Mlioacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe nahitaji msaada wenu

Habari wanajamvi, mimi ni muajiriwa katika shirika Moja lisilo la kiserikali na kazi ninayo jishuhulisha nayo nje ya ajira yangu ni kilimo. Pia nina malengo ya kufuga kuku wa aina zote yaani chotara, wa mayai na wanyama na malengo yangu ni kuacha kazi na kusimamia shuhuli zangu za kilimo na ufugaji.

Sasa wadau ambao mliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe mlipitia changamoto gani pindi Mlipoacha kazi.
Wazo langu kwenye hili.
1. Changamoto ya kwanza ni steady paycheck ndio itakuwa mwisho wake, ukishavuka daraja na kufika ng'ambo ya pili ukajiajiri sio kweli na hawezi ikatokea kwamba kila mwezi utapata kipato kile kile kwahiyo itakubidi uweze kufanya adjustment ya budget yako (kama uko mwenyewe "single") kama unafamilia basi hakikisha unamuandaa mwenza wako kisaikolojia na pia kama unawatoto hakikisha unatenga pesa kwa ajili ya matumizi yao ya msingi na lazima kama ada na mengineyo unayo ona ni ya msingi kabisa!

2. Jiandae kisaikolojia, mambo katika ajira sio magumu kama kujiajiri, ukisha jiari mipango yako hubadilishwa na soko lako, wateja wako, washindani wako, na mara nyingine kuanguka kwa yale unayo wekeza pesa na muda wako huko, kwahiyo kabla hujaacha kazi jiambie kwamba changamoto zitakuja, na jiulize kama utaweza kuzimudu.

3. Ukishajiajiri elewa unaongeza watu wanao kutegemea, utakuwa na wafanyakazi watahitaji mishahara kunakipindi kitafika utalipa mishahara na kukosa cha kujilipa, kwahiyo kabla hujaingia kujiajiri kama unachotaka kufanya kitakuhitaji ulipe watu hakikisha unapesa zao on time ndugu, kama ulishapatwa na kasumba ya mshahara wako kucheleweshwa ukaghadhabika jua hili likitokea kwa wakafanyakazi wako watapitia hali uliyo wahi kupitia.

Ila all in all nakutakia kila la kheri, ukiona uko teyari na utamudu maisha kama mjasiriamali jump on, ila hakikisha unakuwa teyari na kuwa teyari sio kipesa tuu zipo factor nyingi za kuangalia na ningekushauri utafute wajasiriamali wa mambo unayotaka kufanya uongee nao ana kwa ana wakupe mchanganuo mzima wa biashara na jinsi biashara hizo zinavyo endesha maisha yako alafu ujipime kama na wewe utaweza kwenda na speed hiyo au laah!
 
Kujiajiri ni kuzuri sana kwa kwel,ila mwanzo unakuwaga mgumu kama alivyosema mdau fulan hapo juu kwamba unaweza kuwaza kurud tena kuajiriwa,lkn baadae mambo yakishakaa sawa unakula bata 2 na mambo yanaenda sawa mpaka utasema nilikuwa wap ck zote,...kuajiriwa huwez kuwa tajiri...ila ukijiajir una nafasi kubwa ukafanikiwa na kuwa tajir kama sio tajir basi hela haitakupiga chenga kuliko kungoje mshahara wa mwezi..ni hayoo..povu ruksa maana wengne humu wamerukwa na akili wakat haya ni mawazo yangu mm
 
Kaka kwanza Hongera kwa kuanza Kuwa na wazo hilo
Kujiajiri kuna changamoto nyingi sana, ukilala biashara pia imelala .pili vitu huwa haviendi kama unavyotaka wewe inakubidi uwe na subira, jipe muda ukishaingia kwenye shughuli zako mwenyewe. Mfano mimi binafsi nina miaka Miwili now toka nivunje daraja, kuanza Kujiajiri na nimejipa kipindi cha miaka mitano hadi saba ya shida na njaa it means kipindi cha kujenga brand yangu na sasa nimeajiri vijana zaidi ya kumi. Na nilifanya kazi kwenye ngo. Usiogope Kujiajiri. Lila sehemu changamoto zipo naamini hata hapo ulipo changamoto zipo. Like kupelekwa kwenye hearing na vitu kana hivyo. Fanya uamuzi sahihi now na amini ukijiajiri elimu yako Ndio utaitumia vizur
Bro thanks i need this motivation
 
mkuu, nakuomba take from me, kujiajiri mwenyewe kunalipa balaa fanya maamuzi na usiangalie nyuma, unatakiwa kuwa na sifa chache tu muhimu. yaani moyo wa simba, speed ya swala na kulijua soko lako. i mean be a visionary, be patient, know your customer, know your product and know the Industry.
niliajiriwa kwa miaka 4 nikaona sitoki na mshahara wa laki 5 unusu. niliacha kazi nikasema am not going to try but am going to do business.
nilipata shida mwaka wa kwanza sasa nina miaka 6 uraiani, kwa mwaka jana nilifika turnover ya robo Bilion, kwa mwaka huu biashara ni mbaya sana lkn inshaalah naweza kufika 100 milion.
lakini unafanya kazi km punda, unatumia 95%ya ubongo kufikiri vyema kwani ukilegea unapika hasara. kuna jamaa ni mteja wangu yeye kwa mwaka jana alipiga turnover ya Trilion kadhaa, yeye ana investmemet inayoweza kufika 8 trilion. ni km hadithi lkn ni kweli. kwa uwezo wa M.Mungu nakusudia kufungua kiwanda july 2019. lkn sijui km ningewaza haya km ningekuwa nimeajiriwa. kuna phalsapha moja huwa naitumia sana, kuwa watu waliosoma hawabebi Risk, sisi tusiosoma tunabeba sana risk. ndo maana richest people duniani wengi wana PhD za Heshim, ni ngumu kumkuta Professor Bilionea. karibu ndugu ya kushare ni mengi sana.
 
Ndugu unachanganya trioni,billioni na millioni?
 
Kwa atakayepitia hapa nafikiri mjinga atamuona ni nani kulingana na comment zetu,sina hofu wala uoga kimaisha naishi maisha ya kawaida kabisa amabayo nasema Mwenyezi Mungu asante (Hivi wakati mwingine mnaposhindwa kukoment kistaarabu mnapungukiwa nini? Hili ni jukwaa tu sio hukukumu wala hatuwezi kumlazimisha aliyeoomba ushauri aamue kama sie tunavyotaka ),safari ya biashara ina kitu inaitwa break even period,ni kipindi ambacho biashara lazima ikutegemee kabla hujaitegemea,ok...sawa nakubaliana na wewe kazi aache kabla hajaanza kuisoma " return" ya biashara atakuwa na mkondo gani wa kuimarisha biashara hiyo?,kumbuka maisha ya kila siku yanahitaji pesa itoke ndani "and at the same time" hujaisoma poa return ya biashara, akikurupuka kuacha kazi atakumbuka.Kaka hata sisi pia ni waajiriwa lakini "at the same time" tunaujasilia mali na maisha yanasonga.
Narudia tena kazi asiaache mpake aweze kusoma return ya biashara imekaaje,kwani kazi ni jela hawezi kuwa muuajiriwa na mwisho awa siku mambo yakisimama wima kazi unaacha ?maisha ya biashara sio 1+1=2.
Look! Kama unataka kujiajiri wakati umeajiriwa usitegemee mambo yakunyookee ndo uacha kazi! Ni ngumu! Cha muhimu huwe na plan utafanya nini cha kukuingizia kipato au hata kama plan huna lakini kitendo cha kuchukia ajira baada ya kujitafakari na kuona usogei ni mtaji tosha wa ujasiri utakaokupa nguvu ya kupata maono ya kujiajiri. Just quit what next will emerge because employment is a jail
 
nimetizama kwa makini sijaona sehem nilipochanganya je? unaweza kunisaidia ni sehem gani? nami ni binadam
 
mkuu, nakuomba take from me, kujiajiri mwenyewe kunalipa balaa fanya maamuzi na usiangalie nyuma, unatakiwa kuwa na sifa chache tu muhimu. yaani moyo wa simba, speed ya swala na kulijua soko lako. i mean be a visionary, be patient, know your customer, know your product and know the Industry.
niliajiriwa kwa miaka 4 nikaona sitoki na mshahara wa laki 5 unusu. niliacha kazi nikasema am not going to try but am going to do business.
nilipata shida mwaka wa kwanza sasa nina miaka 6 uraiani, kwa mwaka jana nilifika turnover ya robo Bilion, kwa mwaka huu biashara ni mbaya sana lkn inshaalah naweza kufika 100 milion.
lakini unafanya kazi km punda, unatumia 95%ya ubongo kufikiri vyema kwani ukilegea unapika hasara. kuna jamaa ni mteja wangu yeye kwa mwaka jana alipiga turnover ya Trilion kadhaa, yeye ana investmemet inayoweza kufika 8 trilion. ni km hadithi lkn ni kweli. kwa uwezo wa M.Mungu nakusudia kufungua kiwanda july 2019. lkn sijui km ningewaza haya km ningekuwa nimeajiriwa. kuna phalsapha moja huwa naitumia sana, kuwa watu waliosoma hawabebi Risk, sisi tusiosoma tunabeba sana risk. ndo maana richest people duniani wengi wana PhD za Heshim, ni ngumu kumkuta Professor Bilionea. karibu ndugu ya kushare ni mengi sana.
Ni biashara gan unafanya mkuu?
 
Look! Kama unataka kujiajiri wakati umeajiriwa usitegemee mambo yakunyookee ndo uacha kazi! Ni ngumu! Cha muhimu huwe na plan utafanya nini cha kukuingizia kipato au hata kama plan huna lakini kitendo cha kuchukia ajira baada ya kujitafakari na kuona usogei ni mtaji tosha wa ujasiri utakaokupa nguvu ya kupata maono ya kujiajiri. Just quit what next will emerge because employment is a jail
mkuu hii kitu ya kitambo saaaanaaaaaaaaa
 
Huu uzi ulianzishwa march 2017...naomba mrejesho kwa aliyeanzisha na amefikia wapi....

pia naomba mrejesho kutoka kwa wale wote waliofurahia shauri zilizotolewa na wadau mbalimbali na kutoa ahadi kuwa ushauri umewajenga na kuwatia moyo kuacha ajira zao na kujiingiza mtaani kwa kishindo.

LETENI MREJESHO TAFADHALI...
 
mkuu, nakuomba take from me, kujiajiri mwenyewe kunalipa balaa fanya maamuzi na usiangalie nyuma, unatakiwa kuwa na sifa chache tu muhimu. yaani moyo wa simba, speed ya swala na kulijua soko lako. i mean be a visionary, be patient, know your customer, know your product and know the Industry.
niliajiriwa kwa miaka 4 nikaona sitoki na mshahara wa laki 5 unusu. niliacha kazi nikasema am not going to try but am going to do business.
nilipata shida mwaka wa kwanza sasa nina miaka 6 uraiani, kwa mwaka jana nilifika turnover ya robo Bilion, kwa mwaka huu biashara ni mbaya sana lkn inshaalah naweza kufika 100 milion.
lakini unafanya kazi km punda, unatumia 95%ya ubongo kufikiri vyema kwani ukilegea unapika hasara. kuna jamaa ni mteja wangu yeye kwa mwaka jana alipiga turnover ya Trilion kadhaa, yeye ana investmemet inayoweza kufika 8 trilion. ni km hadithi lkn ni kweli. kwa uwezo wa M.Mungu nakusudia kufungua kiwanda july 2019. lkn sijui km ningewaza haya km ningekuwa nimeajiriwa. kuna phalsapha moja huwa naitumia sana, kuwa watu waliosoma hawabebi Risk, sisi tusiosoma tunabeba sana risk. ndo maana richest people duniani wengi wana PhD za Heshim, ni ngumu kumkuta Professor Bilionea. karibu ndugu ya kushare ni mengi sana.

Am not going to try but am going to do business.
 
Huu uzi ulianzishwa march 2017...naomba mrejesho kwa aliyeanzisha na amefikia wapi....

pia naomba mrejesho kutoka kwa wale wote waliofurahia shauri zilizotolewa na wadau mbalimbali na kutoa ahadi kuwa ushauri umewajenga na kuwatia moyo kuacha ajira zao na kujiingiza mtaani kwa kishindo.

LETENI MREJESHO TAFADHALI...
Mimi ndio nilianzisha huu uzi na nilikuwa na malengo ya kuacha kazi kweli ila nilipokea maoni ya wadau na wengine kuni pm na tukawasiliana wengi walinishauri nisiache kazi nijaribu kujigawa sehemu zote mbili mpaka nihakikishe mambo yangu yanaenda vizuri. Nilijikita kwenye kilimo na ufugaji nafuga kuku wa kienyeji aina ya kuroiler na pia nalima mahindi pamoja na machungwa. Nilianza kununua kuku 150 baada ya miezi sita nikawauza wote ingawa changamoto zilikuwepo ila nilipata faida ya kama laki Tisa kwa sasa ninao kuku 250 nategemea kuuza kipindi cha sikukuu ya idd. Kwa upande wa kilimo nimelima ekari nne za mahindi na yanaendelea vizuri. Na pia nina kilimo cha machungwa ambacho nilikianza muda na kwa mwaka huu nikiuza machungwa sitakosa zaidi ya Tsh milioni moja. Na pia kuna post nimeitoa kwamba mwaka huu nina mpango wa kuongeza ekari tano nipande mahindi,machungwa na mikorosho pamoja na kupanua shughuli zangu za ufugaji.

Ningeweza ningeunganisha hiyo post ila labda mods wangenisaidia kuiunganisha au nijaribu kukopi

Ila mwakani ndio nitachukua maamuzi Magumu ya kuacha kazi. Ila Ahsanteni kwa ushauri
 
Back
Top Bottom