Mliooa mlipataje wake zenu?

Big Tymers

Senior Member
Jun 25, 2016
109
76
Mimi ni kijana wa miaka 32 nimesoma university level, ni mfanyabiashara nimeweza kufanya maendeleo makubwa. Jambo ambalo limenishinda ni jinsi ya kupata msichana wa kuoa, kwa kweli hili jambo limekuwa ngumu kama kurusha satellite.

Mlioa jmn tupeni mbinu za kumpata wife material
 
Mfate unaempenda mwambie unampenda akikataa mwambie uwe rafiki yake
 
Mimi ni kijana wa miaka 32 nimesoma university level, ni mfanyabiashara nimeweza kufanya maendeleo makubwa. Jambo ambalo limenishinda ni jinsi ya kupata msichana wa kuoa, kwa kweli hili jambo limekuwa ngumu kama kurusha satellite.

Mlioa jmn tupeni mbinu za kumpata wife material

Unaanza kwa nyumba za Ibada kupiga maombi ya nguvu ukiona hailipi unahamia " mlingotini " pande za Tanga na Bagamoyo kwa kufanya " ndumbaism + miziziology ".
 
Oa kutoka kwa wadada wanaokuzunguka...marafiki, marafiki wa marafiki, marafiki wa ndugu zako, work patners, etc. Ni bora sana kuoa patner ambaye background yake inajulikana au unaweza track historia ya familia/vizazi vyake.

Ila mshirikishe sana Mungu. Yeye ndiye atakupa mke mwema bila kujali hayo niliyoyasema hapo juu yanatimia au la. Ngoja nikueleze namna mimi nilivyooa. Unaweza kujifunza kitu hapa.

Nilionana na wife wakati nipo chuo kikuu. Yeye alikua anauza duka la home kwao jirani na kwa uncle wangu ambapo nilikua naenda mara kwa mara bumu likiisha.

Uncle alikua na kawaida ya kuniachia funguo pale shop. Ndipo nikazoena na binti ambaye baadae alikuja kuwa wife kwa namna ambayo sikuitarajia.

Mwanzo wa uhusiano sikudhani hata siku moja ningekuja kumuoa. Nilimuona kama hana vigezo vingi nilivyohitaji. Pia ukweli kuwa tunapishana sana viwango vya elimu vilinifanya nisimfikirie kama wife material. Sana sana upendo wangu kwake ni kwakua ilikua nikiondoka kurudi chuoni basi nitafungashiwa mazagazaga kibao ya kutumia chuoni. Alinijali na kunipenda sana. Kwa upande wangu nilikua namtumia tu.

Si kitambo sana nikampa mimba (nilikua nimemaliza chuo nipo tu hapo kwa uncle kazi sina). Wazazi wake walichachamaa kweli na uncle aliwaunga mkono kwa namna fulani. Kilichotokea nilifungishwa ndoa ya mkeka.

Kama kunisaidia uncle alinipangishia chumba na sebule na kunipa mtaji wa kuanzia maisha. Mwanzoni maisha yalikua magumu sana hadi nilitamani kumkimbia huyu binti, ukichukukia sikumpenda kivile. Ila kuna kitu kilinizuia mara zote nilizofikiria kumkimbia.

Maisha yaliendelea. Kila siku bond yangu na mke wangu iliongozeka. Tuliivana. Aliniheshimu sana na kunisikiliza. Alinishauri na kunisaidia kimaisha. Alikua na akili ya biashara. Alikua mbunifu sana (hata biashara ambayo imetutoa kimaisha lilikua wazo lake).
Kidogo kidogo nikaanza kumpenda kweli (you can learn to love). Japo shida ndogondogo zilikuwepo kama kutojiamini (elimu), nk ila nilimtengeneza kuwa wife i wanted. Bahati nzuri alikua mtoto wa mjini so alicop haraka kuendana na mimi.

To cut story short, sasa ni mwaka wa tisa tupo pamoja. Tuna watoto wawili. Hatujawahi kupigana. Sijawaji kumpiga. Hatujawahi eti kusuluhishwa au hata kuwa na kesi kwa wazazi, marafiki au hata majirani. Nampenda sasa kuliko kipindi chchote. Naye ananipenda. We are happy family mpaka jamaa zangu waliooa asali wao wa moyo, wake wenye digrii, kazi nzuri, nk wanakuja kutuomba ushauri how to live happily kwenye ndoa.

Mke mwema atatoka kwa Mungu mdogo wangu.
 
Teh teh, naona rushwa ya mapenzi ilihusika
 
Mimi ni kijana wa miaka 32 nimesoma university level, ni mfanyabiashara nimeweza kufanya maendeleo makubwa. Jambo ambalo limenishinda ni jinsi ya kupata msichana wa kuoa, kwa kweli hili jambo limekuwa ngumu kama kurusha satellite.

Mlioa jmn tupeni mbinu za kumpata wife material
Kitu cha kwanza omba sana kila siku uwe mwaminifu kwa Mungu ktk maombi na kuweka nadhiri naye.Pili mshirikishe mtu unaaemwamini muwe mnaomba pamoja na mchungaji wako pia maana bwana anaeza kuzungumza nao pia .Pili hakikisha wewe ni mwaminifu pia then utapata wa kufanana na wewe Mungu hadanganyi ndugu akisema nitakupa wa kufanana nawe amini.Tatu usiwe na vigezo vile vya nje zaidi angalia ndani yake yukoje,kuwaza,kunena,kutenda,mitazamo na uhusiano wake na Mungu ,anamuelewaje ktk mambo mbalimbali na anamchukuliaje Mungu,Rafiki zake,mahali anapopenda kwenda,ni mtu wa kujichanganya ama la,anaishije na watu wake wa karibu ,responce yake ktk shida zako na hivi vitu vinahitaji muda kidogo kuvijua at least 2 yrs.Nakwambia hivi nina ushuhuda jinsi nilivyompata patner wangu in life haikutegemewa tulikutana njiani tu kila mtu akiwa kwenye hekaheka zake though tulisomaga wote chuo so ikawa easy yeye kunirecognize b4 mimi then tukawa marafiki wa kawaida kabisa tunapiga story za maisha like a year hakuna aliemchukulia mwenzie like a patner kumbe wote tulikua single bahati nzuri and love ilianza kuonekana slowly it takes sometime to prove if he is the kind of person that God promised me through prayer tulikaa like 3yrs then tukaoana .The rest is histry .And i never regret to have this person in my life sababu sasa hivi tumeshikamana na Mungu kuliko chochote na good enough tunafanana tabia so we are not strugglin.Kweli Mungu ni mwema nakuombea sana.
 
hata mimi sielewi walioolewa walipataje wa kuwaoa nimejaribu nimeshindwa naishia tu kuwa mchepuko wa muda
hahah heri yako unagusa shimo la Mungu, we chamsingi tafurta mchepuko mkali ambao unajua unafaa tuwa mkeo utie mimba halafu tulia tuu atajileta
 
huyu jamaa nishamsoma ni muoga/domozege chamsingi hapo jichanganye sana na wanawake kwanzia ma group ya whatsaap n.k utapata uzoefu tuu mwisho wa siki utachukua chombo chako safi chumbani kula.
 
hata mimi sielewi walioolewa walipataje wa kuwaoa nimejaribu nimeshindwa naishia tu kuwa mchepuko wa muda
Umemaliza kila kitu mtoa mada yabidi akutafute pembeni msemezane tu...Na hivi ndivyo itakuwa mlivyokutana...
 
Ukiwa Husband material ni rahisi kupata Wife material.

Usipokuwa Husband Material huwezi pata Wife material mana hakuna kilicho bora kikataka kuchangamana na kibovu.
 
Dah yaani hata mimi nashindwa kupata jibu.
Naona kama nimefeli kupata mke wakati uhakika wa maisha upo.
Namudu gharama za maisha kwa asilimia nyingi.
 
Back
Top Bottom