Mlio omba mkopo heslb angalieni hapa mjifunze mapemaaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlio omba mkopo heslb angalieni hapa mjifunze mapemaaa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MKINDE, Sep 1, 2012.

 1. M

  MKINDE Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  MADHARA YA KUPAPATIKIA BUMU HAYA HAPA HADHARANI
  Naitwa XXX mimi ni mwanafunzi niliyemaliza Bwiru secondary. Ninaishi njombe, nilitamani sana kusoma chuo kikuu chochote hapa Tanzania na wakati wote huwa namwomba Mungu anisaidie nipate chuo ambacho ningeweza kupata mkopo kwakuwa familia yangu haikuwa na uwezo. Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Jumatano ndipo matokeo ya kidato cha sita yalipo tangazwa, nilikimbilia internet café nikiwa na shauku kubwa yakujua matokeo yangu. Nilifurahi sana tena sana yaani siwezi kuelezea kiwango cha furaha nilichokuwa nacho siku hiyo nilipoangalia jina langu na kuona nimepata division one ya point 10. Furaha ilitawala zaidi nilipofika nyumbani na kuwapa taarifa ya matokeo yangu………………SIKU ZILISONGA BAADAYE NILIOMBA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NA NIKACHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO HIKO BAADA YA HAPO NILIJUTA………endelea
  Nakumbuka siku natoka nyumbani baada ya nasaha za wazazi na marafiki baba alinipatia shilingi elfu hamsini ikiwa ni pamoja na nauli yangu. Nilipofika jijini Dar es salaam nilifikia kwa rafiki yangu aliyekuwa akisoma mwaka wa pili DIT(Dar es salaam Institute of Technology), kwa kweli ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika katika hili jiji, baada ya siku tatu nilienda kuripoti chuo na nikapatiwa fomu za usajili…..SASA NAANZA KULIJUA JIJI…..nilipozunguka kwenye jengo moja hapa chuoni nilikuta jina langu limebandikwa ubao wa matangazo nilikuwa nimepangiwa kuishi hostel za mabibo, nilienda mpaka kwenye hostel nilikopangiwa………..NAENDELEA KUSONGA MBELE….Sasa mimi ni mwanachuo nahii naithibitisha baada ya kupata kitambulisho cha chuo, baada kama siku mbili hivi ndipo nilipopata taarifa ya kwamba tunahitajika tukasaini majina yetu ilitupewe mkopo(bumu), nilifanya hivyo na kwa mara ya kwanza nilipewa shilingi 500,000/= cash mkononi, aisee akili ziliniruka ghafla nikawa kama nimechanganyikiwa, nilimkumbuka mama nyumbani kisha baba baadae marafiki, aisee nilijiona nami ni kati ya wale matajiri wanao julikana hapa Tanzania…Kitu cha kwanza nilichokumbuka ni kumtumia mama shilingi laki moja kisha baba nikamtumia shilingi elfu hamsini baada ya hapo nikabakiwa na shilingi 350,000/= nikawa napiga hesabu niifanyie biashara gani hii hela iliniweze kupata zaidi……..Nilienda kwanza hostel kupumzisha akili baadaye wazo la kununua redio kubwa aina ya SUB HOOFER likanijia nilimwomba rafiki yangu anipeleke wanapouza subhoofer, nilipelekwa sehemu moja inaitwa Mlimani city nikanunua subhoofer shilingi laki moja na nusu, baada ya kurudi hostel nilikuwa nimebakiwa na kama shilingi laki moja na arobani elfu akili yangu bado haikuwa imetulia nilitamani ni stop kwanza chuo ili nimalizie hizi pesa, baada ya wiki kadhaa kupita tulitangaziwa test namba moja nakumbuka nilipata 2/10, hapa sasa nikastuka kidogo japo haikunitisha sana, kufikia mwezi wa kumi na moja mwishoni tukaambiwa tufungue akaunti ili mkopo wa pili uweze kuwekwa kwenye akaunti zetu, mama yangu uwiiii! hapa sasa ndio nikawa mwendawazimu……..ENDELEA…. Nakumbuka mkopo wa pili niliwekewa kwenye akaunti yangu shilingi laki tatu kama na arobaini hivi sikumbuki vizuri ila kusema kweli walinichanganya sana na hizi hela zao ikapelekea hata baadhi ya lecture siendi….Mitihani ya semester ya kwanza ilitangazwa na nakumbuka nilipata suplimentary tatu za core courses


  Hapa sasa akili ikaanza kufanya kazi baada ya kuambiwa na wenzangu kwamba iwapo sitoweza kuzifaulu course hizo nitafukuzwa chuo na mbaya zaidi sitopewa tena mkopo. Nilianza kukesha kama bundi na huwezi amini semester ya pili nilifaulu vizuri sana ila niliandikiwa nimediscontinue due to min GPA point.. Aisee niliumia sana yaani sana nilipowauliza wenzangu nini kinachofuata waliniambia niende nikaongee na mwalimu wa kila somo nililofeli kama anaweza kunisaidia, nilifanya hivyo ila ilishindikana nikapewa ushauri kama nitakuwa na hela kidogo kama laki moja nimpe mwanafunzi mwenzangu ampelekee mwalimu wa somo ili aweze kunisaidia, niliuza subhoofer yangu shilingi elfu tisini na tano nikaongezea na hela yangu kisha nikampa mwanafunzi mwenzangu akampelekea mwalimu , mwalimu alikula hela yangu kisha akaniambia niwe mvumilivu atarekebisha kwenye profile ya matokeo yangu……ENDELEA…. Siku moja ikanibidi niende ofisini kwa mwalimu ambaye alipewa hela yangu baada ya kuona hakuna jipya kwenye profile yangu ndipo nilipokutana na maneno hayaaa: SIKILIZA KIJANA MIMI SIKUTAMBUI KWA KIPINDI HIKI, MATOKEO NIMESHATOA KAMA HUJARIDHIKA NENDA KA-APPEAL ALAFU WARUDIE KUSAHIHISHA MTIHANI WAKO: mwalimu aliongea kwa ukali huku akiniangalia usoni bila hata ya huruma… daaaaa! Nilichoka ile mbaya, sasa niliona dhahiri ya kwamba mimi sio tena mwanachuo baada ya majina bumu la tatu yalipotoka nilipoingiza kadi yangu ya ATM ilimezwa kwa sababu nilisahau password nilipoingia ndani niliambiwa akaunti yangu haina fedha ya kutosha kuweza kupewa salio, nikawaambia naombeni basi hata hiyo kadi yangu walinipa kadi yangu nikaondoka. MIMI MWENZENU SILIPENDI BUMU NI TOFAUTI NA WANAFUNZI WENGINE NAJUUUUTA KUPATA BUMU.
  USHAURI
  Jamani kama hujui matumizi ya hela ya mkopo unayopewa pliiiiizi nenda kwa dean of student omba ushauri. CHUO SINA TENA NILIRUDI ZANGU HOME NIKISUBIRI MWAKA MWINGINE NIFANYE APPLICATION UPYA.
  ***************ASANTENI KWA KUNISIKILIZA**********
  ..SIJUI KAMA KUNA KITU UMEJIFUNZA KUTOKA KWANGU KAMA BADO UTAJIFUNZA UKIPATA BUMU…
   
 2. m

  milinga godfrey Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thanx 4 ur ushauri ndugu
   
 3. JOH MCHESHI

  JOH MCHESHI Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ya ukweli kinoma alikuwa na wenge toka mwanzo pointi 10 anadai ni one akati ni two.
   
 4. Vodka

  Vodka JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 909
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Asante kwa hadithi yako,ujumbe umefika.
   
 5. sop sop

  sop sop JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 650
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  daaah ama kwel boom ni sumu,tumekuelewa vizur sana mkuu!!
   
 6. f

  fidelis zul zorander JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 679
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kweli mjini shule...!
   
 7. QUALIFIED

  QUALIFIED JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2012
  Messages: 747
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  unahonga wazazi ela ya kukulisha skul umetisha mkuu
   
 8. ze duduz

  ze duduz JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 864
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  hahahahah kaka ulikuwa mshamba balaaa nadhani ilikuwa mara yako ya kwanza kushka kilo5
   
 9. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Xaxa hiv upo wap jomba?
   
 10. m

  matcho New Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ili tupate mmea mbegu lazima ife asahnte kwakua mbegu kaka!
   
 11. temboemll

  temboemll Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli Kufanya kosa ndio kujifunza na kujaribu kipya
   
 12. M

  MKINDE Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nipo sua mwaka wa pili naingia wa tatu mkuu
   
 13. M

  MKINDE Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tumia vizuri sasa huo mmea usije nawe ukaoza
   
 14. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Njoo kwa akina dada sasa ni balaa, wachokoraa wa dampo wanajichukulia madada poa tu pale Mabibo.
   
 15. Upcoming

  Upcoming Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Afu sijui alisoma mwaka gani cauz point 10 anaita div 1 afu boom la kwanza 4 recent yrs linakuwaga 600,000 na .....
   
 16. M

  MKINDE Member

  #16
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mi nadhani kaujumbe kamefika ambaye atataka kubisha na kukosoa baadhi ya makosa mimi najiweka pembeni....
   
 17. d

  dy/dx JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 622
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  pole mkuu,ila zile pesa zinafanya watu wajione matajiri mimi mwenyewe nilivopata kwa mara ya kwanza 667,500 ivi,sikujua hata nitumie vipi nilipata wenge ajabu but nilizitumia vema..nakumbuka kuna roommate wangu alinunua simu ya 300,000 kwa wenge..ni vema kuzitumia vizuri ziko kama zina mapepo vile as utashawishika kuzitumia vibaya...
   
 18. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  bwiru kwa Ndaki o even dat was fictional?
   
 19. S

  Suma mziwanda kageye JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah kwel umeandika kwajazba had point 10 unaxema one
   
 20. siansakala

  siansakala Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu alikuwa mzibua vyoo kule kwao
   
Loading...