Mliofanikiwa Kwenye Biashara : Je, Ulifanyaje Hadi Kufikia Mafanikio Uliyonayo Leo?

Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,343
3,281
Salute bosses!

Uzi huu nauandika mahususi kwaajili ya kupeana mbinu za biashara ulizotumia wakati unaanza biashara yako hadi ukafanikiwa.

Nafahamu hapa JF wapo wafanyabiashara wenye mafanikio wanaoweza kuelezea namna walivyo anzisha biashara zao hatimaye wakafanikiwa.

Je, ulifanyaje hadi ukafanikiwa?

Makosa yapi yakuepuka wakati unaanza biashara?

Wakuu naamini kupitia huu uzi wajasiriamali wadogo wanaoanza biashara watajifunza na itakuwa HESHIMA kwako kutoa ushauri wako hapa JF kwa manufaa ya wengi.

Tafadhali share story yako jinsi mambo yalivyokuwa wakati unaanza hadi sasa biashara ilipofika.

Nimefikiria nianzishe huu uzi kwasababu wajasiriamali wanaoanza hawaelewi njia sahihi zakufuata ili kusimamisha biashara zao.

Tafadhali share story yako tupate kujifunza kwa pamoja.

Shukrani
 
Thought (1)

Binafsi naendesha biashara kadhaa kwa mtindo wa partnership.

Biashara ya kwanza niliyoanzisha ni kampuni ya utalii wa ndani nikilenga zaidi kundi la vijana. Hii business ilikuwa nzuri mwanzoni kwasababu nilikuwa napata wateja wengi sana na pia nakumbuka wala sikunza na mtaji wowote.

Nilipiga hii business almost a year then nikapata chance kwenda Nairobi kushiriki Yali east, Africa (Young African Leaders Initiative). Hii program alianzisha President Obama. Hadi leo ipo inaendelea.

Hapa niseme nilifanya makosa kuacha business nakukimbilia Yali kwasababu niliporudi nilijikuta siko motivated kuanza tena so nikaipotezea nikaelekeza nguvu kwenye CBO ndogo niliyoanzisha. Hii siwezi sema ni business kwasababu ni not for profit.

Biashara ya pili ambayo nipo nayo hadi sasa ni restaurant nikiuza vyakula visivyo na asili ya nyama, pia diary. Naweza sema hii ndiyo biashara yangu ya kwanza ambayo nilianza serious. Wakati naanza sikuwa na mtaji mkubwa kwahiyo nikatafuta partner ambaye hadi leo tunapiga kazi.

Biashara ya tatu ambayo naweza sema sasa hivi ndiyo naelekeza nguvu zaidi ni Ecommerce. Naendesha online store yangu kupitia jukwa la Shopify. Naendelea kujifunza na kukabiliana na changamoto. But so far so good.

Ok, sasa napenda nitoe mambo manne (4) muhimu yakuzingatia wakati unaanza biashara yako.

1. Kuwa focused.

- mambo mengi yatatokea kuku-distract. Jitahidi ukomae na vision yako. Opportunities nyingine zinaweza tokea lakini si muhimu kama vision yako. Kwahiyo siku zote focus kwenye vision yako

2 . Tafuta Wateja Kabla Hujaanza Biashara Yako.

- ongea kwanza na potential clients. Kamwe usidhani idea yako kila mtu atai-support kwasababu "akilini mwako" unadhani ni bora au nzuri. Ongea na wateja utajifunza mambo mengi na kujua uwahudumie vipi.

3 . Tafuta mentor katika biashara husika akupe mwongozo.

- hii itasaidia kuokoa muda na fedha nyingi kwa kuepuka makosa ambayo wajasiriamali wadogo wanafanya wanapoanzisha biashara.

4 . Ni Vizuri Kuanza Kidogo.

- anza na ulichonacho. Usisubiri upate mtaji wa mamilioni ndiyo uanze. Ukianza kidogo itakupa uzoefu wakuweza kukuza mtaji na kuwa na usimamizi mzuri wa fedha.
 
Mimi naomba niandike maneno machache ila yenye maana kubwa, " mali bila daftari hupotea bila habari".
Kabisa. Bila kuweka kumbukumbu ya biashara soon utajikuta utaji umepotea na kinachofuata Biashara inakufa.

Asante kwa mtazamo mkuu jipu
 
Thought (1)

Binafsi naendesha biashara kadhaa kwa mtindo wa partnership.

Biashara ya kwanza niliyoanzisha ni kampuni ya utalii wa ndani nikilenga zaidi kundi la vijana. Hii business ilikuwa nzuri mwanzoni kwasababu nilikuwa napata wateja wengi sana na pia nakumbuka wala sikunza na mtaji wowote.

Nilipiga hii business almost a year then nikapata chance kwenda Nairobi kushiriki Yali east, Africa (Young African Leaders Initiative). Hii program alianzisha President Obama. Hadi leo ipo inaendelea.

Hapa niseme nilifanya makosa kuacha business nakukimbilia Yali kwasababu niliporudi nilijikuta siko motivated kuanza tena so nikaipotezea nikaelekeza nguvu kwenye CBO ndogo niliyoanzisha. Hii siwezi sema ni business kwasababu ni not for profit.

Biashara ya pili ambayo nipo nayo hadi sasa ni restaurant nikiuza vyakula visivyo na asili ya nyama, pia diary. Naweza sema hii ndiyo biashara yangu ya kwanza ambayo nilianza serious. Wakati naanza sikuwa na mtaji mkubwa kwahiyo nikatafuta partner ambaye hadi leo tunapiga kazi.

Biashara ya tatu ambayo naweza sema sasa hivi ndiyo naelekeza nguvu zaidi ni Ecommerce. Naendesha online store yangu kupitia jukwa la Shopify. Naendelea kujifunza na kukabiliana na changamoto. But so far so good.

Ok, sasa napenda nitoe mambo manne (4) muhimu yakuzingatia wakati unaanza biashara yako.

1. Kuwa focused.

- mambo mengi yatatokea kuku-distract. Jitahidi ukomae na vision yako. Opportunities nyingine zinaweza tokea lakini si muhimu kama vision yako. Kwahiyo siku zote focus kwenye vision yako

2 . Tafuta Wateja Kabla Hujaanza Biashara Yako.

- ongea kwanza na potential clients. Kamwe usidhani idea yako kila mtu atai-support kwasababu "akilini mwako" unadhani ni bora au nzuri. Ongea na wateja utajifunza mambo mengi na kujua uwahudumie vipi.

3 . Tafuta mentor katika biashara husika akupe mwongozo.

- hii itasaidia kuokoa muda na fedha nyingi kwa kuepuka makosa ambayo wajasiriamali wadogo wanafanya wanapoanzisha biashara.

4 . Ni Vizuri Kuanza Kidogo.

- anza na ulichonacho. Usisubiri upate mtaji wa mamilioni ndiyo uanze. Ukianza kidogo itakupa uzoefu wakuweza kukuza mtaji na kuwa na usimamizi mzuri wa fedha.
Naomba kujua zaidi kuhusu shopify Mkuu
 
Unaposema MTU kufanikiwa unamaanisha kwa level IPI??
Namaanisha unaendesha biashara yako kwa faida na pia Biashara inakuwa mwaka hadi mwaka.

Haijalishi Biashara ndogo au kubwa. Muhimu uwe unaendesha hiyo business kwa faida
 
Ahsante kwa uzi wako na experience yako pia.

Hapo kwenye kutafuta wateja kwamza, ni kwa kila biashara au zile unique and mew business ideas tu?

Mfano nataka kufungua restaurant naanzaje kutafuta wateja kwanza?
 
Mafanikio hayana formula kwamba ukifanya vile lazima iwe vile, mafanukio ni siri tena kubwa sana usitegemee kusikia kiurahisi.

kuna mengi na jitihada za ziada nje na mbali ya unayoweza kuambiwa kusudi ufanikiwe.

mafanikio ni wewe na yanatoka ndani yako kuja njee na kuonekana na watu. sijui nisemeje lakini nyuma ya mafanikio yeyote kuna siri kubwa mno ikifuatiwa na kujitoa pamoja na juhudi binafsi
 
Salute bosses!

Uzi huu nauandika mahususi kwaajili ya kupeana mbinu za biashara ulizotumia wakati unaanza biashara yako hadi ukafanikiwa.

Nafahamu hapa JF wapo wafanyabiashara wenye mafanikio wanaoweza kuelezea namna walivyo anzisha biashara zao hatimaye wakafanikiwa.

Je, ulifanyaje hadi ukafanikiwa?

Makosa yapi yakuepuka wakati unaanza biashara?

Wakuu naamini kupitia huu uzi wajasiriamali wadogo wanaoanza biashara watajifunza na itakuwa HESHIMA kwako kutoa ushauri wako hapa JF kwa manufaa ya wengi.

Tafadhali share story yako jinsi mambo yalivyokuwa wakati unaanza hadi sasa biashara ilipofika.

Nimefikiria nianzishe huu uzi kwasababu wajasiriamali wanaoanza hawaelewi njia sahihi zakufuata ili kusimamisha biashara zao.

Tafadhali share story yako tupate kujifunza kwa pamoja.

Shukrani

NAUNGA MKONO HOJA!!!!

Sijafanikiwa sana lkn hapa nilipo pana leta faraja nikifanikiwa nitaleta mrejesho hapa in fact nime wekeza sana kwenye TECH 70% na Organic veg production 30%(export)
Kila la kheri mkuu.

Siku mambo yakiwa vizuri utupe mrejesho
 
Nafatilia
Sawa mkuu amu

Ngoja tuendelee kusubiri wadau wamwage nondo kwenye business.

Mwenyewe nafuatilia kwa karibu kabisa. Naamini nitajifunza mengi kutoka kwa wafanyabiashara waliofanikiwa.
 
Back
Top Bottom