Mkuu wa Wilaya ya Serengeti afariki dunia

MKUU wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Kapteni mstaafu James Yamungu amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa amelithibitishia Mwananchi kuhusu kifo cha Kapteni Yamungu kilichotokea jana saa 5 asubuhi katika hopitali ya Muhimbili ambako alifikishwa hapo Agosti 21, mwaka huu akitokea Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza alikokuwa amelazwa.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti, Magohe Zonzo ambaye alikuwa akimuuguza Bugando aliliambia gazeti hili kuwa taratibu za mazishi zinaandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Agosti 16, mwaka huu Yamungu alifikishwa katika Hospitali Teule ya Nyerere DDH wilayani Serengeti na kulazwa kwa saa tatu kisha kupewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando.

Kabla ya kufikishwa hospitalini hapo inasemekana mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Anita Motel iliyoko mjini Mugumu ambako alikuwa anaishi kufuatia nyumba ya Mkuu wa Wilaya kuwa inafanyiwa ukarabati alibaini Yamungu kuwa amezidiwa hivyo alitoa taarifa.

Alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ililazimika kufungua mlango na kumkuta hajitambui na kumpeleka hospitali ya Nyerere kabla ya kumhamishia Bugando.
 
R I P Mzee Yamungu. Sisi Serengeti tulikupenda lakini upendo wa Mungu umekuwa mkuu. Pengo lako kusema litazibwa na mtu mwingine lakini ombwe la fikra, utumishi, weledi na umahiri uliloliacha kamwe halitazibika!
 
Marehemu atakumbukwa kwa kitendo cha kumuunga mkono hadharani DC mwenzie aliyewachapa viboko walimu wa Bukoba Vijijini kitu ambacho kilipingana na msimamo wa mkweree lakini hakuchukuliwa hatua kwasababu ya uswahiba!! R.I.P Yamungu.
 
Msanii mmoja wa HIP HOP *JCB Wa arusha* alisema. . .''kaza buti kamanda, vazi la mwisho ni sanda''
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom