Mkwepa kodi mkubwa huyu hapa

Mkwepa kodi mkubwa huyu hapa

Sinema imekwisha mtuhumiwa mkuu kaingia Nchi Jirani na sasa anaelekea Somalia kumbuka zigo lote atabebeshwa Yeye hivyo kuwarahishia dhamana wote na huenda baadae kukawa na part 2 movie ingine.

Hii nchi kila mtu mwizi, tunaolialia hatujapata nafasi tu,

Kova na mimacho yake mchana kweupe anatuingiza madesa, million 20 hewa tu

Duuh li nchi letu kama li nchi la kusadikika,
 
naona wameona vema kutuletea picha kwa sababu jeshi la polisi limeshindwa kumkamata,,,,,,,

attachment.php

Sinema.........!!!!
 
Kova anajifanya hajui wakati wao ndio wanampa mbinu zote za kutoroka. Hii mijitu bana ni ile ile juzi jana leo kesho na kesho kutwa. Ht huyo padlocks watamwangusha tu. Watamchezea cheusi chekundu mchana kweupeee.

Huyu Kova nae ni jipu linalotakiwa kutumbuliwa haraka sana...........!
 
Huyo Msomali analindwa na Ofisa wa TRA anaitwa Gasper martini Mhina yupo TRA Temeke huyo ofisa kabla ya kuhamia huko alikuwa TRA mwenge anamiliki kikundi kikubwa cha wasomali, Wachina na wengineo weusi Watanzania ambao huwasaidia na kumlipa cash anamiliki nyumba nyingi kuliko masamaki, lakini ni mafia hakuna anayejua majina ya mali zake kwani kaandika majina ya Ndugu zake kwenye nyumba zake za Tanga, Dodoma, Arusha na Huko Dsm ana nyumba nyingi sana na huyo Msomali kamficha nyumbani kwake mbezi makabe anaandaa kumtorosha kwa njia ya barabara usiku hadi Zambia au malawi.

Kwanini usiisaidie Polis kumpata huyu mtu. Ukizingatia pia kuwa utapata milioni 20?
 
Mkuu Gaspar martin Mhina anaijua movie yote wakikaa naye chini watapata information zote lakini wajiandae vizuri kwani na yeye ni Mafia na mshirikina Hatari kwa kifupi kajipanga kwa vita mda mrefu.

Huyo Gasper Mhina ana Jeshi kubwa kiasi gani kupambana kwa Vita na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania !!!????
Kuwa makini na maandiko yako. Muulize Yericko Nyerere. Huyo Mhina atafikiwa na mkono wa Chuma muda si mrefu....mark my words.
 
Unataka kusema huyo Gasper mhina ni untouchable nagwa.. minyoo
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuwa kakimbia lazima awe yeye ndio mwenye makontena yote, nchi ya mihemko.
 
Huyo Gasper Mhina ana Jeshi kubwa kiasi gani kupambana kwa Vita na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania !!!????
Kuwa makini na maandiko yako. Muulize Yericko Nyerere. Huyo Mhina atafikiwa na mkono wa Chuma muda si mrefu....mark my words.

Acha kumtisha mwenzio, taarifa yake ni muhimu kuliko siasa za ccm na ufisadi wao
 
Haya wajasiriamali mliokuwa mnakwamishwa na mitaji. Mnaweza kuungana muunde jeshi, mnafanya msako duka kwa duka kwenye maduka ya kompyuta used pale Kariakoo
 
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za ?JAS EXPRESS FREIGHT LTD? na ?XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD? ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.
Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.
Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.

Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani.


mpaka sasa nina mashaka na taarifa hii ya MH KOVA,Lakini huyu jamaa ni muumini wa bandari zifuatazo jiefang,dicd,azam,ticts na ami,hasa dicd.

huyu alikua na mazoea makubwa sana,Manager wa bandari kavu ya dicd,Neema Mponezya,veronica msaidizi wa ofisi ya tra dicd,kwa sasa staff wote wa tra dicd wanaweza kukusaidieni polisi kupata mawili matatu.


baade ntaleta listi ya majina ya watu wake wa karibu,
 
Vipi kuhusu Jose Mlundi gaidi aliyeenda kutubu kwa Gwajima?vipi waliotdka kituo cha polisi Ushilombo na sitakishali,vipi kuhusu Kamrani wa kupandisha Twigwa hai kwenye ndege,Kova acha mazingaombe tuko kizazi cha 4G,muda wako wa kusitafu haujafika?
 
unaishia kuweka selo vichunusi wakati majipu unayapiga plasta na kuita makovu

Mkuu kwani hujui kuwa hawa no watu wa maigizo? Waweza kuta huyo jamaa alisindikizwa na polisi wenyewe hadi Namanga na Gari yenye bendera.
Mbona wale wauaji wa Arumeru waliotoroka mahakamani hata kuwatafuta hawawatafuti wala kuweka picha magazetini na kutangaza dau? Wanajua kwa vile wapo nchini wakifanya hivyo watakamatwa lakini huyo hata waseme zawadi bilioni hakuna wa kumpata
 
hapa ninachokiona ni kiini macho, huyu hausiki na lolote wanaacha kwenda kuwakamata kina bakhressa wanamtafuta kiwakala flan chenye ofisi ya mfukoni!!! ninachokiona hapa watataka kutuaminisha kua kila kitu ni huyu ndugu na wafanyabiashara waliobaki wote hawahusiki
 
Wasio na hela huwa wanawatafuta kimyakimya na kuwakamata ila wenye hela utashangaa wanatafutwa kwa vyombo vya habari baada ya kumwambia kimbiaaaaaaa. Yupo wai Alex Masawe, Kishimba alitafutwa kwa style hii kipindi meli imezama lakini leo ni mbunge na bado huyu nae anatafutwa kwa style hii.
 
hapa ninachokiona ni kiini macho, huyu hausiki na lolote wanaacha kwenda kuwakamata kina bakhressa wanamtafuta kiwakala flan chenye ofisi ya mfukoni!!! ninachokiona hapa watataka kutuaminisha kua kila kitu ni huyu ndugu na wafanyabiashara waliobaki wote hawahusiki
Hapo umenena maana alieotoa hizo container bila kulipiwa kodi na aliepokea hizo container bila kulipa kodi wote ni walwale tu
 
naona wameona vema kutuletea picha kwa sababu jeshi la polisi limeshindwa kumkamata,,,,,,,

attachment.php
Hao wote wapo kwenye list ya Gasper Mhina yeye ndiyo kinara wa kuwalinda wakwepa Kodi wote .
 
Ha ha mtuhumiwa wa kukwepa kodi anatafutwa na tochi dah
 
Back
Top Bottom