Mliomshauri rais mmempotosha

Mliomshauri rais mmempotosha

1. Barabara za lami nyingi kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
2. Shule za Sekondari nyingi kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
3. Wanafunzi wa vyuo vikuu wengi kuliko wa awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
5. Waalimu wengi kuliko wa awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
6. Huduma ya afya na vifaa vya afya ni bora kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
7. Watanzania wengi wana kazi kuliko awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
8. Viwanda ni vingi kuliko vya awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
9. Watalii ni wengi kipindi chake na kipato cha utalii ni kikubwa kuliko vya awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
10. Demokrasia ni bora na watu wana uwezo wa kusema wakipendacho kuliko awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.

namba 6 na 8 hapo mmmh......kama afya ingekua bora taifa lisingepoteza mamilion kutibia viongoz nje ya nchi au tusingeskia MSD wakilalamika,
Hapo namba 8 viwanda vimekufa dadangu na unajua wahindi wamegeuza magodaoni,na sera ya viwanda imeshazikwa wala hakuna dalili za kufufua viwanda
 
Anza;

Umeme alikuta 10% tu ya Watanzania ndio wanao, changanya wote wa kabla yake miaka 44b na mkoloni wao, leo hii 35% kwa miaka 9 tu ya Kikwete, na kazi imepamba moto ataekuja ni kusimamia miradi tu.

Kinyerezi moja, mbili, tatu na nne unaijuwa?

Pitia hapa: Orodha ya Miradi ya Umeme Vijijini kwa Mwaka wa Fedha 2013-14

what is the cost of electricity kwa watanzania wa kawaida,kwa sasa huko rural areas wamepunguziwa gharama za kuunganisha umeme ila sasa gharama za luku ni mzigo kwa watanzania wa mjini na vijijini
 
1. Barabara za lami nyingi kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
2. Shule za Sekondari nyingi kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
3. Wanafunzi wa vyuo vikuu wengi kuliko wa awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
5. Waalimu wengi kuliko wa awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
6. Huduma ya afya na vifaa vya afya ni bora kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
7. Watanzania wengi wana kazi kuliko awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
8. Viwanda ni vingi kuliko vya awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
9. Watalii ni wengi kipindi chake na kipato cha utalii ni kikubwa kuliko vya awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
10. Demokrasia ni bora na watu wana uwezo wa kusema wakipendacho kuliko awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
Unachekesha kweli...barabara za lami tena za kiwango cha chini kabisa, shule hazina vifaa vyoyote wala maabara..walimu hakuna maana wanalipa mishahara mbuzi.. wakati deni la taifa linazidi kupaa...hilo li-kikwete lako unalolitetea limeuza kila kitu hapa nchini...imebakia sasa kuuuza na raia maana hakuna alichovakiza..nakushauri ujinyamazie tuu na acha kutetea ujinga...magamba hayasafishiki hata kwa bleach
 
Bafuni ule ni utelezi ambao kila mtu anaweza kuanguka. Hata mie nilishaanguka. Au wewe unaogea choo cha passport size chini udongo pembeni bati ndio maana huwezi elewa tofauti? Ubwege wako huko huko?
Mkuu [MENTION=207338]zumbemkuu na Elli njooni mumuone huyu anaye(k)unya machakani na kushangaa kuteleza kwenye tiles bafuni kwa vile MSALANI kwake ni porini.

Hawa watulie tu msumari uingie vizuri
 
Last edited by a moderator:
Bibie Faizafoxy hapa tunajadili maendeleo ya ugonjwa wa rais wa tezi dume na waliomshauri na sio maendeleo aliyoleta.
 
Mimi nikiwa mganga wa kienyeji nilishangazwa sana kwa daktari aliyemtangaza Rais wangu kuwa hatakuwa dume tena kwa sababu tezi dume limeondolewa na kubaki na tezi jike. Kutangaza jambo kubwa la namna hii si tu ni aibu lakini pia lilimdhalilisha Rais wangu na kumhurumia mama salma kuhusu maisha yake ya ndoa ya baadae Jambo kama linapotangazwa kuhusu Rais wetu inatakiwa utolewe na ufafanuzi wa kina tezi dume maana yake ni nini na athari na faida zake kwa binadamu kuwa nalo au kulikosa ni nini na si kwa namna mlivyofanya ninyi.
Ama kweli jf kuna mambo. Lol😂
 
No. Sio kwamba wamempotosha bali wamemshauri kile alichotaka kushauriwa na kusikia toka kwao.
 
1. Barabara za lami nyingi kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
2. Shule za Sekondari nyingi kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
3. Wanafunzi wa vyuo vikuu wengi kuliko wa awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
5. Waalimu wengi kuliko wa awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
6. Huduma ya afya na vifaa vya afya ni bora kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
7. Watanzania wengi wana kazi kuliko awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
8. Viwanda ni vingi kuliko vya awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
9. Watalii ni wengi kipindi chake na kipato cha utalii ni kikubwa kuliko vya awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
10. Demokrasia ni bora na watu wana uwezo wa kusema wakipendacho kuliko awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.

Sina uhakika na Elimu yako, lakini ukiwa objective utagundua haya:
1. Maisha magumu kwa mtanzania wa kawaida kuliko awamu zote zilizomtangulia
2. Mfumuko wa bei mkubwa kuliko awamu zote pamoja. Tumia 'SI' unit hii: alichukua nchi sukari kilo ikiwa 550/= sasa 2200/= Bia ilikuwa 650/= sasa 2300/= Huo mfumuko ni karibia asilimia 400!!! upo? Mkapa alichukua nchi sukari ikiwa 350= na daladala 300/=akatoka daladala ikiwa 300/= but hata 100 unapanda!
3. Deni la taifa lililoshuka toka 9.6 Bil. US$ (1995) hadi 6.3 Bil US$ na kuelekea kufutwa (2005) limepanda hadi 27 Bil. US$ hivyo habari ya barabara kujengwa kwa mikopo ya WB na IMF hata wewe na ushungi wako ugeweza tu, yaani kuchukua mikopo kwa masifa bila kujali athari zake kwa nchi!! Tazama sasa debt service inakwenda hadi 50years!!!!!!
4. Shule za kata hizo ni za EL hata yeye anajua, yeye alijaribu zahanati za kata akashindwa! Tusubiri na hizi maabara za Sekondari tuone! Desemba si kesho tu...
5. Waalimu yeboyebo wengi zaidi ya awamu zote. Zamani shule za serikali zilikuwa bora kuliko private, sasa ni kinyume Priate ndiyo bora kisa ....
6. Ufisadi mkubwa kabisa zaidi ya awamu zote ukijumlisha pamoja ukazidisha mara kadhaa, uliona wapi rais anayewaambia wezi wa fedha za umma rudisheni then no action? Awamu ya 4 ni unique bwana!
7. Ujangili na uuzaji madawa ya kulevya mkubwa zaidi ya awamu zote ukijumlisha pamoja, tena familia ya Rais ikituhumiwa kuhusika
8. Kushusha kiwango cha kujitegemea kuliko awamu zote pamoja. Leo safari za rais nje ya nchi haziishi kwnenda kuomba omba. Nchi sasa imerudi kuwa koloni la wafadhili, amesababisha kuendelea kuwa ombaomba
9. Nchi sasa haina maamuzi kabisa kuliko awamu zote, Ulaya ndio wanatuamulia mambo yetu
10. Rais asiyejali kuheshimu matumizi ya fedha za umma kuliko awamu zote. tazama safari zake zinavyofuja hela za walalahoi
 
Bibie Faizafoxy hapa tunajadili maendeleo ya ugonjwa wa rais wa tezi dume na waliomshauri na sio maendeleo aliyoleta.

Kwani kila kitu anachokolifanya lazima ashauriwe na mtu jinsi ya kukifanya? Kwani nayeye hana za kwake kupima ushauri anaopewa?
Ameshindwa kuwa hata na za mbayuwayu? Au ile story ya mbayuwayu anaizungumza kama nyimbo za kasuku tu.
Profesory bhana!
 
uchumi wa nchi mmbaya, pesa haina thamani, mahitaji bei juu......garama ya maisha kubwa
nashanga kuna wapuuzi wanaona sawa tu...wanatetea ujinga huuu.
 
Acha kupotosha jamii ni misemo iliyopitwa na wakati...Mungu abawapiga matezi dume shauri ya laana.

Ikiwa kuumwa ni laana, basi yakumbuke haya maneno yao siku ukiumwa.

Usijione leo unatembea na una afya yako basi ukajiona wewe ndio wewe, wanaoumwa leo hii wote ni hivyo hivyo walikuwa wazima na afya zao na hakuna analiyechagulia kuumwa.

Nna uhakika ni mwenye kukufuru tu, ambae anaweza kuyaandika uliyoyaandika, sikushangai.
 
what is the cost of electricity kwa watanzania wa kawaida,kwa sasa huko rural areas wamepunguziwa gharama za kuunganisha umeme ila sasa gharama za luku ni mzigo kwa watanzania wa mjini na vijijini

Naam, gharama ziko juu kwa sababu miondo mbinu iliyowekwa kabala ya ujio wa Kikwete ilikuwa mibovu na ya kutumia mafuta mazito ambayo ni gharama. Utakumbuka kuwa Kikwete alipochukuwa madaraka hata umeme wenyewe ulikuwa shida, mgao kila kukicha.

Hayo yte kayafanyia kazi na sasa kuna bomba la gas kubwa linakuja kwenye mitambo mipya ya kutumia gas huko Kinyerezi na hilo ndio suluhisho la gharama kubwa, kuna mitambo mipya inajengwa huko kiwira ya kutumia mkaa wa mawe, nd=adhani unalielewa hilo.

Usiwe na shaka, Kikwete anatimiza zaidi ya Mega watts 4,000 za umeme kwa muda wake, fananisha hizo na mega watt 1,500 zisizofanya kazi ipaswavyo alizozikuta, halafu urudi na useme, nani zaidi?
 
Unachekesha kweli...barabara za lami tena za kiwango cha chini kabisa, shule hazina vifaa vyoyote wala maabara..walimu hakuna maana wanalipa mishahara mbuzi.. wakati deni la taifa linazidi kupaa...hilo li-kikwete lako unalolitetea limeuza kila kitu hapa nchini...imebakia sasa kuuuza na raia maana hakuna alichovakiza..nakushauri ujinyamazie tuu na acha kutetea ujinga...magamba hayasafishiki hata kwa bleach

Umekosea sana, kama barabara za lami zina kiwango chini, unasemaje kuhusu wakati anaingia madarakani kutoka Dar kwenda Mwanza ilikuwa inabidi upitie Kenya?

Utaweka vifaa shule ni wakati shule zenyewe zilikuwa chache na sehemu zingine hakuna kabisa wakati Kikwete anacchukuwa madaraka? Kwanza unajenga shule, na hilo ndilo alilofanya Kikwete, zaidi ya shule 4,500 za sekondari kwa wakati wake tu, yeye alikuta hazifiki 2,000 kwa miaka yote ya Nyerere, Mkapa, Mwinyi na mkoloni wao.

Umeshapata shule, sasa ni kuzijaza vifaaa, na hilo linafanyika sasa hivi nchi nzima, au hujuwi hilo? leo tunaona shule ya kata zikiwa kwenye kumi bora kwa kufaulisha, dogo hilo?

Kumbuka kuwa hukopeshwi kama huko[esheki, neda benki kajaribu kukopa uone. Ukiona nchi inakopeshwa na deni linakuwa kubwa ujuwe ikanopesheka, na hilo wala sikusumbuwe, naona umedanganywa ukadanganyika. Nenda kakope wewe kama ni rahisi kukopa.

Hicho kilichouzwa kiko wapi? unadanganywa na unadanganyika, nchi haiuziki hakuna anaeweza ibeba Tanzania akaipeleka ukofikiri wewe imeuzwa, anaeweza kujiuza ni binadam vipi wewe hujanunuliwa?

Mimi nimejinyamazia kimya, hapa nachambuwa maendeleo, nabofya kwa raha zangu. Unajuwa kuwa wewe leo unauwezo wa kuingia kwenye mitandaao kiulaini kwa mipangilio mizuri ya Kikwete ya kukuza mawasiliano? naona hilo hulijuwi na wala huwezi kulifikiria kwani unaonesha uko finyu sana.

Una miaka mingapi?
 
Back
Top Bottom