Mkuu ZITTO tatizo sio PINDA ni KIKWETE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu ZITTO tatizo sio PINDA ni KIKWETE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Apr 20, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mh ZITTO naona kama PINDA mnataka kumsukumia zigo la dhambi kwa kumuwajibisha kutokana na makosa ya mawaziri wengine. Kwa ni nini tusilie na yule aliyewateua na kuunda baraza lao. Tunajua Pinda naye alishiriki lakini mwenye maamuzi ya mwisho ni rais mwenyewe. Huyu rais kwani hajui ubovu na ubadhirifu wa mawaziri wake?

  Kwa nini asiwapige chini wote wanaotuhumiawa kwa uzembe? Nionavyo rais ndiye anayepaswa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kwa sababu masanamu aliyoyachonga yeye mwenyewe sasa yanamzidi akili na maarifa ya uhalifu. Hivi timu ikifanya vibaya anawajibishwa kocha aliyepanga timu? Au kapteni (nahodha) wa timu?
   
 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Tunaanza na mmoja mmoja!
   
 3. e

  evoddy JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Zitto alichosema yupo sawa maana kwa mujibu wa katiba ndani ya bunge huwezi kupiga kura ya kumwondoa waziri yeyote ispokuwa inapigwa kura ya kutokuwa na imani na serikari,bungeni waziri mkuu ndiyo anayesimamia shughuli za serikali
   
 4. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK(kichwa cha nazi pale magogoni) ndio anawatia kiburi. Kamng'ang'ania waziri wa afya mpaka leo bado yupo. Hata hao wenye tuhuma siajabu amekwisha waambia hakuna kujiuzuru. Nchi hii matatizo yanaanzia magogoni. Anachokifanya baba watoto huwa wanaiga. JK alivyo mwizi kwani wao hawaoni? ndiyo maana anauchuna wakifanya maovu ili wasije kumuumbua yakwake. Unataka kusema JK hajui kuwa Mkulo kavunja CHC kwa maslahi binafsi? naye ana pasu la mgao. Bandari ya Mtwara kuwapa wa Lebanon kwani JK hajui? mie nadhani tutafute sniper wa kutuondolea huyu mtu.

  Kumbuka EL alimuumbua kwenye vikao vya ndani kuwa kila alichokifanya alikuwa anajua..asituchezee.
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Acha ku DILUTE wewe mchakato umeshaanza na tumebakiza vipoint 6 ngoma inoge. Alipopashika Zitto ndo penyiwe haswaa!!!
   
 6. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hili nalo neno tungeanza na huyo aliyewaweka

  pengine ndiye anayewatuma ndo maana anakaa kimya

  kama hausiki angeshawapiga chini yeye ndiye mwizi wetu
   
 7. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  ndg zanguni haya yote tumekuwa kukiyaona, alisimama Dr. Slaa kwenye kampeini lakini kuna watanzania ambao vichwa vimejaa maji ya kijani na njano, yakatuangusha na yale majizi ya kura yakatuangusha - tusingefika hapa kama tungechukua maamuzi ya kuyang'oa ma sisiemu!
  Tatizo ni la watanzania wote ambao ni mbumbumbu.
   
 8. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkuu usemayo ni sawa, lakini mzunguuko wote huo ulikuwa na haja gani wakati ushahidi wa watu kufanya madudu uko wazi? Kwa rais kuwawajibisha wote. Hata waziri mkuu angetaka ilikuwa ni kitendo cha dakika 5 tu. Kwani rais haoni kama suala hili liko wazi na ushahidi upo?
   
 9. B

  Ba'mdgo JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba nikufamishe kitu kimoja, hizi ni kanuni pale mambo ya serekali napoenda kombo na moja ya tatu ya wabunge wakikubali kupia kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu kwa sababu yeye yuko pale kwa ajili ya serekali na kumwakilisha rais...na yeye waziri kuu ndo anayeshauri rais na kwa kuwa yeye ndiye anamwakilisha bungeni. akishauri rais akikataa basi alipaswa kuuzulu kwa kuubadhirifu wa mawaziri wake
   
 10. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hapo umesema ukweli. In fact hata Zitto analijua hilo. Lakini hana jinsi ya kumuokoa. Inabidi aondoke kwa manufaa ya taifa
   
 11. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mku ukitaka kuua nyoka unapiga mkiani? au kichwani? Kichwa cha nyoka ndicho chenye madhara. Mkia wa nini?
   
 12. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni kweli Tatizo la msingi ni JK ... "People pleaser", hata ukimweieka Mawaziri wazuri hataweza kuchukua maamuzi sahihi kwa wakti muafaka. Lakini kwa hali ilivyo kwakweli lazima kuchukua hatua kwa ajili ya heshima ya Nchi na wananchi lazima kufanyike jambo.

  Hatuwezi kusubiri hadi kumchukulia hatua Jk jambo lenye mshiko kwa sasa si lingine zaidi ya Kumwekea JK rekodi ya kuwa Raisi wa kwanza Kupoteza mawaziri wakuu wawili kupitia Bunge.
   
 13. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hiyo najua mkuu. Pamoja kanuni za bunge. Je rais hajui ubovu, wizi na ubadhirifu wa aliowaweka? Ushahidi si upo? Mbona kakaa kimya siku zote? Ndo maana nikasema kura za kutokuwa na imani naye zianzie kwake. Nyoka ni adui wa binadamu, tumpigapo tunaanza na kichwa hatuanzi na mkia wala kiuno.
   
 14. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tukumbuke kuwa, nchi za wenzetu wananchi wakichoka na kuanza kuandamana huanza moja kwa moja na harakati za kumtoa rais ama mkuu wa nchi. Mbovu si yule aliyeshindwa kuwajibika, mbovu ni yule aliyeshindwa kumuwajibisha yule ambaye hakuwajibika.
   
 15. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa mkulima kaonyesha effort gani katika kushughulikia ufisadi unaoripotia mwaka nenda mwaka rudi. kama hakubaliani na maamuzi ya rais kwa nini asijiuzuru na kumshitakia kwa wananchi waliompa dhamana ya nchi hii. Yule mama Banda pale Malawi alifanya nini. Kama jitu linakuwa joga lipate matunda ya uoga wake
   
 16. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  kaunga silencer mwana wa sinza
   
 17. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  huwezi kutoka kutambaa ukaanza kucheza soka... wacha aanze na kusimama, pinda ndio step one
   
 18. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo mmesahau kabisa kwamba hii siriKALI ni ya kishkaji zaidi....lazima kuoneana soo, kamwe kuwajibishana hakuwezi kuwepo.....mlitegemea nini?! Keep it up Zito.
   
 19. Zuia Sayayi

  Zuia Sayayi JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 834
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  au mm cjaelewa inamaana kwa sasa kuna sain 64?
   
 20. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Wala tatizo si Ki'wete, bali Watz kwanza walokubali huu mfumo uendelee!!!!
   
Loading...