Mliosomea/mnaosomea India njooni hapa mumshauri huyu

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
724
551
Jamani kwa wote mnaosomea India au mliowahi kusomea India ninaomba mtushauri kitu hapa mimi na mdogo wangu.

Mdogo wangu amepata skolashipu anatakiwa aende India masomoni huko Mangalore tunaomba anayepafahamu atujuze vitu kama utamaduni wa huko, maisha kwa ujumla wake na tumuandae vipi kisaikolojia mdogo wangu kwani toka azaliwe hajawahi toka nje ya nchi na shule zote alizosoma ni za kawaida sana.

Alimaliza digrii ya kwanza hapo UDSM na huko India ameitwa kusomea digrii ya pili.

Ushauri wenu wakuu.
 
Ubaguzi tu india wabaguzi sana ndio shida yunayoipata uku ila izo ni changamoto ndogo ndogo tu ambazo zinaepikika na maisha india kawaida tu kama bongooo ni rahisi kukabiliana na mazingira
 
Ubaguzi tu india wabaguzi sana ndio shida yunayoipata uku ila izo ni changamoto ndogo ndogo tu ambazo zinaepikika na maisha india kawaida tu kama bongooo ni rahisi kukabiliana na mazingira
Asante sana kwa kunitia moyo!Unajua mdogo wangu tokea apigiwe simu na kuletewa barua yake amekuwa na mawazo sana maana kuna watu wanamtisha sana.
 
Ajitahidi afate kilichompeleka maana akijaribu kuingia mahusiano na watu wa kule kiukweli tutampoteza awe wa kike au wakiume
Kuna kijana mmoja alijiingiza kimahusiano na binti wa kihindi kilichomtokea alirudishwa maiti
Pia aiweke akili yake sawa kukubaliana na ubaguzi wa rangi haswa kwa sisi waafrika, aone ni jambo la kawaida kabisa
Zaidi ya hayo ni mtie moyo aende tu,nice studies kwake
 
Aanze tu kufanya mazoezi ya kula vyakula vya pilipili.kama ni wakike mumkanye tu maana wanakuja wastaarabu lakini kampani zinawaharibu,pia akae mbali na wapopo
Hapana yeye ni wa kiume!Hao wapopo ni watu gani,naomba unifahamishe!!
 
Ajitahidi afate kilichompeleka maana akijaribu kuingia mahusiano na watu wa kule kiukweli tutampoteza awe wa kike au wakiume
Kuna kijana mmoja alijiingiza kimahusiano na binti wa kihindi kilichomtokea alirudishwa maiti
Pia aiweke akili yake sawa kukubaliana na ubaguzi wa rangi haswa kwa sisi waafrika, aone ni jambo la kawaida kabisa
Zaidi ya hayo ni mtie moyo aende tu,nice studies kwake
Aisee,yaani ninakushukuru sana kwa kututia moyo kiutu uzima.Na ninashukuru kwa kutupa angalizo hilo la huo mkasa wa kusikitisha.Ninamwombea kwa Mungu huyu dogo awe mwangalifu sana na afuate kilichompeleka!!!!
 
Bangarole ni jiji kubwa yawezekana kama dar ila lineendelea kidogo sababu ya good infrustructure. Ila kama kawa wahindi wachafu sana. Sio ajabu kuona mtu anakojoa katikati ya barabara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom