Nilivyoingia Dar 99, Kupata na Kupoteza dira 04: True Story by Mr X.

Forrest Gump

JF-Expert Member
Jul 2, 2021
584
1,267
Mr X anaeleza;
"Ilikuwa 1999, hapo nimekaa miaka mitatu bila kuona sura ya baba baada ya kwenda kupambana na maisha Dar es Salaam akitokea nyumbani Tarime. Kibaya zaidi baba hakuweza kufanya mawasaliano ya aina yoyote na familia aliyoiacha nyumbani. Umri wa miaka 17, shauku na hamasa vikanizidi, nataka nimuone baba, nataka na mimi nipambane kama yeye, basi nikajiaminisha nitamuona huko huko nikienda. Kwa hio ikabidi 99 nitimke niende Dar bila ya kuaga nyumbani na kibaya zaidi bila kujua naenda kufikia kwa nani"

"70s hadi 80s, baba alikuwa vizuri kifedha. Lakini mwishoni mwa 90s akawa ameshuka zaidi sana na akawa amepata changamoto fulani ya kisheria, hii ilimpelekea kutimkia Dar."

"Nilifika dar salama, nikashuka ubongo na nikapanda dala dala bila ya kujua inaenda wapi. Nikashukia kituoni kinondoni ikabidi hapo ndio nifanye makazi. Ikabidi niingie mtaani, namaanisha nikaanza kutengezeza urafiki na masela wa mtaani. Kulala kwenye valanda, chini ya madaraja ndio, ilikuwa kawaida. Ili niende nao, ikabidi nianze kuvuta fegi na bangi kama wao. Nilifanya hivi ili wasinifutulie mbali"

"Baada ya mwezi kuchill na hawa jamaa, maisha yakazidi kunipiga kwa maana sikuwahi kuishi namna ile. Pia kapesa niliokuwanako kalikuwa kamekaribia kuisha. Ndio hapo nikaanza kuwaza kuhusu stori niliowahi kusikia kuhusu mjomba wake aishie Kitunda. Nikajisemea kuwa ingawa nilikuwa sina plan ya kwenda kwa mjomba inanibidi niende tu kwa maana hali imekuwa sio hali. Basi nikaanza safari ya kwenda kitunda kwa maana nilikuwa namjua mjomba kwa majina mawili basi nikawa na uhakika wa kumpata. Nilifika Kitunda, kipindi hicho kitunda palikuwa hapana raia wengi na wengi walikuwa wahamiaji kutoka Tarime kwa hio walikuwa wanafamiana. Kwa bahati nzuri nikaelekezwa hadi kwake. Nilifika na mjomba aliniona, alifurahi sana na akanichinjia kuku"

"Nilikaa kwa mjomba na kumsaidia katika ufugaji wa kuku. Mjomba alikuwa akinitoa kidogo kapesa kwa shughuli nilizokuwa nafanya. Nilichill kwa mjomba hadi mwaka 2000. Mjomba alikuwa na kijana wa kiume ambaye tulikuwa tunalingana kimakamo. Kijana huyu nae alikuwa anafanya mishe za kuuza mayai na kuku. Kuna siku aliuza mayai na akapata 80,000. Basi akaniambia twende nikupelekee ukaushe rungu mara moja. Ilipofika jioni tulipanda dala dala na kuishia TAZARA ambapo tukachukua ya kwenda temeke. Tulifika sehemu mtaani, tutakuta vyumba vingi na vinavyoaangaliana na mabinti walikuwa wamekaa kwa nje, walikuwa wakijiuza. Jamaa alinipatia 5000, na akaniambia jichagulie. Yeye akajipatia mdada akaingia chumbani. Mimi kwa hofu nikabaki nje, huku wale madada wakaanzaa kunitania na kejeli kuwa mimi siwezi mambo mara mimi ni shoga. Siku ile sikuweza kumchukua kahaba yoyote. Ila baada ya wiki mbili nikarudi na kujiopolea kahaba. Ndio nikajua ile sehemu panaitwa "KWA WAHAYA". Kipindi hicho 2000 au 1000 ndio ilikuwa bei ya kupata huduma ya kahaba pale. Kipindi kile mdada wa makamo mweupe mwembamba alikuwa anaitwa Pili Kiuno"

"Kuna siku niliamua kutembea kutoka nyumbani nikafika hadi majumba sita, nikawa nimefika maeneo ambayo kuna dala dala, nimekaa sina hili wa lile mara namuona baba amepaki hiace akiwa kwa sterling akishusha abiria. Nilimkimbilia baba na yeye alivyoniona akashuka kunikombatia. Baba alikuwa anapiga route ya gongo la mboto-buguruni-k.koo-ferry. Akaniambia niingie kwenye gari tukafika hadi ferry. Tutakashuka akaninunulia chakula ikiwemo na samaki wa baharini ambao nilishindwa kuwala. Baada ya hapo tukarudi hadi majumba sita, nikakuta baba alikuwa anaishi lodge inayoitwa kiseki. Alinitambulisha kwa wale wahudumu ambao baba alikuwa anamla mmoja wao. Baba aliniambia nimuite mama na yule mhudumu naye alijitahidi kunikulimu. Akanichukulia chumba nikalala. Asubuhi nikaamkukia kwenye dala dala yake kama konda. Baada ya siku mbili nilirudi kuwaaga mjomba na kuchukua nguo zangu nikarudi kukaa lodge na baba. Nikaendelea kupambana na baba katika dala dala, hatimaye baba akaanza kufanya mawasiliano na familia nyumbani"

"Kuna binti mzaramo nilianza nae mahusiano wakati nilikuwa pale kwa mjomba kitunda, kipindi niko naishi lodge ndio alikuwa anazaa mtoto wa kwanza na wa wapili akaja kuzaa wakati ndio narudi Tarime. Ila hawa watoto aliishi nao nyumbani kwao"

"Pia Katika harakati ya kwenda kwa wahaya, nikawa nimeopoa binti mmoja ambaye ilikuwa kila mara nikienda lazima nitamfute yeye. Basi ilitokea yule binti kunikubali na mimi kumkubali sana hadi baadae mbeleni kuja kuacha ile kazi ya ukahaba kwa ajili yangu. Sisi tuliendelea kukaa na baba lodge, baba afya yake ikaanza kuzorota mdogo mdogo. Baba alipata ukimwi katika harakati zake kwa maana alipenda sana ngono. Kwa hio ikawa mimi ndio nasimamia gari pale anapokuwa mgonjwa. Baada ya miaka miwili baba akanianchia ile hiace na yeye akanunua nyingine.

"Hii ilipelekea mimi kuanza kipato kizuri. Nikawa napiga route nyingi, kipindi kile hakuna foleni dar, kwa hio unafanya route nyingi kwa muda mchache kupelekea kukusanya pesa nyingi. Nikahama lodge na kwenda kupanga chang'ombe, nikawa naishi na yule binti niliokutana nae kwa wahaya. Tulifanya mambo mengi na yule binti mzaramo, tuliluka madebe hadi billcanas. Kipindi hicho sasa nimeanza kushika vipesa natamba mjini kidogo. Nilinunua kiwanja Boko pia niliweza kujikimu mimi na mpenzi wangu kwa maisha ya kila siku"

"Bata nilikula sana, viwanja vingi nilizunguka. Nguo za phat pharm, fubu etc zilikuwa hazinipiti. Pesa nyingi nilitumia sana kwa ajili ya ngono. Makahaba, wanafunzi, mabinti wa beach etc. Pia kampani mbaya ya marafiki ilionizunguka ndio iliokula pesa yangu sana, kuwalipia pombe na mambo mengine. Kipindi hicho pombe ilikuwa sio kivile kwangu, mimi nilikuwa mtumwa wa ngono"

"Kipindi hicho ndio nilifahamiana na dully sykes pale billcanas na kutokana na ukaribu akanionganisha na nikawafahamu wakina luteni kalama na ferouz. Ilikuwa siku za juma pili naenda kumtembelea dully mtaani kwao kariakoo. Kipindi kile ana kipiki piki kidogo"

"Afya ya baba ikazorota, akawa hana akiba zaidi ya kuendelea kujiuguza, ikabidi tuuze hiace yake ili ikidhi bills za hospitali. Lakini haikutosha hapo afya ikazorota zaidi, ikabidi niuze na ile hiace ambayo baba aliniachia ili tumuuguze baba, mimi na dada yangu. Nikauza pia na kiwanja cha Boko kujikimu na maisha ya kilas iku na kumsaidia nyingine baba. Kwa hio mimi nikawa sina mishe tena ya kuniingizia kipato. Baba akafariki 2004, tumkarudisha Tarime kuja kumzika"

"Kwa hio nimerudi Tarime, nimeacha watoto zangu dar na yule mpenzi wa wa ahaya niliomwacha chang'ombe akabaki na chumba na vilivyomo. Ukoo ukashauri nibaki Tarime kwa kuwa ni kijana mkubwa nisaidie kuendesha familia. Ila ndio ukawa mwanzo kwa kupoteza direction zaidi. Kwa maana vipesa nilivyorudi navyo tena nikaingia katika ufuska na kibaya zaidi katika ulevi. Nikaanza ulevi mdogo mdogo huku nikishika hiki na kile ila pombe iliighalimu sio pesa tu hata mwelekeo kwa sababu kila nalichopata ni kwenye ulevi. Nikawa mlevi kupindukia hadi nikauza simu kupelekea kupoteza mawasiliano na watu wote wa dar ikiwemo mpenzi wangu. Ilifika wakati nikakosa hata nauli ya kwenda popote na hadi hali ndio imekuwa hivyo"

"Nilimuomba dada yangu awachukue na aishi na watoto wangu, hadi leo sijakutana tena hata bila mawasiliano na mpenzi wangu yule wa wahaya na kipindi naondoka Dar nilimuacha na mimba ya miezi miwili, sijui kama aliweza kujimudu kimaisha na kuzaa baadae. Nina miaka mingi sijakutana na watoto, hata mama aliewazaa sijui hata yuko wapi na anaendelea vipi"

"Niko nje ya reli kwa maana sina tena hali ya kuendelea, nimechoka kimwili, nimechoka kiakili. Mabinti niliowahi kutembea nao wakiniona wengine hunicheka, mwingine aliwahi kutema mate baada ya kuniona. Siwezi tena kaujirika kwa maana kila mtu ashajua mienendo yangu kwa hio naganga njaa na vimishe mia mbili, buku, jero, hamu inanishika navimalizia katika pombe. Jioni ikifika narudi kwa mama kulala. "

■■■MWISHO■■■
 
It's okay ulipata ukala

Daddy Naye hivyo hivyo ila aliingia kiundani zaidi.

All in all, maisha ni vita, ufe au upone.

🚶‍♂️🚶‍♂️huko hukuonana na kaka mwarabu 😎😎
 
Pole sana jamaa yetu, a real sad story..Mungu mkuu akutetee, umepitia mengi magumu
Pamoja na mambo mengi magumu, fanya ufanyalo upate mawasiliano na watoto wako na ujue mkeo ana Hali Gani Kwa sasa, maisha na ugumu wake ni mwalimu mzuri sana wa kukuposition ukae mkao Fulani ambao ni sawa kabisa.

Wale wanawake na washkaji zako wa kitambo usiwaangalie Tena Kwa sababu hawawezi kukusaidia Tena, lakini kama hautajali, utilize moyo, azimia mambo mapya, jikubali ulivyo, acha mambo mabaya yaliyokugharimu kiasi hicho, Anza maisha mapya, na kataa kivuli cha mambo ya kale kisikuendeshe, wewe ni wa leo si wa Jana...

Utashinda, wala usiogope.

Back
Top Bottom