Alphaking2023
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 2,092
- 2,122
Muda mwingi huwa nawaza mafanikio naweka plan zangu tayari kwa kuzifanyia kazi lakini tatizo linakuwa katika utekelezaji nitafanya siku ya 1 na 2 baada ya hapo sifanyi tena , Nina vitabu vingi sana softcopy vinavyoelezea mafanikio na jinsi watu wanavyofanikiwa lakini nikipanga mda wa kusoma naweza kusoma siku 2 tu nashindwa kabisa kuji control katika malengo yangu tangu nipo o-level huwa napanga siku flani naanza kusoma rasmi lakini inakuwa tofauti na mipango yangu hali imeendelea hadi saizi university huwa napanga semester flani nisome kweli lakini haiwi kama navyopanga.. Naomba watu ambao wana uzoefu kidogo katika suala hili wanisaidie ni mbinu gani nitumie niweze kufanya kile ninachokusudia kufanya?