Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Mimi nilimpoteza mama mwaka 2020, nikampoteza mtoto mwaka 2021, mwaka huo huo 2021 mwezi uliofuata nikampoteza baba...haya mambo nikumuachia Mwenyezi Mungu tu na katika kipindi hicho kila jambo unaloliwaza kumbuka kwamba Mungu yupo na unazidi kumuomba yeye akupe uvumilivu na akuvushe salama...pia amini wazazi wapo mahali salama na siku Moja tutaonana katika heriiii ....

Pole sana kwa magumu unayopitia na Mwenyezi Mungu atakuvusha salama.
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Pole sana.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9

Mkuu Mimi mama yangu alifariki akiwa na umri mdogo Sana yaani alikuwa na miaka 32 Mimi nikiwa na miaka 7 tu
 
Ukijizuia kulia hutapona!!lia utoe uchungu ndugu!
Pole Sana kwa msiba huo mzito!

Umenikumbusha mama yangu alifariki nikiwa chuo mwaka wa tatu tukiwa kwenye mitihani ya semester ya mwisho,nilijikaza sikulia,kilichofuatia wiki moja mbele nilianza kulia,pona yangu ilikuwa ni kuhama nyumbani,lakini mpaka leo nikifika nyumbani lazima machozi yananilengalenga.
 
Miaka 17 imepita tangu mama yangu atoke duniani nakumbuka vizuri ulitoka ukiwa msaada mkubwa sana kwangu na ndio nilikuwa nakutegemea kwa kila kitu

Ni uchungu usiyoelezeka nakumbuka nililia sana kwenye ule msiba ila naamini upo sehemu salama nakupenda sana mama yangu na nilikupenda sana ata wewe ulijua ilo
 
Mishe zakufiwa zisikie tu kwa jirani! My parents gone when I was 5yrs! Alianza Dingi 1990 December,karibu na x-mass akafata Maza 1991 pia was karibu na pasaka! Hua nikiona mtu kazinguana na mzazi wake, hua nasema I wish angekua wangu,niite tu japo Mama au Baba! All in all now nipo na maisha yangu,tunasonga taratibu
 
Back
Top Bottom