Mlipuko mkubwa umetokea leo majira ya saa 1.30 usiku katika baa maarufu ya Arusha night park "Matak0 bar" iliyopo eneo la Mianzini mjini Arusha.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa mlipuko huo unatokana na bomu lililotengwa katika eneo la bar hiyo na kujeruhi watu zaidi ya 20 waliokuwa wakiangalia mchezo wampira wa miguu ligi kuu ya England kati ya Chelsea na Swansea.
Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya dk. Mohamed na Mount Meru. Mashuhuda wanaeleza kuwa kuna baadhi ya majeruhi wamekatika viungo kama miguu nakadhalika.
Hili ni tukio la tatu mjini arusha bomu kurushwa na kutegwa katika maeneo ya mikusanyiko ya watu na hadi sasa Polisi hawajawahi kukamata wahusika wa matukio yote matatu.
Kitu kama bomu kimelipuka Hapa Arusha maeneo ya MTK Bar Mianzini na kusababisha mshindo mkubwa sana.
Taarifa zinasema baadhi ya watu wameumia.
watu wote wameshatawanyika...wikiendi Arusha imevurugika....
Mkuu huu uchoyo wote wa nini?? Si ungejinyamazia tu? Si lazima uwe wa kwanza kurepoti jambo. Utakuwa wa maana ikiwa utaleta ripoti yenye mifupa na minofu juu yake. Siyo Skeleton. Eleza jambo tulielewe. Wengine tuna ndg huko. Wengine bado tuna mawazo fresh ya Olasiti na Unga ltd. Usitupandishe BP bure.
Mwingulu yuko wapi jamani??? Hivi yupo bungeni kweli naona kakaa kimya saana this week. Aisaidie polisi kubaini chanzo wasije sema ni kitu kibutu kwani Chagonji hachelewi
Kitu kama bomu kimelipuka Hapa Arusha maeneo ya MTK Bar Mianzini na kusababisha mshindo mkubwa sana.
Taarifa zinasema baadhi ya watu wameumia.
- Jamani mbona nipo hapa ndio kwanza tumetoka mpirani na sijasikia kitu mkuu au?
Le Mutuz System
Asante PK kwa kuendelea kuifanya jf, "be the first to know!".Kitu kama bomu kimelipuka Hapa Arusha maeneo ya MTK Bar Mianzini na kusababisha mshindo mkubwa sana.
Taarifa zinasema baadhi ya watu wameumia.
Well spoken bro!Asante PK kwa kuendelea kuifanya jf, "be the first to know!".
Endelea kufuatilia tukio hilo, haswa chanzo cha mlipuko na matokeo!.
Usiwajali watakaokulaumu kwa nini umeleta habari nusu, hao wamezoea kula chakula kikiwa kimeishaiva, na kupakuliwa kwenye sahani, wao kazi yao ni kula tuu, sisi ambao ni wapishi, hata chakula kabla hakijaiva, huonja kwanza, hivyo tunakushukuru kwa kutuonjesha, tunakisubiri kiive utupakulie tule!.
Pasco