Mlinzi adaiwa kumpiga risasi mwananchi Morogoro

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
443
Reaction score
1,100
Mlinzi wa kituo cha mafuta cha Puma kilichopo Kata ya Kihonda Magorofani, Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kumpiga risasi mwananchi aliyekuwa ameegesha gari katika eneo la kituo hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda akiwemo mwandishi wa TBC, mwananchi huyo alikuwa ameegesha gari katika eneo hilo kwa lengo la kufanya ibada katika msikiti mdogo uliopo ndani ya kituo hicho cha mafuta.

Hata hivyo, bado haijafahamika rasmi chanzo cha tukio hilo wala hali ya mwananchi huyo baada ya kupigwa risasi.

TBC inaendelea kufuatilia taarifa zaidi kutoka kwa mamlaka husika kuhusu tukio hilo.
 
Mlinzi kama mlinzi ametuawakilisha vizuri kwenye hilo tukio.
Mna chuki sana wapuuzi nyie! Ndiomaana Samia anadili na nyinyi kiakili na bila kuwaangalia usoni! Nchimbi wenu kampiga chini, maana mlikuwa mnamtia ujinga kuwa kajiwekea ulinzi wakutosha,mara hakuna wakumtisha kanisa lipo nyuma yake!

Kiko wapi sasa na sharubu zake kama mfagio wa chachandu! Na bado mtatiwa sana adabu ....
 
Mlinzi wa Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Kata ya Kihonda Maghorofani, Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kumpiga risasi mwananchi aliyekuwa ameegesha gari katika eneo la kituo hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mwananchi huyo alikuwa ameegesha gari katika eneo la kituo hicho kwa lengo la kwenda kufanya ibada katika msikiti mdogo uliopo ndani ya kituo hicho.

Mpaka sasa chanzo cha tukio hilo bado hakifahamika na Jambo Tv inaendelea kufuatilia kwa mamlaka ili kujua undani wa tukio hilo


​
 
Mbona hao walinzi wanakuwaga makini? Kwanzia lini wameanza tabia kama za hawa migambo wanaopiga wamama mateke sokoni?
Kama kuna cctv itasaidia sana pande zote kupata haki
 
Nimeomba nipewe bastola huu mwaka wa tano sasa mm nataka bastola serikali inipe bastola.
 
Daah ni mwendo wa kujiamlia tu siku hizi.

Hadi mlinzi nae anapga risas kuua.??
INASKITISHA
 
Hivi hawa wanapitia kozi za ulinzi, kichwani huwa wako timamu?
Huyu achukuliwe na mkono was sheria uwe pembeni yake, ila km Taifa tulipofika ni pabaya, 😢😢😢
Hata wewe ungekua mlinzi usingekua timamu
Mtu unalala nje mwezi mzima ili uje kupewa laki mbili na nusu
 
Hivi kama tukio lina ushahidi kwanini bado linatamkwa kuwa inadaiwa kufanya hivi na vile wakati mtuhumiwa kafanya tukio wazi kabisa,
 
Uandishi wako ndo ulokuponza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…