Mkuu wa Wilaya ya Serengeti afariki dunia

Familia ya Marehemu na Watanzania wote tujipe pole. Mh. D.C Pumzika kwa amani.
 
aisee JK wetu atakua busy sijui ataanzia msiba wa DC wake au atawahi ethiopia...Poleni kwa wafiwa

Lazima ataenda Ethiopia, huko kwa dc RC atosha kumuwakilisha. Anyway naona magamba yameanza kupiga ndogo kurithi nafasi iliyoachwa wazi.
 
captain mstaafu.hivi kila mtu akistaafu halafu akaitwa kwa jina lake itakuwaje?
.......injinia mstaafu,mwalimu mstaafu,nesi mstaafu,kuli mstaafu,dereva mstaafu,fundi viatu mstaafu!
 
Mkuu wa wilaya ya Serengeti afariki dunia katika hospitali ya taifa, Muhimbili. Mkuu wa mkoa wa mara bwana John J Tuppa ametoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari. Captain James Charles Lyamungu aliugua kwa mda mfupi na taarifa za kifo chake zitatolewa na ikulu.

Kama ndiye ninayemfahamu mimi ni Capt. James Charles Yamungu na si Lyamungu, ila kama amefariki au la sina uhakika maana habari zinazohusu vifo humu mara kadhaa zimeleta tafrani baada ya kufahamika si sahihi.
 
serengeti kule kwenye ishu ya ujenzi wa barabara mbugani?MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI AMEN!
 
Mungu amlaze mahala pema peponi, amina;

Inasikitisha sana kusikia Mzee Yamungu alikuwa bado mkuu wa wilaya badala ya kuwa mkuu wa mkoa, hasa ikizingatiwa utumishi wake uliotukuka, uadilifu, na pia kuwepo kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya kwa miaka karibia 20 (pengine kuzidi) huku watoto wake (kiumri) wakiteuliwa kuwa wakuu wa mikoa na wilaya; si ajabu wananchi wengi katika katiba mpya wangependelea mamlaka za uteuzi zitazamwe upya;
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom