Mlevi na Mahubiri

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Kuna mlevi mmoja alikuwa katokea kilabuni akapita karibu na Mahubiri na mambo yalikuwa hivi

Muhubiri: Ndugu zanguni tubuni ili muweze kwenda mbinguni, huko kuna asali
nyingi saaanaaa na maziwa mengiii ni nchi mpya tuliyoandaliwa

Mlevi akawaza moyoni mwake akaropoka

Mlevi: Kama huko mbinguni kuna asali nyingi saaanaaa basi kutakuwa na nyuki
wengi , sasa nani anataka kuenda huko akang'atwe na manyuki?

Muhubiri akabaki amebung'aaa tu
 
Mvuta bangi nae kapita karibu na msikiti..kaskia ustaadh anatoa hotuba "ndugu zangu muache dhambi manake huko jehanam kuna moto mkali sanaaa na mateso mengi"...mvuta bangi nae akaropoka kwa nguvu..."WATISHIE HAO USTAADH,WATISHIEEE !!! "
 
Mchungaji alienda Iceland kwa waeskimo na kuwahubiria neno la Mungu. Akawausia wawache madhambi kwani ahera kuna moto mkali sana.
Baada ya mwaka, alirejea na kukuta waeskimo wamezidisha madhambi. Alipouliza kulikoje, wakamwambia wanatenda dhambi ili waende motoni kwani kule baridi imewachosha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom