Mlimuona Mwakyembe jana? Ana kipaji cha ajabu...

Mlimuona Mwakyembe jana? Ana kipaji cha ajabu...

...alafu mtu mwanaume mwenyewe anaelia wala hana uhusiano wa kindugu na marehemu...yani unawezaje kulia kuliko ndugu wa mfiwa!..unafiki wa ajabu...kwa msomi aliye na exposure..wala haielezeki...huyu mwakyembe amedhihirisha pasi na shaka hujma yake ya kumtoa lowassa u waziri mkuu...akishirikiana na marehemu....anyway...Mungu anawajibu....watalia sana misibani.,.

Eti Mungu anawajibi!! Hivi mtu akifa ina maana Mungu anakuwa amemuadhibu?? Wanaofariki wote inatokana na makosa yao kwa binadamu wengine?? Embu tumieni akili jamani, mnaudhi. Huyo Lowassa wenu nae atakufa. Je na yeye atakufa kisa kamkosea mwanadamu mwingine??!!! Wote njia yetu ni hiyo. Na mwenzetu akitangulia basi tumtakie mema huko alikoenda. Sio mlete siasa zenu hapa.
 
wewe ndo mnafiki kumlilia mtu sio lazma uwe nae sawa kimatendo...ndomana hata khadija kopa alimlilia asma...japo alkuwa ni adui wake wanajbshana vijembe...mwakyembe ametoa hisia zake za kwel kabisa...na binadamu alotimia n yule.mwenye kuweza kumlilia hata adui yake anapokufa au mtu yeyte ambaye alkuwa tofaut nae....www n mjinga husojua nankuelewa hisia na utu wa kibinadamu....sitta ametokwa na roho hakika ya roho ni chungu mno....acha upumbavu ....hata mm simkubali kabisa lowasa lkn kwenye siasa lkn sipend apate matatzo sipend aumwe na sipendi afe japo sote tutakufa nataman awe hai awe mzima niweze kupingana nae kwa mambo mengne......Mwenyezi mjalie sitta msamehe mdhambi aliyoyatanguliza na yanafomfatia...msamehe yeye na kizazi chake...amin

Naamini mtoa mada hapa atakuwa amekuelewa. Halafu yeye ndio mnafki kabisaaa. Analeta mzaha kwenye msiba!!.
 
Hehehehe hujakosea mkuu
Kama mwakyembe aliikana "thesis" yake iliyompa PhD kwenye bunge la katiba sioni kingine anachoshindwa kuigiza
 
Mimi naona Watanzania Ndio wanafiki, Leo tunajifanya kusahau Sitta alivyotufanya kwenye Bunge La katiba, tunamwona so pure hatuwezi kumfaninisha na Mwakyembe!!?
 
Kaka The Boss hujakosea...
Hamna mtu mnafiki kama Mwakyembe na jana amelidhihirisha hilo.
Unamlilia mtu ambae matendo yake na yako ni vitu viwili tofauti... Aibu iliyoje..!!
Maana kwa yale yote ambayo Sitta alikuwa ameyafanya kwa upande wa Mwakyembe ni opposite in a negative way..!!
Mwakyembe na Makonda ndio wemeonekana wakimlilia Sitta hadharani lakini hawana chembe ya mfanano wa lolote lile ni bora wangelia kimya kimya lakini kwa kuzungumza na kumuelezea marehemu kwa mazuri wakati wewe unayoyafanya ni kinyume chake ni AIBU kabisa.
Nakubaliana na The Boss, nakubaliana na wewe pia. Nakubaliana na nyie kuwa Mwakyembe na Makonda ni wasanii na hawafanani na marehemu Sitta kwa matendo. Ninachotofautiana na nyie hapa ni kwamba mtu kumlilia SANA marehemu yeyote yule huwa kuna sababu nyingi, na ile ya kufanana matendo inaweza isiwe mojawapo. Kuna watu wanalia tu kwa sababu machozi yao yako karibu, kuna wengine wanalia tu ili kuonyesha kama wameumizwa sana na msiba, kuna wengine hulia wakikumbuka ukaribu na hata ushirikiano waliokuwa nao baina yao na marehemu; nakadhalika.

Hii ya akina Mwakyembe na Makonda ni kielelezo tu cha namna jamii zetu zinavyojiweka unapotokea msiba wa mtu mkubwa. Huzidisha chumvi kiasi kwamba mambo chanya peke hutawala. Kwa mfano, wakati tumesikia uzuri wa Sitta ukitawala vinywa na hata coverage kwenye vyombo vya habari. Jamii haitaki tuone mambo mabaya ambayo Sitta ameyafanya ambayo kimsingi, yanaweza kuwa funzo kwa aliotuacha. Mfano, ni namna alivyowatukana maaskofu alipokuwa mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Jambo hili lina mahusiano makubwa sana na maisha ya binadamu kwa wale wanaoamini katika Biblia. Akina Mwakyembe na Makonda ni wasanii, na sanaa zao haziishii kwa marehemu Sitta, tutaendelea kuziona na walichokifanya kipuuzwe tu kama wanavyopuuzwa wasanii wenzao, maana hawa ndio wanatuharibia nchi!
 
Kwani kumlilia mtu mpaka matendo yenu yaendane!!? Huenda wana historia flan wewe huijui. Na pia kipindi kile cha richard wa monduli walifanya kazi vuzuri pamoja
Hata mimi nashangaa Kwan kumlilia mtu mpaka matendo yenu yafanane? Ajibu hili kwanza kabla hatujaendelea kuchangia hii post.
 
Kaka The Boss hujakosea...
Hamna mtu mnafiki kama Mwakyembe na jana amelidhihirisha hilo.
Unamlilia mtu ambae matendo yake na yako ni vitu viwili tofauti... Aibu iliyoje..!!
Maana kwa yale yote ambayo Sitta alikuwa ameyafanya kwa upande wa Mwakyembe ni opposite in a negative way..!!
Mwakyembe na Makonda ndio wemeonekana wakimlilia Sitta hadharani lakini hawana chembe ya mfanano wa lolote lile ni bora wangelia kimya kimya lakini kwa kuzungumza na kumuelezea marehemu kwa mazuri wakati wewe unayoyafanya ni kinyume chake ni AIBU kabisa.



Nahisi wanasiasa hao wawili walimlilia Sitta kwa sababu tofauti na za kisiasa! Yawezekana Mwakyembe anamkumbuka Sitta kama mmoja kati ya watu wachache sana waliokuwa karibu nae sana wakati akiugua kutokana na kinachosadikiwa kulishwa sumu na aliyesafiri hadi Appolo India kumjulia hali; Sijui! Makonda kasomeshwa na kuozwa na Sitta, ni sababu za msingi, sijui pia!
 
Tanzania yetu imebarikiwa wanasiasa wenye vipaji vya ajabu...

Kikwete anatajwa vipaji vingi tu ikiwemo kushawishi watu wamuunge mkono
akiwahiidi hiki na asiwape. Sitta sasa tunagundua alikuwa na kipaji cha kutumia wanasiasa wote tu wa upinzani na wa chama chake kufikia malengo yake.

Jana watu tulimuona Mwakyembe akionesha kipaji kingine kabisa,kipaji cha 'kugusa watu' kupitia msiba.

Jana watu walimuona Mwakyembe akilia na kuliza watu akimsifia Sitta na kusema yeye Mwakyembe nae ni 'mwanafunzi' wa Sitta.

Ilkuwa kama kumuona mwanafunzi akimlilia mwalimu wake aliyemkubali kuliko wote.

cha ajabu Mwakyembe huyu huyu 'anampinga kabisa Sitta' kwa matendo.

Sitta anasifiwa kwa bunge lenye meno,Mwakyembe anashiriki kuliondoa bunge la sasa meno.

Siita anasifika kuheshimu wapinzani na kuwapa nafasi,Mwakyembe anashiriki kuwakandamiza.

Sitta alisifika kwa uhuru wa vyombo vya habari hasa bunge live, Mwakyembe anashiriki kuua yote hayo.

Sitta alisifika kwa kupenda sheria na kanuni ziheshimiwe,Mwakyembe yuko tayari kuzipinda au hufurahia zikikiukwa mradi tu serikali ipate inachotaka.

Mwakyembe kaenda mbali zaidi kunukuliwa akisema 'taifa sasa halihitaji katiba mpya'.

Huku Sitta akiwa ndio mwenyekiti wa bunge la katiba iliyobaki kupigiwa kura tu.

Sitta atakumbukwa pia kwa kutokuwa mtu wa kujipendekeza kwa Rais au serikali bali misimamo ndo ilikuwa inampa nguvu, Mwakyembe amewahi kunukuliwa akimsifia Magufuli katika namna unayoweza kuiita ni kujipendekeza.

Wakati jana Mwakyembe anamlilia kwa nguvu Sitta nilibaki najiuliza Mwakyembe huyu hiki kilio ni cha moyoni au 'anatuonesha' tu kipaji chake kingine?

Nchi hii wanasiasa wana vipaji vingi sana kama kipaji cha kinyonga kubadili rangi kila mara.
Pale alikuwa anawaenzi bongo movie waliokuwepo. Tofauti nyingine yao ni namna walivyofika bungeni.Mmoja alikuwa anachaguliwa na wananchi ila mwingine utaalam wa kucheza na mabox ya kura ndio uliompeleka bungeni.
 
..wanaoleta siasa kwenye misiba ni wanaolia kinafiki kuliko hata ndugu a mfiwa....hii ndio hoja....


Eti Mungu anawajibi!! Hivi mtu akifa ina maana Mungu anakuwa amemuadhibu?? Wanaofariki wote inatokana na makosa yao kwa binadamu wengine?? Embu tumieni akili jamani, mnaudhi. Huyo Lowassa wenu nae atakufa. Je na yeye atakufa kisa kamkosea mwanadamu mwingine??!!! Wote njia yetu ni hiyo. Na mwenzetu akitangulia basi tumtakie mema huko alikoenda. Sio mlete siasa zenu hapa.
 
Kama ni tui la nazi,basi limeongezwa maji sana hadi radha haipo kumebaki rangi tu.

Mwakyembe wasasa sio yule alitengeneza jina.
 
Hata mimi nashangaa Kwan kumlilia mtu mpaka matendo yenu yafanane? Ajibu hili kwanza kabla hatujaendelea kuchangia hii post.
Issue ni kwamba alikua anahorodhesha mema aloyofanya marehemu ila Mwakyembe yeye binafsi anatenda kinyume chake.
Mfano: anapomsifia Sitta kuwa alikua anapenda uwazi bungeni at the same time yeye Mwakyembe hapendi uwazi na anasisitiza bunge lisirushwe live ili kusiwe na uwazi.

Kama sio uchawi huu ni nini?
 
Back
Top Bottom