Mlinzi wa Makamu Rais Dr Shein auwa kwa risasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlinzi wa Makamu Rais Dr Shein auwa kwa risasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Sep 9, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  KIJANA Mohammed Ali Mohammed amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mmoja wa walinzi wanaolinda nyumba ya makamu wa rais Dk Ali Mohammed Shein Maisara Mjini Unguja.

  Mtu ambaye anatuhumiwa kuwa mwizi alionekana maeneo ya gereje maarufu Gofu iliyopo katibu na nyumba ya makamu wa rais Kikwajuni (Bosnia) Mkoa wa Mjini Magharibi.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma akizungumza kwa njia ya simu alithibitisha kutokea kwa kadhia hiyo ambapo alisema tukio hilo lilitokea usiku baada ya kijana huyo kuruka ukuta nyumbani hapo na kupigwa risasi kwa kuwa haikujulikana dhamira ya kijana huyo kupitia ukutani badala ya mlangoni.

  Kamanda Juma alisema katika uchunguzi wa awali imemgundua kijana huyo kuwa na kisu kimoja na baadhi ya vifaa vya kutengenezea magari alivyokuwa ameviweka katika mfuko wake wa suruali aliyokuwa ameivaa wakati huo alipopatikana amenaguka chini baada ya kupigwa risasi kifuani na kuanguka chini.

  Baadhi ya vijana walioshuhudia tukio hilo usiku wameeleza kwamba kijana huyo juzi alipita katika mitaa ya kikwajuni na kuiba power window ya gari zilizokuwa zimeegeshwa katika eneo hilo la Kikwajuni juu lakini baada ya kuonekana baadhi ya watu walimkimbiza na ndipo alipokimbia na kurukia kwenye kuta za makamu wa rais na kuingia ndani.

  “Nadhani hakujua maana jamaa walimtimua mbio sasa nadhani katika kupaparika kwake roho ndipo alipoona akimbilie katika ukuta ule na alipoingia ndani tu jamaa wale walinzi wakampiga risasi ya kifua na ndipo hapo tena alipoaga dunia” alisema Issa Juma fundi wa magari katika mtaa huo wa Kikwajuni.

  Mlinzi mmoja mbaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini alisema walipata taarifa hiyo na kuwa wenzao waliokuwa lindo walishituka walipomuona kijana huyo akiparamia ukuta wa nyumba waliokuwa wakilinda wenzake.

  “ Tumesikia habari hiyo ya kutokea kijana kuparamia ukuta na pia tukasikia kwua walinzi walimpiga risasi lakini aliyepiga hasa sijui nani maana pale pana walinzi wengi kwa hivyo sijui nani kati yao aliyechukua uamuzi huo lakini kawaida kiongozi wa walinzi ndio mwenye kuchukua uamuzi au ndio mwenye kutoa amri na wengine huwa wanafuata tu” alisema mlinzi huyo ambaye hakuwa katika ulinzi wa makamu kwa siku hiyo.

  Walioshuhudia mwili wa marehemu wamesema wamekuta maiti ikizongwa na nzi asubuhi na ndipo wasamaria wema wakaichukua na kuipeleka katika hospitali kuu ya mnazi mmoja ambapo madaktari wa hospitali hiyo alithibitisha kupokea maiti na kuifanyia uchunguzi.

  “Ni kweli tumeipokea maiti hiyo na katika uchunguzi wetu wa awali tumeona kwamba kijana huyo amepigwa risasi kifuani lakini sisi jukumu letu kuchunguza na kuandiak ripoti za kidaktari na wataalamu watakuja kuchukua maelezo” alisema Daktari mmoja ambaye alikuwa maeneo ya kuhifadhia maiti katika hospitali ya mnazi mmoja.

  Wazazi wa marehemu wanaoishi ameneo ya Mikunguni na mkele jana wlaikusanyika katika mazishi ya kijana wao huku baadhi ya watu wakielezea kisa kilichomkuta kijana huyo ambaye hakuna mtu aliyeweza kutoa taarifa sahihi za kazi aliyokuwa akifanya kijana huyo wakati wa uhai wake.

  “Kila mja ataonja mauti na mtoto wetu ndio ameshaonja mauti ingawa inauma sana maana bora mtu umuuguze angalau machungu yake utakuwa unayajua lakini mwanao ametoka nje mzima halafu unaletewa maiti kwa kweli inauma sana lakini Mungu mwneyewe ndio anayeweza kutoa hukumu ya waja wake hatuna la kusema zaidi ya kushukuru Alhamdulillah” alimalizia mama Asha Ali aliyekuwa katika msiba huo

  source:Mlinzi wa makamu auwa kwa risasi | MZALENDO.NET
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,495
  Trophy Points: 280
  Sijui, lakini what else could they have done in such a situation? Huenda angekamatwa na hao waliokuwa wanamfukuza wangemuua tu anyways. RIP....
   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,924
  Likes Received: 12,124
  Trophy Points: 280
  Walinzi walitakiwa waangalie kama ilikuwa threat kwao na maisha ya Shein na si kupigia risasi ovyo, wange m-contain na kumhoji anyway damu imeshamwagika hairudi RIP.
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hivi walinzi si hufundishwa kutumia silaha? au waliona huu ni wakati wa uchaguzi huenda ikawa ni hujuma?

  halafu hii ya kuiacha maiti tokea siku ikin'gon'gwa na nzi hadi asubuhi imekaaje? au mwizi hana ubinaadamu?
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Makamu wa Rais alikuwa ndani ya nyumba wakati huo?
   
 6. m

  mchakachuaji Member

  #6
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni umbumbu wa maaskari wetu, situation kama hiyo alitakiwa kutumia intelligence skill amkamate so farhajamfikia makamu anayomawasiliano ambayo angeweza kutoa amri au taarifa ili wamzunguke kiinteligencia, matokeo yake ndio hivyo ametumia unnecessary & unreasonabo excessive force kukabiliana na mtuhumiwa huyo, labda tungepata data za nini alchokuwa anataka na je anawenzake wezi atutajie tuwakamate pia. Yakheeeeeeeeeeeeee weye askari muuaji, hata kama labda ulikuwa umelegea kwa kufungaaa weye si ungeweka jitihadaaaa? Ujikaze kiumeeeee? Ni dhahiri hata weye utakuwa na iddi mbaya sasa, nenda katubu na uache uvivu wa kufikiri
   
 7. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #7
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  So many questions. So few answers.

  Innalillaahi Wa Innalillaahi Raaj'un!
   
 8. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni instant justice kwa sababu utaratibu mwingine kwa sasa haufanyi kazi. Mlinzi huyu ni makini na kazi yake
   
 9. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wenye kazi ya kukamata ni polisi na wameshindwa
   
 10. M

  Mutu JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mtu ambaye hana silaha si wangempiga silasi za miguu au ndio sabaha ndogo?
   
 11. T

  Tom Lyimo Member

  #11
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walinzi wetu wana matatizo sana
   
 12. W

  Wakuja Member

  #12
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very sad indeed, walinzi wanamuona mtu "anaparamia" ndani ya lindo lao hata silaha ya maana hana - wao wanachojua ni kumpiga risasi ya kifuani. Lol...
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sikubaliani na hiyo red texts. Mpo walinzi wengi, anaingia mtuhumiwa tena kwa kishindo, hatua ya pekee unamtandika risasi tena ya kifua inamaanisha walikuwa face to face, mtuhumiwa na kisu kiunoni mlinzi na bunduki mkononi.
  Either mlinzi hakuwa na ujuzi mwingine au ni hamu tu ya kutumia bunduki.
  Jeshini mlinzi kama huyo angepewa adhabu kali.
   
Loading...