Mliosomea/mnaosomea India njooni hapa mumshauri huyu!!!!!

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
726
564
Jamani kwa wote mnaosomea India au mliowahi kusomea India ninaomba mtushauri kitu hapa mimi na mdogo wangu.Mdogo wangu amepata skolashipu anatakiwa aende India masomoni huko Mangalore tunaomba anayepafahamu atujuze vitu kama utamaduni wa huko,maisha kwa ujumla wake na tumuandae vipi kisaikolojia mdogo wangu kwani toka azaliwe hajawahi toka nje ya nchi na shule zote alizosoma ni za kawaida sana.ALIMALIZA DIGRII YA KWANZA HAPO UDSM NA HUKO INDIA AMEITWA KUSOMEA DIGRII YA PILI.USHAURI WENU WAKUU.
 
Nampa hongera kwa kuchaguliwa kuendelea na Masomo, kuna ndugu zangu wengi wamemaliza vyuo huko, yeye azingatie kilicho mpeleke that's all! Nchi ya ugenini lazima uwe na hekima na busara! Na nyinyi mnaobaki mumkumbuke kwa maombi mara kwa Mara haswa mama yake amwombee sana mwanae! Namtakia kila la kheri hamna linalo mshinda Mwenye Enzi Mungu
 
Maisha ya huku ni kuwa na uvumilivu kuna wahindi wanauzi na wanakuchukulia unahela do umakini uwepo.

Kuiheshimu hela maana rupii inakatika haraka.

Cha kufanya ni kununua stock ya mwezi mzima ya chakula kuiweka ndani.

Usipende kugombana nao kama kupigana nao maana hata wakikuua hawana kesi na ubalozi sijaona ukifuatilia haya mambo.

Awe na akili yake na ajue kafuata nini huku asisahau hilo. Starehe zipo na ule ufree upo kupanga ratiba vizuri tu

Kimasomo wapo vizuri na wanajitolea kufundisha ma professor. Fika huku soma hicho unachosoma ma unaweza kuongeza kozi za pembeni ni bei rahisi kuliko Tz.

Nisehemu nzuri ishi na watu vizuri waafrica ni wengi na Watanzania wakiwemo. Tunaishi ka ndugu usiwe mtu kujiweka ubinafsi. Hayo tu mengine utaniuliza ni kwambie...

Karibu jiji la Mahatma Gadhi
 
Kuna taasisi kama Global Educational Link na Universities Abroad Link (kama sijakosea) ambazo zinapeleka wanafunzi nje pamoja na India. Hawa nina amini watakupa ushauri mzuri kabisa pamoja na ubora wa chuo aendacho na jinsi ya kuchunga usalama wake. Hebu google au aulizia (nimewaona mara nyingi kwenye TV, naamini wanajua wanalo liongelea).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom