Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,192
- 680
KIJANA Mohammed Ali Mohammed amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mmoja wa walinzi wanaolinda nyumba ya makamu wa rais Dk Ali Mohammed Shein Maisara Mjini Unguja.
Mtu ambaye anatuhumiwa kuwa mwizi alionekana maeneo ya gereje maarufu Gofu iliyopo katibu na nyumba ya makamu wa rais Kikwajuni (Bosnia) Mkoa wa Mjini Magharibi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma akizungumza kwa njia ya simu alithibitisha kutokea kwa kadhia hiyo ambapo alisema tukio hilo lilitokea usiku baada ya kijana huyo kuruka ukuta nyumbani hapo na kupigwa risasi kwa kuwa haikujulikana dhamira ya kijana huyo kupitia ukutani badala ya mlangoni.
Kamanda Juma alisema katika uchunguzi wa awali imemgundua kijana huyo kuwa na kisu kimoja na baadhi ya vifaa vya kutengenezea magari alivyokuwa ameviweka katika mfuko wake wa suruali aliyokuwa ameivaa wakati huo alipopatikana amenaguka chini baada ya kupigwa risasi kifuani na kuanguka chini.
Baadhi ya vijana walioshuhudia tukio hilo usiku wameeleza kwamba kijana huyo juzi alipita katika mitaa ya kikwajuni na kuiba power window ya gari zilizokuwa zimeegeshwa katika eneo hilo la Kikwajuni juu lakini baada ya kuonekana baadhi ya watu walimkimbiza na ndipo alipokimbia na kurukia kwenye kuta za makamu wa rais na kuingia ndani.
Nadhani hakujua maana jamaa walimtimua mbio sasa nadhani katika kupaparika kwake roho ndipo alipoona akimbilie katika ukuta ule na alipoingia ndani tu jamaa wale walinzi wakampiga risasi ya kifua na ndipo hapo tena alipoaga dunia alisema Issa Juma fundi wa magari katika mtaa huo wa Kikwajuni.
Mlinzi mmoja mbaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini alisema walipata taarifa hiyo na kuwa wenzao waliokuwa lindo walishituka walipomuona kijana huyo akiparamia ukuta wa nyumba waliokuwa wakilinda wenzake.
Tumesikia habari hiyo ya kutokea kijana kuparamia ukuta na pia tukasikia kwua walinzi walimpiga risasi lakini aliyepiga hasa sijui nani maana pale pana walinzi wengi kwa hivyo sijui nani kati yao aliyechukua uamuzi huo lakini kawaida kiongozi wa walinzi ndio mwenye kuchukua uamuzi au ndio mwenye kutoa amri na wengine huwa wanafuata tu alisema mlinzi huyo ambaye hakuwa katika ulinzi wa makamu kwa siku hiyo.
Walioshuhudia mwili wa marehemu wamesema wamekuta maiti ikizongwa na nzi asubuhi na ndipo wasamaria wema wakaichukua na kuipeleka katika hospitali kuu ya mnazi mmoja ambapo madaktari wa hospitali hiyo alithibitisha kupokea maiti na kuifanyia uchunguzi.
Ni kweli tumeipokea maiti hiyo na katika uchunguzi wetu wa awali tumeona kwamba kijana huyo amepigwa risasi kifuani lakini sisi jukumu letu kuchunguza na kuandiak ripoti za kidaktari na wataalamu watakuja kuchukua maelezo alisema Daktari mmoja ambaye alikuwa maeneo ya kuhifadhia maiti katika hospitali ya mnazi mmoja.
Wazazi wa marehemu wanaoishi ameneo ya Mikunguni na mkele jana wlaikusanyika katika mazishi ya kijana wao huku baadhi ya watu wakielezea kisa kilichomkuta kijana huyo ambaye hakuna mtu aliyeweza kutoa taarifa sahihi za kazi aliyokuwa akifanya kijana huyo wakati wa uhai wake.
Kila mja ataonja mauti na mtoto wetu ndio ameshaonja mauti ingawa inauma sana maana bora mtu umuuguze angalau machungu yake utakuwa unayajua lakini mwanao ametoka nje mzima halafu unaletewa maiti kwa kweli inauma sana lakini Mungu mwneyewe ndio anayeweza kutoa hukumu ya waja wake hatuna la kusema zaidi ya kushukuru Alhamdulillah alimalizia mama Asha Ali aliyekuwa katika msiba huo
source:Mlinzi wa makamu auwa kwa risasi | MZALENDO.NET