Mlinzi anapofanya kazi ya customer care

Jimjuls

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
484
161
Nilikuwa jana ofisi za startimes Arusha maeneo ya Friends corner.Nilishangazwa na mlinzi kuwafanyia installment zile decoder zao na kuonyesha jinsi ya kuunganisha.Sasa huyu mlinzi anfanya kazi ya ulinzi au ndo customer care?Na hii nimeona kwenye maeneo mengi sana.Hivi wadau hii inakuja kweli?Ndo maana bongo customer care services ni ovyo ovyo tuuu.
 
kama kaifanya kwa ufanisi hiyo kazi aliyokuwa anawasaidia wateja kuna ubaya. wengine wanafanya kazi ya ulinzi sio kwa sababu hawana elimu ila shida tu akiwa anatafuta kazi nzuri zaidi na wengine wanaweza mambo mengi tu. ila kama aliharibu alichokuwa anafanya hapo kuna la kulijadili.
 
Bora hiyo kuna siku nilienda wizara fulani mlinzi wa getini akaanza kuniuliza unaenda kumuona nani??
Nikamwambia
Una shida gani??
Nikajiuliza what a hell hilo swali si natakiwa kuulizwa na customer care nikamwambia binafsi haimuhusu
Akasema binafsi haina jina?
Nikamwambia kama ningekuwa ninataka kukwambia wewe ningekuja moja kwa moja kwako ila mm nataka kwenda kwa huyo mtu
Kukatokea mabishano pale baadae nikamwambia haya namdai huyo jamaa na nimekuja kuchukua pesa yangu nikamtajia kiwango halafu nikamwambia nilipe wewe basi maana unataka kujua shida za watu
Akakaa kimya akaniambia ni sign niende ndani
 
Haina tatizo lolote lile

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Pale CRDB Azikiwe, kuna mlinzi yuko sharp na makini kwenye Customer care kuliko hata wahusika wenyewe
 
Ndio kazi halisi ya ulinzi au mtumishi yeyote ktk kampuni.si kitu cha ajbu ingawaje kwetu sasa ndio customer care inaanza kuingia

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ni bora kuhudumiwa na mlinzi kuliko hawa dada zetu unamkuta anaongea na simu ya bwana yake wewe mteja anakuona kama nuksi unamkatia stim.Mtapanga foleni kama una gauti utaomba kiti ukae.
 
Back
Top Bottom