Mlinzi adaiwa kutishia kumuua mke wa Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlinzi adaiwa kutishia kumuua mke wa Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema)

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Apr 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  UPELELEZI wa kesi ya kutishia kuua kwa maneno iliyofunguliwa na mke wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, Dar es Salaam, umekamilika.
  Hakimu Jonas Mahende anayesikiliza kesi hiyo aliutaka upande wa mashitaka kupeleka vielelezo mahakamani hapo ili kesi ianze kusikilizwa.
  Shauri hilo ambalo awali lilitajwa Machi 3 mwaka huu, lilifunguliwa na Lilian Mbowe baada ya kudai kuwa mlinzi wa klabu ya Bilicanas, Herman John (36), ametishia kumuua kwa kumtumia ujumbe mfupi wa maneno.
  Ilidaiwa mahakamani hapo na Karani Hatanawe Kitogo kuwa Februali 3 mwaka huu, katika club hiyo iliyopo wilayani Ilala, Dar es Salaam, John alitishia kumuua Lilian.
  Kitogo alidai kuwa, mshitakiwa alituma ujumbe mfupi wa maneno kupitia namba 0762 055605 uliosema kuwa anampa siku saba Lilian amuachishe kazi mtu anayeitwa Power, na kima cha chini cha mshahara wake kiwe 320,000 la sivyo atakuwa hatarini.
  Hakimu Mahende aliahirisha kesi hiyo ambayo jana ililetwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuleta vielelezo.
  Alimtaka mlalamikaji (Lilian ) awasiliane na mpelelezi wa kesi yake ili vielelezo viletwe mahakamani na kesi hiyo ianze kusikilizwa Aprili 14 mwaka huu.
   
Loading...