samahanini wenzangu kwa kuwakatisha stimu, lakini mimi naona hii agenda ni marketing strategy.
kila mtu anajua Rotam alikuwa na caspian kabla na baada ya vodacom, iweje voodacom ishambuliwe wakati caspian ipo?
mbona tunajidai wachambuzi lakini hakuna anaetaka kujua kiini cha Caspian yenyewe?
au kama rostam, au mojawapo ya kampuni tanzu zake anamiliki celtel au kampuni nyingine ya simu?
ina maana ukweli hautafutwi hapa?
siwezi kuamini hii data moja tu hapa ya share distribution ya vodacom ndio imelete mwamko mkubwa hivi wa watu 'kuhamia' celtel.
samahani tena
nahisi tunaendeleza 'hate' policies. Lengo liwe kuwa na nchi ambayo straight and transpatent policy zinafuatwa, sio kufuata upepo.
naomba kuwakilisha.