Mkuu wa Wilaya na OCD Serengeti wakamatwa wakifanya hujuma hifadhi ya Serengeti!

Sasa mjiulize ndege zinazotua na kuruka kwenda nchi za nje kutoka kwenye migodi yetu kule Nyamongo, Tulawaka, Buzwagi, Kahama, nk wanaondoka na nini? Tukisema tunaanchiwa mashimo matupu, Ngeleja anakasirika!
 
Hujamaliza, juu kwa juu. Nimekusihi uombe msamaha kwa kumwita Mwita muongo. Baada ya hapo ndipo mtakuwa pamoja.
Msafara wa Mamba na kenge huwa hawakosekani na ukiangalia vizuri utawaona mpaka mijusi na magong'ole..........mpuuze tu huyo kama wapuuzi wengine.
 
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti bw. Edward Ole Lenga akiwa ameambatana na watumishi kadhaa wa Wilaya hiyo wamekamatwa hivi karibuni wakiendesha hujuma ndani ya hifadhi ya Serengeti, eneo linalofahamika kwa jina la Goga.

Katika hujuma hiyo, DC ole Lenga alikuwa ameambatana na mkuu wa polisi Wilaya(OCD), Afisa Usalama wa Wilaya (DSO) pamoja na watumishi wengine wa vyeo vya chini.

Watu hao walikamatwa baada ya kuwekewa mtego na mkuu wa hifadhi ya Serengeti kufuatia taarifa za siri alizopenyezewa na wananchi.
Imedaiwa DC huyo kwa kushirikiana na wakuu wa vyombo vya dola wilayani humo OCD na DSO wamekuwa wakishirikiana na askari wa wanyamapori kuingia ndani ya hifadhi na kufanya ujangili pamoja na uchimbaji wa madini kinyume na sheria.

Kinachowasikitisha wananchi wa wilaya hiyo ni kitendo cha wakubwa hawa; DC, OCD na DSO kuachiwa huru huku watumishi wengine wakiendelea kusota ndani.

MY TAKE:
Vitendo hivi vya viongozi wakubwa katika wilaya kufanya uhalifu ndani ya wilaya waliyokabidhiwa kulinda na kuimarisha usalama ni cha kufedhehesha sana na kama tungekuwa ni nchi inayojali utawala bora, hawa watu walitakiwa kuwa wamejiudhuru nyadhifa zao na sasa wangekuwa wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma zao.
Lakini cha kusikitisha ni kwamba DC, OCD na DSO wako nje wakiendelea na majukumu yao huku watumishi wengine wa kada za chini walioshirikiana nao wakiwa tayari wamekamatwa na kufunguliwa mashitaka mahakamani.

Tunaomba uthibitisho wa madai yako.
 
Huyu juu kwa juu mbona anaharibu siku yangu: Mwita Maranya na wengine endeleeni kuleta habari na wanafiki kama huyu juu kwa juu ni wa kupuuza
 
Ocd amevuliwa wadhifa wake na kurudisha ofisi ya kamanda wa mkoa kwa mahojiano zaidi na hatua za kijeshi. Wananchi waliokuwa wameambatana nao wamekamatwa kwa uchunguzi.

Source: tbc taifa.

Mytake: Mkuu wa wilaya yupo juu ya sheria? Mbona hawajasema hatua alizochukuliwa?


Hili tukio na lile la kupakia nyara ya serikali mchana kweupe uwanja wa ndege halina tofauti!

Dawa ya hawa mafisadi ni wa kuwatoa madarakani tu kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini!
Ama sivyo hawa mafisadi watutuuza ingali tupo macho mchana kweupe!


sisiem ni JANGA kwa Nchi yetu ya Maziwa na ASALI!
 
ndugu yangu jasusi mie siuombi msamaha kwa kuwa mwita hakuwa makini alipoleta hiyo taarifa humu jf. wana jf tujifunze kupost inf yenye ukweli ama ni taarifa .kama ni tetesi hapo sawa au aweke swali kwa maana hana uhakika wa jambo hilo. humu ndani kuna watu wengi wanaojua mambo au walio katika maeneo mbalimbali ndio maana jf imeendelea kuimalika ,kama zitawekwa taarifa zenye mchanganyiko na usiokuwa ukweli basi tutapotoshwa. nafunga mjadala huu .stop
 
Naomba tuweke adhabu ya kunyonga watu kama hao waliopewa dhamana halafu wao wanafanya kinyume!
 
kwa mazingira hayo inabidi wakumbane na wananchi wenye hasira kali kama vibaka wengine tu... hatuwezi kuendelea kuwaamini viongozi ambao tunajua ni wezi
 
Wacha wachukue tu madini na wanyama wao, nacho shauri waachiwe huru kwani wengi wameiba sana mali za umma wapo huru, sasa hao washikwe wamekosa nini? Wacha tuendelee na siasa.

Hakikwanza!!nimeipenda sana comment yako mkuu!!niliwahi kuandika humu JF kwamba kwakuwa watanzania hatujakubaliana kuijenga nchi basi kila mtu ahangaike tu ili aishi,EMBU fikiria mtu kama naibu waziri Malima Mr. MOROGORO pesa alizokuwa nazo huenda zimetoka kwenye mikataba feki ya madini tuliyonayo ambayo ni haki ya kila mtanzania!!sasa tuendelee kuwaacha wachache wafaidi? la hasha!!acha kila mmoja wetu ahangaike kutumia resources tulizonazo kwa namna anayoona inafaa.Mm naona sawa tu walivyofanya sababu kila mtu sasa anaangalia tumbo lake zaidi hakuna wa kumletea maendeleo mwingine humu huo ndio ukweli kwetu sisi wadanganyika!! HUTAKI UNAACHA PITA TU UTACHANGIA BAADAE!!
 
Back
Top Bottom