Mara nyingi matatizo yanafana.hasa hasa vijana tunapata changamoto kubwa kwenye ndoa!inabidi watu wafahamishwe kwamba ndoa ni safari.Safari ambayo tamu na ni hatari!safari ambayo tamu ndiyo maana tunapongezana(ndugu yangu ehhh hongera kwa kuoa au kuolewa)lakini ujue kwamba na utamu wa safari hiyo umechanganyika na uhatari.Sasa sisi tunaitizama ndoa kwa jicho moja tu! Mtu anaenda ku enjoy(kufurahia) amepata jiko au amepata mume,mwenzetu amepata mwanamke mzuri au mume mzuri,sifa tofauti tofauti,hatutizami upande mwengine ambao wa matatizo.chukulia mfano wa kusafiri na ndege tu! Kwa waliowahi kusafiri na ndege,ile hatari yake ndiyo iliyowafanya watu (wahandisi)kukaa na kupanga mikakati ya chombo kile(ndege)na umadhubuti wake.Ni safari tu ya masaa 6 pengine zaidi au chini ya masaa hayo,lakini wewe angalia tu ndege yenyewe ilivyotengenezwa,watu wakawa na uhakika wa asili mia moja (100%)wakaona hapa tumefikia katika uhakika wa chombo hichi(ndege)lakini bado kuanzia yale mazingira mpaka unaingia kwenye ndege yote yanakuonyesha unaingia katika safari hatari ya ndege.kuanzia pale Air port ule ulinzi uliokuwepo,unaambiwa usivute sigara,usiwashe mitambo yako na zile checking zote n.k,na bado ukiingia kwenye ndege kuna matangazo mkanda ule na kutovuta sigara na unaambiwa kuna baadhi ya vitu hivyo ukiviona vinashuka weka puani mwaka utavuta hewa ya oksijen fanya mwenyewe kwanza kisha umsaidie na mwengine yaani unapewa maelezo mengi kiasi ambacho unaweza kujiuliza kwani sisi tuna kwenda wapi au tunakwenda kufa?


.lakini yote yale unaambiwa ujitambue upo katika safari hatari.ikiwa safari ya ndege ni kama hivyo ni masaa kadhaa je safari ya ndoa? Safari ambayo utasafiri umri wako wewe wote uhatari wake sasa ukoje? ni nani ambaye anatupa instruction(maelezo)yake ikitokea moja tufanye nin?vijana tunasoma wapi kabla ya kuingia katika ndo?,ni nani anatufundisha namna ya kuingia katika suala hili.watu huoa au kuolewa kwa mambo makuu manne na haya nikitaka niyatolee na ufafanuzi ni somo kubwa sana labda nianzishe mada nyengine,la kwanza mali yake la pili uzuri wake la pili ukoo wake na la mwisho la nne ni tabia. Kwa hayo hapo ukisikia mtu kaoa lazima mojawapo limepatikana.muhimu ni kuzingatia misingi bora ya kuchagua kwa sababu ni patner off life(mshirika wa maisha)kwa sababu ni safari ambayo ni hatari inaweza kupigwa na mawimbi makubwa mara mtu anaweza kusema bora nife au afe yeye,jambo ambalo mara nyengine hupelekea vita siyo ya mke na mume tu! Mara nyengine huingia vita ya familia zote mbili ile ya mume na ya mke,vita ambayo familia zinaweza kupigana na kuuana,tatizo ni wana ndoa tu.baba akatoka huko na panga na mwengine akatoka na kisu wanataka kupigana kwa sababu ya ndoa ya mtoto wao, inaweza kufikia mahali mpaka kabila nzima! Ya bwana harusi ikawa na ugomvi na kabila nzima ya bibi harusi.kwa hiyo ndugu zangu mara nyengine sisi tunakosea hesabu kwa kumtizama mtu sura,mazingira au kipato chake halafu tukahukumu huyu mtu anafaa au hafai,kwa kutizama tu!. Wazee wa zamani ukitaka kuoa mpaka wajue unatoka nyumba gani kwanza,siyo kama sisi tunaojiita wa kidigital tunakutana kwenye social network na kuoana humo humo


ndoa inatimia.mtu hajawahi kujua anatoka wapi anishi wapi mzee wake nani? Baasi maisha yanakwenda na wengine wanasikia sauti tu,kapiga mwanamke kakosea namba kapokea ni mwanaume basi kashampenda kwa sauti ile,hajui kama ni kipofu wala hajui yupo vipi basi yeye anasema tu nipo tayari mimi kukuoa

.miongoni mwa wanawake mwa wanawake 35 ambao waliwahi kuhojiwa aliwahi kusema mume wake hamshughulikii kabisaa anamuona kama ni takataka isipokuwa anapohitaji tendo la ndoa tu ndipo anakuwa mtu wa sawa kabisa.vijana haya ndiyo matatizo asilimia kubwa tunayo,unamuona mume anatoa mashairi mazuri na mke naye anajua mume wangu leo anahitaji kitu fulani,hapo ndiyo na yeye anapoomba vitu ambavyo hana kama ni viatu n.k. Sasa munaishi hivyo hapo pana ndoa au ndoano? Basi mjue pale mulipoanziana mwanzo kabisa muliharibikiana pale pale.ikiwa mtu anataka apate furaha ya ulimwengu apate mke bora na upande wa mume nao apate mume bora.Atasahau shida zote kwa sababu mwenzake aliyekuwa naye katika safari ile ni mwenzake ambaye anafaa na ni mwenzake ambaye amemchagua.Tujitahidi tupate elimu ya ndoa jamani,siyo kukurupuka tu unasema kesho unaoa au unaolewa.nani anaweza kuendesha gari bila kulisomea au kupata mwalimu,unaambiwa usi overtake kwenye mlima au kwenye kona bila kusoma utajuaaje?.ndoa yoyote haina upendo haina utulivu,haina huruma hiyo usiite ndoa.lazima mume amuhurumie mkewe na lazima mke amuhurumie mumewe.
