Oa kutoka kwa wadada wanaokuzunguka...marafiki, marafiki wa marafiki, marafiki wa ndugu zako, work patners, etc. Ni bora sana kuoa patner ambaye background yake inajulikana au unaweza track historia ya familia/vizazi vyake.
Ila mshirikishe sana Mungu. Yeye ndiye atakupa mke mwema bila kujali hayo niliyoyasema hapo juu yanatimia au la. Ngoja nikueleze namna mimi nilivyooa. Unaweza kujifunza kitu hapa.
Nilionana na wife wakati nipo chuo kikuu. Yeye alikua anauza duka la home kwao jirani na kwa uncle wangu ambapo nilikua naenda mara kwa mara bumu likiisha.
Uncle alikua na kawaida ya kuniachia funguo pale shop. Ndipo nikazoena na binti ambaye baadae alikuja kuwa wife kwa namna ambayo sikuitarajia.
Mwanzo wa uhusiano sikudhani hata siku moja ningekuja kumuoa. Nilimuona kama hana vigezo vingi nilivyohitaji. Pia ukweli kuwa tunapishana sana viwango vya elimu vilinifanya nisimfikirie kama wife material. Sana sana upendo wangu kwake ni kwakua ilikua nikiondoka kurudi chuoni basi nitafungashiwa mazagazaga kibao ya kutumia chuoni. Alinijali na kunipenda sana. Kwa upande wangu nilikua namtumia tu.
Si kitambo sana nikampa mimba (nilikua nimemaliza chuo nipo tu hapo kwa uncle kazi sina). Wazazi wake walichachamaa kweli na uncle aliwaunga mkono kwa namna fulani. Kilichotokea nilifungishwa ndoa ya mkeka.
Kama kunisaidia uncle alinipangishia chumba na sebule na kunipa mtaji wa kuanzia maisha. Mwanzoni maisha yalikua magumu sana hadi nilitamani kumkimbia huyu binti, ukichukukia sikumpenda kivile. Ila kuna kitu kilinizuia mara zote nilizofikiria kumkimbia.
Maisha yaliendelea. Kila siku bond yangu na mke wangu iliongozeka. Tuliivana. Aliniheshimu sana na kunisikiliza. Alinishauri na kunisaidia kimaisha. Alikua na akili ya biashara. Alikua mbunifu sana (hata biashara ambayo imetutoa kimaisha lilikua wazo lake).
Kidogo kidogo nikaanza kumpenda kweli (you can learn to love). Japo shida ndogondogo zilikuwepo kama kutojiamini (elimu), nk ila nilimtengeneza kuwa wife i wanted. Bahati nzuri alikua mtoto wa mjini so alicop haraka kuendana na mimi.
To cut story short, sasa ni mwaka wa tisa tupo pamoja. Tuna watoto wawili. Hatujawahi kupigana. Sijawaji kumpiga. Hatujawahi eti kusuluhishwa au hata kuwa na kesi kwa wazazi, marafiki au hata majirani. Nampenda sasa kuliko kipindi chchote. Naye ananipenda. We are happy family mpaka jamaa zangu waliooa asali wao wa moyo, wake wenye digrii, kazi nzuri, nk wanakuja kutuomba ushauri how to live happily kwenye ndoa.
Mke mwema atatoka kwa Mungu mdogo wangu.