Mkwepa kodi mkubwa huyu hapa

Mkwepa kodi mkubwa huyu hapa

Huyo Msomali analindwa na Ofisa wa TRA anaitwa Gasper martini Mhina yupo TRA Temeke huyo ofisa kabla ya kuhamia huko alikuwa TRA mwenge anamiliki kikundi kikubwa cha wasomali, Wachina na wengineo weusi Watanzania ambao huwasaidia na kumlipa cash anamiliki nyumba nyingi kuliko masamaki, lakini ni mafia hakuna anayejua majina ya mali zake kwani kaandika majina ya Ndugu zake kwenye nyumba zake za Tanga, Dodoma, Arusha na Huko Dsm ana nyumba nyingi sana na huyo Msomali kamficha nyumbani kwake mbezi makabe anaandaa kumtorosha kwa njia ya barabara usiku hadi Zambia au malawi.

...Hakuna anaejua majina ya mali zake .... ila ww unajua!
 
minyoo huna namba ya simu ya Kamanda Kova?
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahah!! Hiyo imetoka yani hii nchi bhana!! Magufuli nilikupenda sana Ila ccm wamekupenda zaidi!! Magaidi yote yalivyo vamia kule Paris almanusura wadakwe kama siyo kujilipua!! Lakini hapa kwetu kumdaka tu mkwepa kodi mnashindwa???? Halafu kesho Mwenye hiyo passport atajitokeza na kusema yeye hausiki kwa namna yoyote ya ukwepaji kodi na wala siyo mfanya biashara!! Hii nchi bhana watu hawapo sirias hata kidogo
 
Yupo kajificha nyumbani kwa Mhina kule mbezi makabe Ndani ndani sana ni vigumu kufika.

Mkuu zawadi ya milion 20 imetolewa, si umchome ukamate huo mshiko tukanunue kiwanja Goba.
 
Kova anajifanya hajui wakati wao ndio wanampa mbinu zote za kutoroka. Hii mijitu bana ni ile ile juzi jana leo kesho na kesho kutwa. Ht huyo padlocks watamwangusha tu. Watamchezea cheusi chekundu mchana kweupeee.
 
naona kova kaamua kuja na bongo movie ya kufungia mwaka.
 
Mkuu zawadi ya milion 20 imetolewa, si umchome ukamate huo mshiko tukanunue kiwanja Goba.

Amkamate na minyoo nae atabaki salama?? Kwa million 20 Imtoe mtu uhai we unafikiri Kova ameshindwa kumkamata au hajui alipo?? Hii nchi bhana kama hujaisoma hutakaa uisome tena!! Magufuli hatoweza kupiga hatua lazma atakwama tu
 
We kweli famba wapi kataja majina ya mali anazo miliki???

'...kaandika majina ya ndugu zake kwenye NYUMBA zake anazomiliki Tanga, Dodoma ...' mie famba nimeona majina ya mali anazomiliki wewe je?
 
Amkamate na minyoo nae atabaki salama?? Kwa million 20 Imtoe mtu uhai we unafikiri Kova ameshindwa kumkamata au hajui alipo?? Hii nchi bhana kama hujaisoma hutakaa uisome tena!! Magufuli hatoweza kupiga hatua lazma atakwama tu
Aatake risk tu kuliko kukomaa nyuma ya keyboard.
 
Yupo kajificha nyumbani kwa Mhina kule mbezi makabe Ndani ndani sana ni vigumu kufika.

Mbona wewe umefika nakujua anakojoficha? Ina maana wewe una intelejensia kali kuliko polisi?
 
Wayii.......hakuna kitu.....tushachoka na sarakasi za namna hii.........tunahitaji aina mpya.........
 
Mbona wewe umefika nakujua anakojoficha? Ina maana wewe una intelejensia kali kuliko polisi?

Ndiyo maana yake lakini sasa Msomali yupo njiani anatoroka kuelekea Nchi Jirani
 
Watuhumiwa waweke wazi ni nani alikuwa analeta vimemo vya kupitisha makontena

Sinema imefungwa sasa Mtuhumiwa mwenye Siri katoroshwa hivyo tegemea kupata visingizio kuwa shahidi muhimu katoroka hivyo hakuna ushahidi tena.
 
Wakitaka wampate haraka atafutwe Gasper Mhina atawelekeza alipoelekea vizuri.
 
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za ?JAS EXPRESS FREIGHT LTD? na ?XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD? ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.
Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.
Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.

Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani.

Ikiwa hizo kontena zilichukuliwa contena yard ya azam mwenye kampuni alipie hiyo hasara kwani waliohusika ni wafanyakazi wake anaowalipa na kuwaamini yeye. Naamini mfumo wa malipo uko centralized kwenye system ya tra,bandari na out yard containers zote kwamba ukigonga tu utapata taarifa kuwa fulani amelipia container no. fulani lililopo bandarini au yard fulani inayomilikiwa na fulani hivyo mfanyakazi mhusika akiridhika analitoa hilo container na asipojiridhisha anapiga simu tra au lilikolipiwa kuthibitisha uhalali wa muamala fulani ulioletwa kwake. Haiwezekani container lolote liwe bandarini au bandari ya nchi kavu litoke bila kulipiwa na ankara zithibitishwe uhalali wake na zaidi ya maofisa wawili wahusika na wajiridhishe kabla kontena halijakabidhiwa kwa mhusika. Vivyo hivyo siamini kama document fake inaweza kupenyezwa hadi kwenye mtandao na jioni ya siku hiyo hiyo isiwe imegundulika kwani mizigo iliyotoka lazima ilingane na fedha iliyokusanywa. Ninachokiona hapa ni wizi wa kupangwa na jioni ya siku husika wahusika wa bandari na tra hukaa na kugawana au kama ni toka yard ya nje watagawana ofisi tatu kwani wote wataliona container kwenye computer system zao kwani ni centralized kila mmoja anaona kila transaction ya hela na container husika. Sasa kama haya ya 2014 kina Mwigulu na waziri wake walikuwepo lakini ajabu kateuliwa na raisi kwenye baraza lake. Hao kina Muhongo,Mwakyembe na Nape wake mbali ya kashfa za escrow na mabehewa yaliyoliingizia taifa hasara ya mabillion lakini nao wamo. Nape ni utovu wa maadili na uwezo mdogo kupewa wizara kamili. Tusubiri bunge la January litakuwa moto sana.
 
Back
Top Bottom