Mkuu wa Wilaya na OCD Serengeti wakamatwa wakifanya hujuma hifadhi ya Serengeti! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Wilaya na OCD Serengeti wakamatwa wakifanya hujuma hifadhi ya Serengeti!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Mar 27, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa Wilaya ya Serengeti bw. Edward Ole Lenga akiwa ameambatana na watumishi kadhaa wa Wilaya hiyo wamekamatwa hivi karibuni wakiendesha hujuma ndani ya hifadhi ya Serengeti, eneo linalofahamika kwa jina la Goga.

  Katika hujuma hiyo, DC ole Lenga alikuwa ameambatana na mkuu wa polisi Wilaya(OCD), Afisa Usalama wa Wilaya (DSO) pamoja na watumishi wengine wa vyeo vya chini.

  Watu hao walikamatwa baada ya kuwekewa mtego na mkuu wa hifadhi ya Serengeti kufuatia taarifa za siri alizopenyezewa na wananchi.
  Imedaiwa DC huyo kwa kushirikiana na wakuu wa vyombo vya dola wilayani humo OCD na DSO wamekuwa wakishirikiana na askari wa wanyamapori kuingia ndani ya hifadhi na kufanya ujangili pamoja na uchimbaji wa madini kinyume na sheria.

  Kinachowasikitisha wananchi wa wilaya hiyo ni kitendo cha wakubwa hawa; DC, OCD na DSO kuachiwa huru huku watumishi wengine wakiendelea kusota ndani.

  MY TAKE:
  Vitendo hivi vya viongozi wakubwa katika wilaya kufanya uhalifu ndani ya wilaya waliyokabidhiwa kulinda na kuimarisha usalama ni cha kufedhehesha sana na kama tungekuwa ni nchi inayojali utawala bora, hawa watu walitakiwa kuwa wamejiudhuru nyadhifa zao na sasa wangekuwa wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma zao.
  Lakini cha kusikitisha ni kwamba DC, OCD na DSO wako nje wakiendelea na majukumu yao huku watumishi wengine wa kada za chini walioshirikiana nao wakiwa tayari wamekamatwa na kufunguliwa mashitaka mahakamani.
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii ni hatari sana manake nimekuwa najiuliza ikiwe ile dhahabu ya kilima fedha kama itabaki salama chini ya watawala wenye uchu na tamaa ya fedha kuliko utu. Kumbe sasa nimeelewa kwa nini wakubwa wanakodolea macho serengeti.
   
 3. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mwita maranya, habari yako sio ya kweli, wewe muongo sana, thread zako zote hazikaa ziaminike hapa jf kwa vile unapost bila kuwa na taarifa za kutosha. soma gazeti la mwananchi la juzi tarehe 24 ndio utapata taarifa iliyo sahihi. acha kupotosha wananchi. muongo sana wewe.
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Na bado yuko ofisini.
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Taarifa yenyewe ya Mwananchi haina mshiko. Imeweka majina yote kapuni.

  Maofisa polisi mbaroni kwa kuchimba madini Serengeti

  MAOFISA waaandamizi wa Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa pamoja na watu wengine watano wamekamatwa wakichimba dhahabu katika eneo Kilimafedha ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti (Senepa).

  Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), zinasema watu hao walikamatwa wakiwa na sururu, koleo, nyundo, viroba 10 vipya na kifaa cha kupimia dhahabu. Tukio hilo limetokea Machi 23, asubuhi na maofisa hao walikamatwa wakiwa na gari la polisi. Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi alithibitisha kukamatwa kwa maofisa hao (majina tunayo) na kufafanua kuwa watu hao wanahojiwa na mamlaka husika ili kukamilisha taratibu.

  "Nimepata taarifa kutoka kwa mhifadhi wa Senapa, nilikuwa safarini, wameniambia kuwa wanaendelea kuwahoji. Kwa ujumla hatutaliachia suala hilo, mamlaka zilizotakiwa kulinda maliasili ndizo zihusike kuhujumu! Wakibainika kuhusika lazima sheria ichukue mkondo wake,"alisema na kuongeza:

  "Kama watakuwa wamehusika kuchimba madini ndani ya hifadhi hawashindwi kuungana na majangili kuua wanyama kama tembo na wengineo. Kesho nitakuwa ofisini, nitafute nitakueleza zaidi maana sisi hatuna vyombo vya kisheria tutawapelekea wahusika kama itathibitika."

  Habari zaidi zinaeleza kuwa hadi jana jioni maofisa hao walikuwa bado wakihojiwa katika ofisi ya Mhifadhi Mkuu wa Seronera. Imeelezwa kwamba maofisa hao waandamizi wa usalama waliondoka mjini Mugumu wakiwa na vijana wanaodaiwa kuwatumia kwa kazi hiyo na kupitia katika Lango la Fort Ikoma wakiwa na gari hilo likiwa limefungwa turubai na ndani wakiwemo watu watano ambao hawakukaguliwa kama utaratibu unavyoagiza.

  "Wamefika hapa getini saa 12 asubuhi wakiwa wamefunga turubai wakidai wako watatu dereva na kuwa wanakwenda kikazi Serena lodge, hatukuwakagua kwa kuwa maofisa wanafahamika, tuliwaamini," alisema mmoja wa watu waliokuwa kwenye lango hilo. Alisema baada ya maofisa hao kupita walitoa taarifa sehemu mbalimbali za uongozi wakidhani kuwa kulikuwa na ugeni unaotembelea hifadhini humo.

  "Maofisa walipokataa kuwa hakuna mgeni ndani ya hifadhi ilibidi askari wa doria kuanza kufuatilia maeneo yote ikiwamo eneo la Kilimafedha ambako wanyama kama Faru huhifadhiwa, ndipo walipowakuta vijana wakichimba huku maofisa hao waliokamatwa wakiangalia," alisema mtoa habari huyo. Ilidaiwa kuwa ofisa mwandamizi wa polisi wilaya aliyekamatwa alikutwa akiwa na bastola na alipohojiwa alidai kuwa walikuwa wanafuatilia watu wanaodaiwa kuingia na bunduki eneo la hifadhi.

  Baadhi ya askari wa hifadhi hiyo wamedai kuwa mtandao wa watu hao ni mkubwa ukihusisha pia baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali ambao ndiyo wanunuzi na wafadhili wa matukio hayo yakiwemo ya ujangili wa meno ya tembo. Walisema sababu za kusaka bunduki bila mhifadhi wala askari wengine kuwepo hazikuwa na maana kwa watu hao ambao awali, walieleza kuwa wanakwenda eneo la Seronera tofauti na walipokamatiwa.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz alisema hajapata taarifa za tukio hilo kwa kuwa alikuwa kwenye kikao. Kwa upende wake, Mhifadhi wa Senapa, Mtango Mtahiko hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo akisema alikuwa hajapata taarifa kamili.

  http://174.132.155.185/news/4-habari-za-kitaifa/21408-maofisa-polisi-mbaroni-kwa-kuchimba-madini-serengeti.html
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sasa ndugu yangu juu kwa juu unachotakiwa kufanya hapa ni kumwomba radhi Mwita Maranya kwa kumuita muongo. Maranya ametusaidia kujaza dots na majina yaliyofichwa kwenye ripoti ya Mwananchi.
   
 7. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mwita Maranya nae still ameendeleza ambiguity,hajataja kinaga ubaga majina ya wote i.e OCD anaitwa nani?kamtaja taja Ole Lenga tu,,anyway hii inanikumbusha tukio la Dodoma-Mpwapwa ambapo DSO,OCD na DC wote walijimilikisha vitalu vya uchimbaji kwa kutumia madaraka/vyeo/nafasi zao tu! serikali hii mmmmmmmmh!
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wote katika serikali hii wanafanya hivyo hivyo kwa kufuata mfano wa wakubwa wao; mfano ni pale mkoa wa Singida ambapo mkuu wa mkoa Koney amejimilikisha vitalu vya madini kule Sambaru!!
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kumbe imesambaa eh? Watu wanaingia kuvuna humo na gari za polisi.
   
 10. S

  STIDE JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Uchunguzi upi wakati wamekamatiwa eneo la tukio na VIZIBITI!!!? Kamata mijitu hiyo weka Segerea!!! Hii serikali vp!!!!??
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ocd amevuliwa wadhifa wake na kurudisha ofisi ya kamanda wa mkoa kwa mahojiano zaidi na hatua za kijeshi. Wananchi waliokuwa wameambatana nao wamekamatwa kwa uchunguzi.

  Source: tbc taifa.

  Mytake: Mkuu wa wilaya yupo juu ya sheria? Mbona hawajasema hatua alizochukuliwa?
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  nimeipenda sana nilipohadhithiwa na afande mmoja. Hata kama wameachiwa lazima sheria ichukue mkondo wake
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160

  Mkuu inaonekana una chuki binafsi na Mwita Maranya au umekurupuka kwenye kuchangia hapa!

  Taratibu Mkuu, just be a great thinker!
   
 14. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,929
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  sasa unachosisitiza Mwita Maranya ni muongo bila kutoa hoja yako ni nini?kati ya mwita na wewe nani muongo? Au wewe ndiyo OCD mwenyewe!
   
 15. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Wacha wachukue tu madini na wanyama wao, nacho shauri waachiwe huru kwani wengi wameiba sana mali za umma wapo huru, sasa hao washikwe wamekosa nini? Wacha tuendelee na siasa.
   
 16. escober

  escober JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  huyo atakuwa ndiye OCD au DC aliyedakwa
   
 17. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  sio mkuu wa wilaya,ni afsa usalama na ocd,fanya utafiti before
   
 18. only83

  only83 JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hii nchi ni ya kishenzi kwelikweli.Sasa tunaowapa dhamana ya kulinda mali zetu ndio wanafanya kazi ya kuiba.Ni bora sasa tuchukue hatua wenyewe kulinda nchi yetu.
   
 19. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  RPC Mara ametoa tamko. Anasema wao wamechukua hatua kwa kumhamishia OCD makao makuu ya Polisi mkoa. Eti hiyo ndiyo adhabu stahiki. This country bwana!
   
 20. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  What a post!!
  Nyie watu mtapata akili lini nyie!???
   
Loading...