Mliofanikiwa Kwenye Biashara : Je, Ulifanyaje Hadi Kufikia Mafanikio Uliyonayo Leo?

Subscribed...

Kwa sisi ambao hatuna background ya mambo ya biashara, wala familia zetu hazijajikita kwenye biashara, its a mountain to climb.
 
Subscribed...

Kwa sisi ambao hatuna background ya mambo ya biashara, wala familia zetu hazijajikita kwenye biashara, its a mountain to climb.
Unatoka familia ya walimu?
Every thing is business in this world.
 
Thought (1)

Binafsi naendesha biashara kadhaa kwa mtindo wa partnership.

Biashara ya kwanza niliyoanzisha ni kampuni ya utalii wa ndani nikilenga zaidi kundi la vijana. Hii business ilikuwa nzuri mwanzoni kwasababu nilikuwa napata wateja wengi sana na pia nakumbuka wala sikunza na mtaji wowote.

Nilipiga hii business almost a year then nikapata chance kwenda Nairobi kushiriki Yali east, Africa (Young African Leaders Initiative). Hii program alianzisha President Obama. Hadi leo ipo inaendelea.

Hapa niseme nilifanya makosa kuacha business nakukimbilia Yali kwasababu niliporudi nilijikuta siko motivated kuanza tena so nikaipotezea nikaelekeza nguvu kwenye CBO ndogo niliyoanzisha. Hii siwezi sema ni business kwasababu ni not for profit.

Biashara ya pili ambayo nipo nayo hadi sasa ni restaurant nikiuza vyakula visivyo na asili ya nyama, pia diary. Naweza sema hii ndiyo biashara yangu ya kwanza ambayo nilianza serious. Wakati naanza sikuwa na mtaji mkubwa kwahiyo nikatafuta partner ambaye hadi leo tunapiga kazi.

Biashara ya tatu ambayo naweza sema sasa hivi ndiyo naelekeza nguvu zaidi ni Ecommerce. Naendesha online store yangu kupitia jukwa la Shopify. Naendelea kujifunza na kukabiliana na changamoto. But so far so good.

Ok, sasa napenda nitoe mambo manne (4) muhimu yakuzingatia wakati unaanza biashara yako.

1. Kuwa focused.

- mambo mengi yatatokea kuku-distract. Jitahidi ukomae na vision yako. Opportunities nyingine zinaweza tokea lakini si muhimu kama vision yako. Kwahiyo siku zote focus kwenye vision yako

2 . Tafuta Wateja Kabla Hujaanza Biashara Yako.

- ongea kwanza na potential clients. Kamwe usidhani idea yako kila mtu atai-support kwasababu "akilini mwako" unadhani ni bora au nzuri. Ongea na wateja utajifunza mambo mengi na kujua uwahudumie vipi.

3 . Tafuta mentor katika biashara husika akupe mwongozo.

- hii itasaidia kuokoa muda na fedha nyingi kwa kuepuka makosa ambayo wajasiriamali wadogo wanafanya wanapoanzisha biashara.

4 . Ni Vizuri Kuanza Kidogo.

- anza na ulichonacho. Usisubiri upate mtaji wa mamilioni ndiyo uanze. Ukianza kidogo itakupa uzoefu wakuweza kukuza mtaji na kuwa na usimamizi mzuri wa fedha.
Ahsante
 
Sijafanikiwa sana lkn hapa nilipo pana leta faraja nikifanikiwa nitaleta mrejesho hapa in fact nime wekeza sana kwenye TECH(software, hardware & internet) 70% na Organic veg production 30%(export)

samahani naweza pata mawili matatu juu ya export ya organic veg..??
 
Back
Top Bottom