipuko = mripuko
   
 5. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kila la kheri makamanda, kama spidi hii ccm kazi watakuwa na shughuli pevu 2015.
   
 6. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Thanks Kamanda
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongereni sana wana Kimara
   
 8. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kamanda wa kweli hajali haya, nipo kikazi zaidi, CDM inasonga mbele....!
   
 9. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ahsante Mkuu, jitahidi uje basi
   
 10. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Usihofu Mchungaji, saa ya ukombozi yaja, kama sio hapa duniani basi mbinguni...teh.teeh...!
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Taarifa njema!
  Kidogokidogo, hatimaye tutafika tu!
   
 12. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Thanks PJ, nitafurahi sana kukuona Mkutanoni Mkuu.
   
 13. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,934
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Makamanda tupo pamoja front no back hadi magogoni tutatinga viva people's power!
   
 14. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kamanda, hadi kieleweke, magamba wanahaha
   
 15. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona umechelewa kuleta taarifa?Jf huwa ya kwanza kujua jambo lolote linalotokea nchi hii,poa mkuu tunashukuru kwa taarifa!
   
 16. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Vipi kin'go'ngo je?
   
 17. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Usijali Mkuu, tusubiri Ratiba kesho, ingawa sina uhakika na King'ong'o.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Juzi juzi ilikuwa Igunga, huko nako kusonga mbele, halafu ikaja Uzini, huko nako ni kusonga mbele. Kurudi nyuma inakuwaje?
   
 19. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Aisee mi nilivyoona hicho kichwa ilibidi nimpigie ndugu yangu aliyeko huko kimara mavurunza. Nimemuuliza kama kweli kulitokea mlipuko akashangaa kwani hana habari hiyo...Kumbe mlipuko anaozungumzia huyu jamaa sio ule niliokuwa naufikiria!
   
 20. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Keep it up! Congrats!
   
Loading...