MKWELI UKWELI HUJAMTENDEA HAKI DR. SLAA PAMOJA NA CHADEMA
Ukiisoma Makala ya ndugu MKWELI UKWELI katika gazeti la Raia mwema toleo namba 259 utagundua sio tu kwamba ndugu Mkweli ana chuki binafsi na DK. Slaa na chama anachokiongoza cha CHADEMA bali pia haitakii amani nchi yetu kwa kuto ueleza uma wa watanzania ukweli kuhusu chanzo cha migogoro na vifo vya watanzania vinavyotokea katika mikutano mingi ya nje ya chama cha CHADEMA.
Katika makala hiyo ndugu Mkweli ameonyesha dhahili kwamba makala yake ilikuwa na lengo la kuwachonganisha watanzania na chama cha chadema kwa sababu katika makala hiyo ndugu mkweli ametoa hukumu mbaya moja kwa moja kwa chadema bila kuwa katikati ya pande mbili alizokuwa anazijadili ambazo ni CHADEMA NA SERIKALI, Kwanza kabisa ameanza kwa kukataa kuwa Dk.Slaa hastahili kufananishwa na mfalme Solomoni ,mimi hiyo naiona kama chuki binafsi kwa sababu aliyemfananisha Slaa na Mfalme Solomoni ulikuwa mtazamo wake yeye na si ustaarabu kupinga kwa sababu ule ulikuwa ni mtazamo wa mwandishi mwanakijiji .
Pili katika makala ile ndugu mkweli alieleza tu juujuu kwamba mikutano ya CHADEMA inasababisha vifo kwa watanzania bila kueleza kinaganaga ni jinsi gani CHADEMA ni chanzo cha vifo, napingana na ndugu Mkweli kwa kuangalia matukio machache yafuatayo ambayo ni miongoni mwa mifano ya Mkweli na ambayo mimi naona sio kosa la CHADEMA.
Tukio la Msamvu Morogoro, Katika tukio lile polisi wenyewe walionekania kujichanganya juu ya sababu ya kifo cha Yule kijana, polisi ambao wanavyombo vyote vinavyoweza kuchunguza chanzo cha kifo kile na kutoa majibu ya uhakika walijikanyaga na kuanza kusema kifo kile kilisababishwa na kitu kilichorushwa kutoka upande usiojulikana wakati mashuhuda walioshuhudia tukio lile wanasema ilikuwa ni risasi, hata kama ndugu Mkweli alishindwa kuwaamini mashuhuda labda kwa kuhisi kuwa walikuwa wanaitetea CHADEMA, lakini kwa jinsi polisi wanavyotenda kazi kukandamiza upinzani walishindwa kuchunguza na kugundua kuwa chanzo ni CHADEMA? Lakini tukiachilia mbali kitu kilichopelekea kifo kile na tukirudi tukio zima Mkweli haoni kuwa maandamano yale yalikuwa ni ya amani na hayakustahili nguvu kubwa kiasi kile? Hapo kosa la CHADEMA lipo wapi?
Tukio la Nyololo Iringa,Katika tukio hili vyombo vya habari vilionyesha jinsi polisi walivyokuwa wanamburuza mwandishi wa habari Daud Mwangosi ilhali akiwa na alama zote zinazomtambulisha kama mwandishi wa habari lakini bado walimburuza na hatimaye kupelekea kifo chake mbele ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, sasa hapa kosa la CHADEMA NA DR.Slaa lipo wapi? Na kama sikosei Mwandishi alipokuwa anaandika makala yale jeshi la polisi lilikuwa tayari limemfungulia mashtaka Mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi, kwa hatua hiyo tu unaweza kutambua kuwa CHADEMA hawahusiki na tukio kifo kile , kwa nini Mkweli amewashutumu CHADEMA kwamba ndio chanzo cha kifo kile?
Sababu nyingine inayonifanya nimuone Ndugu Mkweli kama mwenye chuki binafsi na Dr.Slaa pamoja na CHADEMA ni kitendo cha yeye kutoandika choachote kuhusu ile mikutano ambayo ilipelekea mauaji kwa wafuasi wa CHADEMA mfano lile tukio la Igunga ambalo kuna kijana alipotea katika mazingira ya kutatanisha na hatimaye kukutwa amekufa, Ndugu Mkweli hajazungumzia lolote kuhusu hili utafikiri ni mtanzania aliyekuja juzi na kukuta matukio hayo tu aliyoyasema yeye.
Hitimisho, napenda kumuomba mwandishi ili aeleweke vizuri ni bora ayaeleze matukio kwa kuangalia pande zote kwa kuzikosoa zilipokosea na na kuzisifu zinapofanya vema ili kuzifanya pande zote zijisahihishe na kuimarisha shughuli zao kwa maslahi ya Taifa.
Mimi ni msomaji wa Raia Mwema, Iringa