Mlioacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe nahitaji msaada wenu

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,019
1,671
Habari wanajamvi, mimi ni muajiriwa katika shirika moja lisilo la kiserikali na kazi ninayojishughulisha nayo nje ya ajira yangu ni kilimo. Pia nina malengo ya kufuga kuku wa aina zote yaani chotara, mayai na wanyama na malengo yangu ni kuacha kazi na kusimamia shughuli zangu za kilimo na ufugaji.

Sasa wadau ambao mliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe mlipitia changamoto gani pindi Mlipoacha kazi.
 
Habar wanajamvi mimi ni Muajiriwa katika shirika Moja lisilo la kiserikali na kazi ninayo jishuhulisha nayo nje ya ajira yangu ni kilimo na pia nina malengo ya kufuga kuku wa aina zote yaani chotara, wa mayai na wanyama na malengo yangu ni kuacha kazi na kusimamia shuhuli zangu za kilimo na ufugaji. Sasa wadau ambao mliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe mlipitia changamoto gani pindi Mlipoacha kazi.
Karibu sana mdau labda nikutie Moyo tu kwa uamuzi wako na nikupe mfano wa kosa linalofanywa na wengi walio ajiriwa. Kuna watu kama wewe huanzisha miradi hii na kuajiri watu waisimamie, unakuta anayesimamia haifanyi kazi ipsavyo ila atakuibia kidogo kidogo na akiondoka anaanzisha biashara kama hiyo bila wewe kufahamu alikuwa anakuibia kiasi cha kupata mtaji.

Tunaona vijana wengi wanavyo ajiriwa kwenye maduka hasa ya rejareja na kuacha kazi baadae na kufungua maduka binafsi wakati mshahara wake ulikuwa elfu hamsini au laki. Sasa aliyemuajiri angeacha hiyo kazi anayofanya na akasimamia mradi mwenyewe si mradi ungemtoa?

Kikubwa kuwa jasiri na ujue kujifariji maana kuna nyakati mambo yanaweza kuwa hovyo ukawaza kurudi kuajiriwa. Self motivation is key to succeed in this. Kila la heri.
 
Kama unataka kujiajiri,ni vizuri ukafanya research ya kutosha kabisa kwenye hiyo sector unayotaka kuingia.
 
Kaka kwanza Hongera kwa kuanza Kuwa na wazo hilo
Kujiajiri kuna changamoto nyingi sana, ukilala biashara pia imelala .pili vitu huwa haviendi kama unavyotaka wewe inakubidi uwe na subira, jipe muda ukishaingia kwenye shughuli zako mwenyewe.

Mfano mimi binafsi nina miaka Miwili now toka nivunje daraja, kuanza Kujiajiri na nimejipa kipindi cha miaka mitano hadi saba ya shida na njaa it means kipindi cha kujenga brand yangu na sasa nimeajiri vijana zaidi ya kumi. Na nilifanya kazi kwenye ngo. Usiogope Kujiajiri.

Kila sehemu changamoto zipo, naamini hata hapo ulipo changamoto zipo. Like kupelekwa kwenye hearing na vitu kama hivyo. Fanya uamuzi sahihi now na amini ukijiajiri elimu yako Ndio utaitumia vizuri.
 
Kaka kwanza Hongera kwa kuanza Kuwa na wazo hilo
Kujiajiri kuna changamoto nyingi sana, ukilala biashara pia imelala .pili vitu huwa haviendi kama unavyotaka wewe inakubidi uwe na subira, jipe muda ukishaingia kwenye shughuli zako mwenyewe. Mfano mimi binafsi nina miaka Miwili now toka nivunje daraja, kuanza Kujiajiri na nimejipa kipindi cha miaka mitano hadi saba ya shida na njaa it means kipindi cha kujenga brand yangu na sasa nimeajiri vijana zaidi ya kumi. Na nilifanya kazi kwenye ngo. Usiogope Kujiajiri. Lila sehemu changamoto zipo naamini hata hapo ulipo changamoto zipo. Like kupelekwa kwenye hearing na vitu kana hivyo. Fanya uamuzi sahihi now na amini ukijiajiri elimu yako Ndio utaitumia vizur
Thanks Mkuu
 
Jiajiri tu,huna haja ya kuhofia kitu. kila kitu kinaenda kwa mipango ya mungu na jitihada ndo kila kitu. kapambane mkuu
 
Asanten kwa ushauri ila kwenye kilimo nishaona mafanikio yake ila changamoto ni muda kwani kuna kipindi natakiwa kusafiri kwenda kuangalia miradi yangu ya kilimo na huku kazini nahitajika hivyo nashindwa kujigawa hivyo inabidi nimtume mtu sasa hapo ndio garama inavyoongezeka kwani lazima kijana umgaramie kila kitu kisha umpe na posho
 
Acha kumtia ujinga mwenzako,hofu na uoga wako wa maisha usimuambukize mwenzio.

ABUBAKAR SHEKAU songa mbele baba maamuzi yako ni sahihi 100%.Achana na utumwa.
Kwa atakayepitia hapa nafikiri mjinga atamuona ni nani kulingana na comment zetu,sina hofu wala uoga kimaisha naishi maisha ya kawaida kabisa amabayo nasema Mwenyezi Mungu asante (Hivi wakati mwingine mnaposhindwa kukoment kistaarabu mnapungukiwa nini?

Hili ni jukwaa tu sio hukukumu wala hatuwezi kumlazimisha aliyeoomba ushauri aamue kama sie tunavyotaka ),safari ya biashara ina kitu inaitwa break even period,ni kipindi ambacho biashara lazima ikutegemee kabla hujaitegemea,ok...sawa nakubaliana na wewe kazi aache kabla hajaanza kuisoma " return" ya biashara atakuwa na mkondo gani wa kuimarisha biashara hiyo?,

kumbuka maisha ya kila siku yanahitaji pesa itoke ndani "and at the same time" hujaisoma poa return ya biashara, akikurupuka kuacha kazi atakumbuka.Kaka hata sisi pia ni waajiriwa lakini "at the same time" tunaujasilia mali na maisha yanasonga.

Narudia tena kazi asiaache mpake aweze kusoma return ya biashara imekaaje,kwani kazi ni jela hawezi kuwa muuajiriwa na mwisho awa siku mambo yakisimama wima kazi unaacha ?maisha ya biashara sio 1+1=2.
 
Back
Top Bottom