Mlioacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe nahitaji msaada wenu

Karibu sana mdau labda nikutie Moyo tu kwa uamuzi wako na nikupe mfano wa kosa linalofanywa na wengi walio ajiriwa. Kuna watu kama wewe huanzisha miradi hii na kuajiri watu waisimamie, unakuta anayesimamia haifanyi kazi ipsavyo ila atakuibia kidogo kidogo na akiondoka anaanzisha biashara kama hiyo bila wewe kufahamu alikuwa anakuibia kiasi cha kupata mtaji.

Tunaona vijana wengi wanavyo ajiriwa kwenye maduka hasa ya rejareja na kuacha kazi baadae na kufungua maduka binafsi wakati mshahara wake ulikuwa elfu hamsini au laki. Sasa aliyemuajiri angeacha hiyo kazi anayofanya na akasimamia mradi mwenyewe si mradi ungemtoa?

Kikubwa kuwa jasiri na ujue kujifariji maana kuna nyakati mambo yanaweza kuwa hovyo ukawaza kurudi kuajiriwa. Self motivation is key to succeed in this. Kila la heri.
Big point. Sanasa ili kuacha kazi na kujiajiri unapaswa kuwa sawa kiakili (ready mind set), Na kama unaona ni ngumu kwenye mind set yako ni vyema kuwa unasikiliza motivation mbalimbali kutoka youtube na sehemu nyingine, hii itakusaidia. Maana kuacha kazi, tena unakuta umeizoea ni ngumu sana.
 
Usiache wewe tafuta mfanya kazi akusaidiage tuu
Mfanyakazi yupi, halfu mnawachukulia wafanyakazi ni watu wanaofanya kitu kw kukurupuka hawafanyi utafiti, au haijawakuta ndo maana, watu wanafungua biashara za milioni 8 mpk 10 lkn hao wanaowaweka ndo wanaowafirisi. Biashara inapoanza inakuw na changamoto lkn changamoto hizo uzipate ww ili uwe na uchungu na biashara zko
 
Ukweli ni kwamba kuajiriwa ni utumwa na kunakuzeesha mapema sana mana maisha yako yote utaishi under stress mana kazi nyingi tunazofanya hazina ujira hata wa kutosha mahitaji ya kila siku nyumban kinachotufanya watu wengi wakae kwenye ajira ni woga wa kujitegemea ila ukweli kama vijana tujiajiri hata kwa kuuza mayai ila yawe yako

Utakuta mtu umeajiriwa kufanya sales ya products za mtu sasa km unaweza kuuza bizaa za mtu kwanni usitafute bizaa yako uiuze na ukapata faida au hasara ya kwako
Mfano utakuta mjini wale vijana wanatembea na mabeseni au dawa za meno wanauza sio zao ila wanawauzoa watu sasa kwann usinunue mabeseni hata mawili ukauze ila yawe yako
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Tapeli mkubwa wewe, lima na uuze mwenyewe.
 
Habari wanajamvi, mimi ni muajiriwa katika shirika moja lisilo la kiserikali na kazi ninayojishughulisha nayo nje ya ajira yangu ni kilimo. Pia nina malengo ya kufuga kuku wa aina zote yaani chotara, mayai na wanyama na malengo yangu ni kuacha kazi na kusimamia shughuli zangu za kilimo na ufugaji.

Sasa wadau ambao mliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe mlipitia changamoto gani pindi Mlipoacha kazi.
Mkuu habari za siku, nimatumaini yangu kuwa baada ya kupata ushauri mbalimbali kutoka kwa wanaJF kuna maamuzi uliyafanya na tayari utakuwa na jambo live la kufundisha wengine. Kwa ufupi nilitaka nipate feedback ya maamuzi yako na maendeleo yako kwa sasa.
 
Habari wanajamvi, mimi ni muajiriwa katika shirika moja lisilo la kiserikali na kazi ninayojishughulisha nayo nje ya ajira yangu ni kilimo. Pia nina malengo ya kufuga kuku wa aina zote yaani chotara, mayai na wanyama na malengo yangu ni kuacha kazi na kusimamia shughuli zangu za kilimo na ufugaji.

Sasa wadau ambao mliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe mlipitia changamoto gani pindi Mlipoacha kazi.
JIAJIRI NGO NYINGI SIO PERMANENT , ANGALIA KIPATO KIKUBWA KINA KUJA WAPI NI KILIMO , BE BUSINESS MAN NOT EMPLOYED BOY
 
Hivi ndg yangu trillion 8 unaijua lkn?

hio trillion 8 unayoisema ni umejumlisha utajiri wa (Bakhressa+Mengi+Rostam+Dewji) na bado combined hawajafikia hio trillion 8.Atakua ni tajiri gani hapa bongo mwenye pesa hio?Kudanganyana sio kuzuri aisee.

Hoja kama hio yako ndiyo inafanya ule msemo wa za kuambiwa changanya na zako aisee.
Huyu Jamaa anaweza kuwa Jah People
 
Kwa kifupi.
Wakati tunamaliza darasa la saba miaka hiyoo,
Kuna rafiki yangu anaitwa Chaula,akatuuliza swali,hivi mnaenda sekondari kufanya nini?
Yeye alikuwa na maono yake,kwamba masomo ya darasa la saba yanamtosha kutatua changamoto zilizo mzunguka.
Namnukuu,ujanja ni kufahamu kujumlisha,kutoa,kugawanya na kuzidisha,pia na lugha kama kiigereza na nyinginezo muhimu.
Tulipo maliza sekondari Chaula akawa ana meza sokoni,duka moja la rejareja na moja la jumla.
Tulipo maliza six yeye akawa anamiliki mashine ya kusaga nafaka,na malori mawili.
Tulipo maliza chuo,akawa tayari ana mabasi ya kwenda Dar es salaam.
Tulipo anza kutafuta kazi akatushauri tujiajiri,wakati huo tayari anamiliki hoteli kadhaa.
tulipo kuwa tunastaafu kazi,anatukaribisha kwenye shughuli zake kwa mkataba maalum,ili aone kama elimu tuliyopata inaweza kumsaidia.
KWA USHAURI>
Bora ujiajiri mapema ,kuajiriwa ni utumwa.
Motivation speaker
 
Back
Top Bottom