Mlipuko ulisababishwa na kombora kutoka nje?

Kuna nyingine zimevuja leo zinasema...

'section of intelligence suggests the incident was planned to divert public attention from that of discussing Dowans payment and power blues'
.
duh! Sifikirii kama binadamu wanaweza kuwa wabaya kiasi hicho.
 
Mara baada ya tukio la Gongo la Mboto kutokea maelezo ya kwanza (kina Kova na wenzake) walianza kutuambia ni "ajali". Baadaye taarifa zilitoka kwamba siku tatu kabla yake ulifanyika ukaguzi na kuhakikisha maghala yale yako salama na hakukuwa na dalili lolote la tatizo. Hivyo, tunakabiliwa na maelezo yafuatayo:

a. Ukaguzi haukuwa makini ilivyotakiwa (yaani wa kubabaisha) - uzembe!
b. Ukaguzi haukufanyika kama ilivyotakiwa (wa kuharakisha) - uzembe
c. Ukaguzi ulifanyika kwa kiwango kinachotakiwa na hakukuwa na tatizo lolote - JWTZ linasafishwa
d. Mtu/Watu wa ndani ambao walikuwa wanajua hali ilivyo waliamua kusabotage maghala kwa sababu zao - ughaidi
e. Mtu/watu wa nje ambao wanajua uwepo wa hiyo ghala na waliamua kusabotage kwa kutumia silaha - ughaidi.

Ninajiuliza maswali hayo kwanza kutokana na upekee wa tukio lenyewe lakini vile vile tukiangalia hali ya kisaikolojia miaka hii michache ambapo tumeona wanajeshi wetu (Polisi na Jeshi, na hata magereza) wakipatwa na msongo wa mawazo kiasi cha kutumia silaha kujidhuru wao wenyewe. Pendekezo kuwa hili laweza kufanywa na mwanajeshi linakuwa ngumu hasa baada ya taarifa kuwa hakuna mwanajeshi aliyekufa (japo hawasemi hakuna aliyedhurika).

Hivyo, njia pekee ya kuwaaminisha wananchi kuwa tukio hili halikuwa ughaidi ni muhimu (kama ilivyoamuriwa) kuleta chombo cha nje na huru kuchunguza na kutoa taarifa. Haiwezekani na taarifa ya Gongo la Mboto kuwa kificho tena. Tunahitaji kujua kiilichotokea, tunastahili kujua kilichotokea.

Lakini katika upande wa kusababisha madhara makubwa kwa wananchi hili halina mjadala - ni uzembe uliokubuhu wa viongozi walioko madarakani. Naungana na wale wanaotaka Dr. Mwinyi ajiuzulu na pamoja naye Katibu Mkuu MoDNS Bw. Andrew Nyamuso???

hata kama ghala zingekaguliwa mara 100, kama ni meteorite, hakuna kitu wangeweza kufanya! Hapo hakuna uzembe wowote. Je mbona hamkulia na resignation ya mtu yeyote kwenye yale mafuriko ya Morogoro? Tofauti yake ni nini?
 
g ni pull ya gravity. Ina-vary sehemu mbalimbali duniani. Lakini kumbuka averagely wanasema ni 10g, yaani 10m/s^2. Kwa hiyo kitu kikiwa kinadondoka lazima ki-accelerate mpaka pale kinapofika terminal velocity which is caused by friction with air.
Kwa hiyo hata wewe ukianguka kutoka kwenye ndege, lazima uta-experience hiyo acceleration due to the pull of gravity.

kama sikosei argument yangu ilianzia hapa
V=u +at, nikasahau kuna ishu ya linear motion na free falling object(sijui v=u-gt).
Tatizo haya mambo tulibeba tu hakuna application!
 
kama sikosei argument yangu ilianzia hapa
V=u +at, nikasahau kuna ishu ya linear motion na free falling object(sijui v=u-gt).
Tatizo haya mambo tulibeba tu hakuna application!

yea...ambapo a = g in this case. wewe ulisema hakuna acceleration ambapo ingekuwa v = u
hii ndio maana ukienda angani ukaangusha tani 1 ya mawe na jiwe moja, vyote vitafika ardhini na spidi moja. in this case u = 0. kwa hiyo v = gt. and since g is constant to all objects na time itakuwa constant kwa sababu umeangusha at the same time, vitakuwa na v moja.
by the way...mimi sio physics major. Ila hizi ni basic concepts na vizuri tuna-refresh memory. It's good kujua vitu mbalimbali maana knowledge ni power.
 
GHILIBA ZA SERIKALI KUTAFUTA VISINGIZIO KUTANGAZA HALI YA HATARI
KUUA MOTO WA KUDAI TATIBA NCHINI HAIKUBALIKI


Hii dhana inayojitokeza hivi sasa kwamba kuna mtu mmoja Tanzania nzina (kwa jina la Dr Mbura) kuona kitu cha ajabu angani mda mfupi kablaa mabomu kuanza kulipuka Gongolamboto na sasa kudeshesha wazo kwamba huenda tulishambuliwa kutoka nje ya nchi yote niwazo la hatari sana na yakemewe sana na wapenzi wa demokrasia nchini.

Ni wazi kwamba pindi mawazo ya ajabu ajabu na kauli za KINAJIMU HIZI zote ni katika KUTAFUTIA SERIKALI KISINGIZIO CHA SERIKALI YA KIKWETE KUTANGAZA HALI YA HATARI ili kuua moto wa kudai KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI zote kupitia bungeni.

Wa-Tanzania tuamke na tuangalie sana hizi ghiliba wakati wananchi wenzetu wanapotezeshwa uhai hivi!! Tukumbuke haya yote yanatokea wiki moja tu tangu Lowassa kupewa uwenyekiti wa kamati hiyo bungeni, tukiwa katikati ya moto wa kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na hatua dhidi ya mafisadi.

Hakuna aliyetarajia huyu bwana kupewa kiti nyeti kiasi hicho kwa taifa letu mbali na shutuma lukuki shingoni mwake!!
 
Back
Top Bottom