MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,353
- 22,922
Mwaka gani?Umenikumbusha mbali sana aisee!!!! Napamiss sana Mkwawa Complex School. Napamiss sana Makanyagio. Nalimiss sana bweni langu la Lumumba East ambapo pia nilikuwa kiranja wa bweni chini ya Mwalimu Mgimwa ambaye alikuwa Mwalimu mlezi wa bweni.
Nazimiss sana vurugu za maisha ya Mkwawa. Yaani kila mtu alikuwa na namna yake ya kwenda "preps" za jioni/usiku. Wakati wewe umelala bwenini ndio muda ambao mwenzako yumo darasani akipiga msuli wa kitabu na wakati ambao wewe unapanda juu huko academic zone ukajisomee utakuta unapishana na wengine wakienda kulala. Mkwawa ilikuwa raha sana na full kujiachia.
Nakumbuka sana baadhi ya wasichana kwenye combination yangu ya HKL walinisumbua sana kutaka ukaribu wa masuala ya kitaaluma lakini pia kuhusu mambo mengine yaliyokuwa yanaifanya shule kuwa complex zaidi yaani socialization. Hii yote ilikuwa kwa sababu ya uwezo wangu kitaaluma japo kifedha nilikuwa tu kapuku.
Mkwawa hakika ilikuwa sehemu nzuri kwangu ksomea kwani kulikuwa na everything in terms of reading materials.
Mimi nipo Mwanza
Mkwawa jamaniiiiii!!!!!!!