Mkuu wa Wilaya na OCD Serengeti wakamatwa wakifanya hujuma hifadhi ya Serengeti!

Hii nchi ni ya kishenzi kwelikweli.Sasa tunaowapa dhamana ya kulinda mali zetu ndio wanafanya kazi ya kuiba.Ni bora sasa tuchukue hatua wenyewe kulinda nchi yetu.
Hawa nao wanafuata njia za wakubwa waliowateua. Usisahau hawa wanawajibika kupeleka kitu kidogo kwa wakubwa wao kila baada ya kipindi fulani. Tuliamua kubomoa msingi wa taifa, hakuna njia nyingine, lazima taifa lenyewe liendelee kubomoka.
 
Kwa taarifa za ndani nilizonazo toka kwa mtu wa ndani kabisa Wilayani Serengeti, ukweli wa mambo ni kwamba shughuli nzima inawahusisha Mkuu wa Wilaya(DC), Kamanda wa polisi Wilaya(OCD) na Afisa Usalama wa Wilaya(DSO).

Haya sasa tumewafahamu, Sasa tutawafanya nini?
 
Ocd amevuliwa wadhifa wake na kurudisha ofisi ya kamanda wa mkoa kwa mahojiano zaidi na hatua za kijeshi. Wananchi waliokuwa wameambatana nao wamekamatwa kwa uchunguzi.

Source: tbc taifa.

Mytake: Mkuu wa wilaya yupo juu ya sheria? Mbona hawajasema hatua alizochukuliwa?

Kwanini OCD avuliwe wadhifa wake na kurudishwa kwa ofisi ya kamanda wa polisi mkoa(RPC)?
Je hiyo ndio adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria? kwanini hakupelekwa mahakamani kama walivyofanya kwa watumishi wengine?

Hii inaweza kuwa ni mbinu ya kuwanusuru OCD, DSO na DC, kwani akipelekwa mmoja mahakamani, nadhani watalazimika pia kuwaburuza wote mahakamani.
 
Wakuu mimi nipo hapa Mugumu makao makuu ya wilaya ya Serengeti, hizi taarifa ni za UKWELI KABISA na wala sio uzushi hata kidogo. Kwa kifupi hapa Mugumu polisi ni patashika wamejaa wanausalama, anaepinga hajui anachokipinga maana sie ndo tupo eneo la tukio huku huku Mugumu Serengeti
 
Afadhali mdau uko Mugumu utatusaidia kutupa current news toka eneo la tukio.

Hao wanausalama waliojazana hapo Mugumu wametoka wapi? kwakuwa afisa usalama wa wilaya naye ni mtuhumiwa, haitarajiwi kwamba anaweza kushiriki kujiwajibisha ama kuwawajibisha polisi na mkuu wa wilaya.

Na vipi kuhusu waliofunguliwa mashitaka na kufikishwa mahakamani jana?
 
mwita maranya, habari yako sio ya kweli, wewe muongo sana, thread zako zote hazikaa ziaminike hapa jf kwa vile unapost bila kuwa na taarifa za kutosha. soma gazeti la mwananchi la juzi tarehe 24 ndio utapata taarifa iliyo sahihi. acha kupotosha wananchi. muongo sana wewe.

Hivi na wewe Juu kwa Ju ni GT? Kama Maranywa amesema uongo, basi wewe twambie UKWELI ni upi kuliko kutoa hizo blanket statements. Kumuita mtu muongo hakumfanyi awe muongo bila kuonesha uongo wake. Indeed wewe ndiyo umeonekane muongo.
 
Hi nchi iuzwe kila mtu apewe chake tujue lakufanya . Yaani kila mtu ni mwizi.
 
mwita maranya, habari yako sio ya kweli, wewe muongo sana, thread zako zote hazikaa ziaminike hapa jf kwa vile unapost bila kuwa na taarifa za kutosha. soma gazeti la mwananchi la juzi tarehe 24 ndio utapata taarifa iliyo sahihi. acha kupotosha wananchi. muongo sana wewe.

Habari ni ya kweli kabisa, imerushwa na Wapo radio katika kipindi chao cha patapata cha jumapili saa moja na robo asubuhi. Mwita hajaongeza chochote wala kupunguza. Wewe ndo muongo kwa kutegemea source moja tu ya habari. Infact mimi serengeti ni kwetu tena kijiji cha issenye so mbali na habari za radio nina other altenative kupata habari hizo. Usiwatetee mafisadi wanaoihujumu serengeti

Afadhali mdau uko Mugumu utatusaidia kutupa current news toka eneo la tukio.

Hao wanausalama waliojazana hapo Mugumu wametoka wapi? kwakuwa afisa usalama wa wilaya naye ni mtuhumiwa, haitarajiwi kwamba anaweza kushiriki kujiwajibisha ama kuwawajibisha polisi na mkuu wa wilaya.

Na vipi kuhusu waliofunguliwa mashitaka na kufikishwa mahakamani jana?

Kwa taarifa za sasa huyu afisa usalama kasimamishwa kazi tayari
 
Hapo ndio utajua Serikali gani tulionayo kwa sasa!!! Serikali ya kinyanganyi, wezi, wakwapua rasilimali zetu... Duuu hii habari imenisikitisha sana.
 
wana jf sasa mmepata taarifa sahihi. Jama yangu anasema wahusika ni ocd na dso na wananchi wa kawaida 5 . Kwa hiyo hao dc na askari wanaolinda wanyama au mbuga hiyo ndio waliowadaka au waliowakamata wezi hao wa mali za nchi baada mmoja wa askari polisi kuwapa taarifa za siri. Tupo PAMOJA MWITA. Wengine hapa jf tunapategemea kupata taarifa za namna nchi au dunia inavyokwenda maana hatuna acces na watawala sasa mtu anapost taarifa ambazo hazina ukweli wa kutosha inashusha HESHIMA YA JF.
 
Hii nchi ni ya kishenzi kwelikweli.Sasa tunaowapa dhamana ya kulinda mali zetu ndio wanafanya kazi ya kuiba.Ni bora sasa tuchukue hatua wenyewe kulinda nchi yetu.

Mkuu hiyo ndio kauli mbiu ya CCM Wizi kwanza nchi baadae.
 
Unaandika ukiwa wapi ???? Umekasirika mno au vipi ??? Hasira hasara !!!
wacha wachukue tu madini na wanyama wao, nacho shauri waachiwe huru kwani wengi wameiba sana mali za umma wapo huru, sasa hao washikwe wamekosa nini? Wacha tuendelee na siasa.
 
Watanzania 2ache ubinafs, kweli m2 unapewa dhamana ya ku2nza mali ya umma halafu wewe unahujumu! 2we na sheria kali huenda ikasaidia.
 
sio mkuu wa wilaya,ni afsa usalama na ocd,fanya utafiti before
Na wewe ndio mbumbumbu wa kwanza, kila Muajiliwa wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Afisa usalama, huyu unatakiwa umuite kwa rank yake nayo ni DSO........ Mijutu mingine humu hovyo kweli kweli, akili ukwaju mtupu!
 
wana jf sasa mmepata taarifa sahihi. Jama yangu anasema wahusika ni ocd na dso na wananchi wa kawaida 5 . Kwa hiyo hao dc na askari wanaolinda wanyama au mbuga hiyo ndio waliowadaka au waliowakamata wezi hao wa mali za nchi baada mmoja wa askari polisi kuwapa taarifa za siri. Tupo PAMOJA MWITA. Wengine hapa jf tunapategemea kupata taarifa za namna nchi au dunia inavyokwenda maana hatuna acces na watawala sasa mtu anapost taarifa ambazo hazina ukweli wa kutosha inashusha HESHIMA YA JF.
Hujamaliza, juu kwa juu. Nimekusihi uombe msamaha kwa kumwita Mwita muongo. Baada ya hapo ndipo mtakuwa pamoja.
 
Back
Top Bottom