Mkuu wa wilaya Singida aapa kupambana na Tundu Lissu, CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa wilaya Singida aapa kupambana na Tundu Lissu, CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, Jun 3, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa Wilaya ya Singida Pascal Mabiti akizungumza na wananchi wa Kata Mpya ya Lighwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

  [​IMG]

  Mkuu wa Wilaya ya Singida Paschal Kulwa Mabiti ameahidi kupambana na Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, kutokana na kile alichodai kuwa Mbunge huyo amewadanganya wananchi wasichangie fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo lake.

  Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi kwenye sherehe za uzinduzi wa Kata mpya ya Lighwa, Tarafa ya Mungaa katika halmashauri ya Wilaya ya Singida

  Kauli hiyo ya Bw. Mabiti imekuja baada ya risala ya wananchi kumwomba awasaidie katika kutatua tatizo la Mbunge huyo kuwalaghai wananchi wasichangie miradi mbalimbalai ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika jimbo hilo.

  Katika risala hiyo, wananchi pia wameiomba serikali kuwapatia msaada wa chakula ili kukabiliana na tishio la njaa, wajengewe ofisi ya kata, huduma ya maji safi kwa kuchimbiwa visima virefu na kukarabati bwawa kwa ajili ya matumizi ya mifugo yao.

  Amesema kuwa tabia ya Mbunge huyo kuwadanganya wananchi wasichangie miradi ya maendeleo kwa kuwa serikali inazo fedha za kutosha, haitavumiliwa na yeyote atakayepuuzia agizo hilo kuanzia sasa atashughulikiwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.

  Mabiti amesema wananchi wa Jimbo hilo wamekatazwa kutoa michango ikiwemo ushuru na ujenzi wa Sekondari, wakati kila mzazi au mlezi hutakiwa achangie Sh.500 kwa mwezi, kwa ajili ya posho ya mlinzi, mpishi, kuni na maji, huku Shirika la Chakula Duniani (WFP) lenyewe hugharamia chakula mchana kwa shule zote za msingi.

  Akijibu maombi hayo, Mabiti ameahidi serikali kutoa msaada wa kutosha wa chakula kwenye eneo hilo lililoathiriwa na mvua chache msimu uliopita, lakini amesisitiza kuwa chakula hicho kitasambazwa na watendaji wa kata na vijiji pekee, wakati wanasiasa hawataruhusiwa kujihusisha nacho.

  Amesema kata hiyo bado ni Mpya na ipo nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na maeneo mengine, hivyo zinahitajika juhudi kubwa kutoka kwa wananchi ili wajikwamue hapo walipo, ili baadaye iweze kukidhi mahitaji na huduma zingine muhimu.

  Kuhusu maombi ya bwawa, maji na ofisi ya kata, Mabiti ameiagiza kamati ya maendeleo ya kata chini ya diwani wake kukutana haraka kuandaa mikakati ya kutekeleza miradi hiyo, ili wananchi wachangie kwa kufuata utaratibu uliozoeleka wa ‘kipaumbele cha kwanza’, kulingana na mahitaji yao.

  Mapema akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Celestine Yunde alisema kata hiyo ni kati ya kata 19 mpya zilizotangazwa na serikali mwaka jana na kuifanya wilaya hiyo kuwa na jumla ya kata 47.
   
 2. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Anahutubia wananchi au anahutubia watoto wa shule?
   
 3. A

  Awo JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Anayechanga ni nani? Ni wananchi au Tundu Lisu? Maana kama Lisu amewaambia wasichange na wao wanataka kuchanga, si wataendelea kuchanga? Lisu hawezi kumzuia mtu anayetaka kuchanga asichange.
   
 4. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  inaelekea wanakijiji wa eneo hilo wote ni wanasheria
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sina nia ya kudharau lakini wakuu mmeona huo umati? wanafikia wangapi hao wananchi?
  Mbaya zaidi mwenyewe kapiga suti na tai huku 'UMMATI' ukionekana kupauka vibaya!
   
 6. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hillarious,kweli tuingie kwenye federal sysytem tu.Kazi za wakuu wa wilaya ni kutoa viapo vya kupambana na viongozi wa upinzani tu?Hiyo ndiyo mandate waliyopewa,loh
   
 7. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Exactly! Watoto wa shule hao.
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  Wana jf mtu ana njaa namna hiyo halafu unamwambia achangie pesa ya mlinzi etc!itawezekana?naona dc hana akili timamu
   
 9. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa kama wananchi hao wanakabiliwa na balaa la njaa watachanga nini? siwatumie pesa kidogo walizonazo kujinunulia chakula. Tundu Lisu analaumiwa kwa lipi hapo? Na Mabiti atapambana na Lisu kwa lipi? mbona anachekesha!
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  hahahahahahahhhaaaaaa
   
 11. S

  Shiri Member

  #11
  Jun 3, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  mkuu wa wilaya ni mtu mdogo sana kumtishia kamanda Lissu, na kufanya ivyo nikuwatishia wananchi waliomchagua Lissu uku yeye akiringia kubebwa na JK ili akitetee chama kilichokufa! wananchi tutaandamana nchi nzima uongozi wa kijinga kama wa ukuu wa Wilaya usiwepo, maana naona kazi yao ni kutumia ma Cruiser ya serikali kwenda kupata vikombe kwa babu tu!
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,648
  Likes Received: 21,857
  Trophy Points: 280
  Risala ya wananchi au risala ya Mtendaji wa kijiji au Kata? Wananchi hawana hata chakula watasema sie tunataka kuchangia. Tindu alisema wasichangie kwa vile halmashauri inarudisha hazina pesa za miradi eti hazikutumika na mwaka wa fedha umeisha, kosa lake nini?
   
 13. p

  politiki JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  MKUU wa Wilaya ya Singida, Paschal Mabiti amesema amedhamiria kupambana na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu, kwa kile alichodai kuwa Mbunge huyo anatumia mbinu chafu kukwamisha maendeleo ya eneo hilo.

  Mabiti alisema hayo jana kwenye sherehe ya uzinduzi wa kata mpya ya Lighwa, iliyopo tarafa ya Mungaa, Singida Mashariki.

  Wakazi wa eneo hilo kupitia risala yao walimuomba DC huyo awasaidie kuondoa sumu na hadaa iliyopandikizwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.

  Katika risala hiyo, wananchi pia waliiomba serikali kuwapatia msaada wa chakula ili kukabiliana na tishio la njaa, wajengewe ofisi ya kata, huduma ya maji safi kwa matumizi ya binadamu na mifugo yao.

  Mabiti alisema, tabia ya Mbunge huyo kuwadanganya wananchi wasichangie miradi ya maendeleo kwa kuwa serikali inazo fedha za kutosha, haitavumiliwa.

  Ameonya kuwa, yeyote atakayepuuza agizo hilo atashughulikiwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.

  Alisema, wananchi wa jimbo hilo wamekatazwa kutoa michango, ikiwemo ushuru na ujenzi wa sekondari wakati kila mzazi au mlezi hutakiwa achangie Sh 500 kwa mwezi kwa ajili ya posho ya mlinzi, mpishi, kuni na maji, na kwamba, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) hugharamia chakula cha mchana kwa shule zote za msingi.

  Mabiti aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa serikali itatoa msaada wa kutosha wa chakula, lakini akasisitiza kuwa chakula hicho kitasambazwa na watendaji wa kata na vijiji pekee na wanasiasa hawataruhusiwa kujihusisha na suala hilo.

  Alisema, kata hiyo bado mpya na ipo nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na maeneo mengine, hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kutoka kwa wananchi wenyewe ili wajikwamue walipo.
  source: habari leo.
  MY OPINION.
  Habari hii inaonekana wazi ni ya kutungwa, inakuwaje watu wanaomba chakula serikali kwamba wana njaa watu haohao wanalalamika kuwa wana pesa wanataka kuchangia wanazuiwa kwanini wasichukue pesa walizonazo kwanza wakanunue chakula kwa familia zao zenye njaa baada ya kuipa seriakli ambapo hakuna uhakika kama pesa hizo zitafanya kazi iliyopangiwa. it does not make sense.
   
 14. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  HIVI UKWELI NI UPI KWA WATU WENYE UELEWA WA KUTOSHA, WANANCHI HAO HAO KATIKA RISAL;A HIYO HIYO WANAMLAUMU MBUNGE WAO ALIYEWAMBIA WASICHANGIE MICHANGO. LAKINI WAKATI HUO HUO WANAWASILISHA OMBI LA KUPATIWA MSAADA WA CHAKULA KWA MKUU WA WILAYA. HAPO NI LAZIMA UJUMBE MWINGINE UMEPIKWA ILI MTU AJIPATIE UJIKO KUWA ANAPAMBANA NA CDM If you can not afford buying your own food, how possible you can avail your money to somebodyelse. kama tunaendelea kukubali kuwa kuna umuhimu wa kuw na wakuu wa wilaya basi "lets formulate a different job description for the RCs and DCs, this will be proper and a fitting decision for our country
   
 15. k

  kakin Member

  #15
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  anamuweza Tundu lissu??? au anatfuta matatizo maana sijui kama akili zake zipo timamu aache kupambana na mke wake akapambane na Tundu lisu mavi kweli huyu mkuu wa wilaya
   
 16. p

  plawala JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazee kama hawa wanatakiwa washaondoka kwenye system siku nyingi,tatizo ni kwamba hata ikichangwa inaliwa na wajanja,watu wenyewe wanaochanga ndio hao hao wanaomba kupatiwa msaada wa chakula
   
 17. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Source itakuwa habari leo au jamba leo
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hajui analolisema huyo bwana, anataka mchezo wa mawe wakati anaishi kwenye nyumba ya vioo?
   
 19. peck

  peck JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  njaa inapunguza ufahamu, ni njaa tu ya hawo wanakijiji(wanafunzi) ndio inawaponza hata uwezo wao wa kufikiri, sio rahisi kulalamikia mbunge kuwazuia kutoa michango at the same time unaomba msaada wa chakula
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Kwanini wanafungua kata shuleni? au wakaazi wa hiyo kata ni wanafunzi na waalimu wao tu!
   
Loading...